Usajili Updates: Wenger asema suala la usajili ni siri.
Msalheer wakuu,
Leo meneja amesema suala la usajili ni siri na Arsenal watakaposajili mchezaji watatangaza.
Ifuatayo ni taarifa yake kwa vyombo vya habari:
WENGER KEEPING PLANS SECRET
Arsene Wenger does not plan to reveal
Arsenal's transfer plans after Lyon claimed yesterday that they rejected an offer from the Gunners for Alexandre Lacazette.
"Lyon are responsible for their own statements," said Wenger. "On the transfer front, I think the best [option] is always to keep it as secret as possible. If we sign somebody, we will announce it. But I cannot tell you much more on that."
Wakati huohuo, akiongea na gazeti la New York Times la Marekani, Afisa mtendaj mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amedai kwamba Arsenal hawawezi kushindana na timu zingine katika kufanya usajili wenye fedha nyingi.
Ivan Gazidis afisa mtendaji mkuu wa Arsenal tangu 2009
Aliendelea kwa kusema:
"We can't afford to outgun competitors that have far more money. We have to be very careful, very selective,"
Arsenal inaaminiwa kuwa na kiasi cha pauni milioni 200 zikiwa ni akiba yake ya fedha ambazo haziguswi.
Hata hivyo Arsenal tayari mapema kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa walimsajili Granit Xhaka kutoka timu ya Borussia Monchengladbach kwa gharama ya pauni milioni 35.
Mpaka sasa nyuma ya pazia Arsenal wanahangaika kumsajili Alexandra Lacazette na inasemwa wameongeza offer ya pauni milioni 40.
Pia Arsenal imebidi waingie tena dirishani kutafuta beki wa kuziba nafasi ya Per Mertesacker ambae ameumia goti na atakaa nje kwa miezi Zaidi ya mitano.
Tusubiri kuona Arsenal mwaka huu wakipigwa vikumbo na timu zingine kama Man City ambao mpaka hivi sasa wanafnya mazungumzo na wachezaji watatu kuwasajili.
Wachezaji hao ni Leroy Sane, Gabriel Jesus na Marlos Moreno.
Wenger vunja benki wewe mzee!
COYGs!
Chanzo cha habari: New York Times