London, England. Kiungo wa Arsenal, Henrikh Mkhitaryan, amemwaga chozi baada ya kuambiwa na daktari kuwa majeruhi aliyoyapata yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Madaktari wamemwambia mchezaji huyo aliyeumia Jumatano iliyopita katika mechi ya Kombe la Ligi ambayo walipoteza kwa kufungwa 2-0 na mahasimu wao Tottenham Hotspur anaweza kukaa nje hadi mwisho wa msimu huu.
Kiungo huyo aliumia mguu sehemu ya misuli mkubwa wa uliopo kati ya dole gumba na kifundo cha mguu ‘ankle’ siku tatu tangu aifungie Arsenal mabao yote ilipofungwa 3-2 na Southampton katika Ligi Kuu England.
Mchezaji huyo kutoka Armenia, aliyetua Arsenal siku ya mwisho ya usajili wa Januari mwaka huu, akitokea Manchester United anaamini benchi litamnyima fursa ya kutoa mchango wake kwenye timu hiyo.
Madktari wamesema kama hatajitonesha atarejea uwanjani katikati ya Februari 2019, hivyo ataikosa michezo dhidi ya Liverpool wa Desemba 29 na ule wa Manchester City Februari 3 mwakani.
Wakati kiungo huyo akikutwa na majanga hayo, Arsenal imetangaza kuwa beki wake wa kulia Nacho Monreal na Shkodran Mustafi wamepata ahueni na wanatarajiwa kuwepo uwanjani katika mchezo wa kesho dhidi ya Brighton & Hove Albion.
Ingawa itaendelea kumkosa Hector Bellerin, kwa wiki mbili zaidi kwani bado hajaruhusiwa kuanza mazoezi na madaktari.