Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Alisher Usmanov ametoa ofa ya Paund Bilioni 1.3 kununua hisa kubwa katika klabu ya Arsenal , kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.

Imearifiwa kwamba anayemiliki hisa nyingi katika klabu ya Arsenal kwa sasa ni Stan Kroenke bado hajajibu chochote kuhusu ofa hiyo , lakini inatarajiwa kutupiwa kapuni.

Usmanov kwa sasa anamiliki asilimia 30 tu ya hisa katika klabu hiyo ya London na ana utajiri wa thamani ya Pauni Bilioni 11.2
 
Up his ass!
 
Bora hta tusiende champions league maana ni vipigo tu kila mwaka so haina maana hta kushiriki!!
Kabisa, kama tumecheza kwa muda wa miaka ishirini na kufika mbali mara mbili tu, hatustahili kwa kweli. Ngoja tujaribu futuhi huku wenger akiendelea kuburuzwa, arsenal tutabadilika na kuwa tena timu ya kugombea vikombe wenger alitoka.
 
Dah natamani arsenal tupate kocha kma simeone ili tusajili wachezaji wa ''kazi kazi'' ili timu ipate muamko mpya kma enzi za mijitu kma lauren,cygan,vieira,campbell,keown n.k dah ila kwa kikosi hiki cha wauza sura kma bellerin,gibbs na Oxlade sioni wapi tunachukua ligi ndani ya karne hii
 
Ni wenger aondoke tu, aje mtu wa kazi kazi, Simeone akipewa na pesa ya kupata wachezaji anaowataka, timu itarudi kwenye heshima yake! Hii timu ya sasa wa kubaki ni Cech, Sanchez na Kolsielny!
 
Una maana goli 10 zinajirudia tena mwakani πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€...... huu ni uchochezi mkuu
Hawa jamaa tukiwa na wenger tumewashindwa, tulikuwaga tunadai sababu tunamaliza wa pili, tukimaliza wa kwanza ktk kundi wao wanakuwa wa pili, tunakutana nao na safari yetu inaishiaga hapo.
 
Ni wenger aondoke tu, aje mtu wa kazi kazi, Simeone akipewa na pesa ya kupata wachezaji anaowataka, timu itarudi kwenye heshima yake! Hii timu ya sasa wa kubaki ni Cech, Sanchez na Kolsielny!
Bellerin ni mzuri sana, Cech kachoka mno, bado tunamuhitaji Mtakatifu Carzola japo injury hua hazimwishi. Pia naamini kua Chamberlain ni aina ya mchezaji ambae akipata cocha kwenye hamasa anaweza kuleta matokeo. Wengine wote wasepe, hawana quality ya kuwepo Arsenal.
 
Lee Dixon, winterburn,Tony Adams, keown, hii ndio beki bora ya arsenal
 
Lee Dixon, winterburn,Tony Adams, keown, hii ndio beki bora ya arsenal
Dah walikuwa hatari sana hao..... afu mbele tukapata mtu kma ian wright, alan smith au thierry henry!!!! Mbona the invicibles class of 2004 itajirudia
 
Hawa jamaa tukiwa na wenger tumewashindwa, tulikuwaga tunadai sababu tunamaliza wa pili, tukimaliza wa kwanza ktk kundi wao wanakuwa wa pili, tunakutana nao na safari yetu inaishiaga hapo.
Kumbe nyie ni Arsenal wenzangu?
Ila mkuu barafuyamoto umepata maumivu mara dufu!
Huku Simba kule Arsenal,dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…