Usajili Updates- Arsenal wapo Italy.
Kalidou Koulibaly na Alvaro Morata
Baada ya kufanya usajili wa Granit Xhaka mapema na kuzuia timu zingine zisimsajili mchezaji huyo, Arsenal sasa wameelekeza macho nchini Italy.
Nafasi ya ulinzi.
Arsenal wamemgundua mchezaji mkoba wa Napoli aitwae Kalidou Koulibaly kama mtu anaeweza kushirikiana vema na Boss (Laurent Koscielny)
Kaoulibaly ana umri wa miaka 24 na ni mzaliwa wa France anaweza kugharimu kama Euro milioni 26 hivi.
Pia katika eneo hili la sehemu ya ulinzi kuna wachezaji wengine kadhaa ambao wameangaliwa na maskauti akiwemo Lucas Hernandez wa Athletico Madrid, mkoba wa Celtic ya Scotland Kieran Tierney, mkoba wa Bolton Wanderes Robert Holding na Ryan Sessegnon wa Fulham.
Hali kadhalika yumo beki mwingine wa kati wa timu ya Velez Sarsfield aitwae Maxi Romelo.
Nafasi ya ushambuliaji.
Olivier Giroud na Theo Walcott wameipotezea Arsenal nafasi nyingi za kushinda mechi kadhaa muhimu katika msimu uliopita.
Na hata Danny Welbeck aliporudi kutoka kwenye majeraha ya gotihakuweza kucheza mechi nyingi kabla ya kuumia tena na sasa atakosa kucheza kwa zaidi ya miezi sita.
Hivyo bila shaka yoyote Arsenal hasa baada ya kumsajili Granit Xhaka bado wapo kwenye dirisha la usajili wakiangalia uwezekano wa kusajili mshambuliaji ambae yupo tayari kuleta tofauti.
Alvaro Morata ndie anaeongoza kwenye orodha akifuatiwa na mshambuliaji mwenzie wa Juventus Paulo Dybala.
Tofauti ya Alvaro Morata na Paulo Dybala ni kwenye kasi ya kushambulia ambapo Morata ni wa mtindo Olivier Giroud ambae anapoteza mipira na anapopoteza mpira huacha kuufuata lakini Morata huwa hapotezi mipira (ball control) na huweza kufunga kwa kila situation.
Alvaro Morata
Lakini wote hawa wawili wana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti na kufunga na kwa sasa wao wanashindana katika first 11 ya Juventus huku Mario Mandzukic na Andrea Favilli wakiwa wanaanza kama wachezaji wa akiba.
Lakini meneja wa Juventus Massimilliano Allegri alianzisha mtindo wa kuzungusha muda wa uchezaji kati ya washambuliaji hawa wanne na kutokana na kila mmoja kutaka kucheza kwa muda anaopenda hii inaweza kuwa sababu ya Morata au Dybala kuamua kutafuta kuchezea timu ingine.
Paulo Dybala akijaribu kukabiliana na beki wa AC Millan ambae anatoka Colombia Cristian Zapata.
Uchezaji wa Dybala ambae ana miaka 22 ni mithili ya uchezaji wa Alexis Sanchez ambapo hupenda kusukuma nyuma mabeki na wakati huohuo kutafuta nafasi ama kwa wachezaji wenzake au yeye mwenyewe kufunga.
Vincent Janssen wa AZ Alkmaar ya Holland akifuatiwa na Sadio Mane wa Southampton na hawa ndio washambuliaji ambao hawaonei haya nyavu za timu pinzani.
Vincent Janssen
Vincent Janssen amefunga magoli 27 katika mechi alizochezea kwenye timu yake hiyo ya AZ Alkmaar yeye ana nguvu, uwezo wa kumiliki mpira na hukimbia kwa kujiamini awapo na mpira.
Lakini hawa wachezaji wote bado wapo kwenye utafiti wa kina ingawa Alvaro Morata anaongoza kwa kuwa mchezaji wa pili kuweza kusajiliwa na Arsenal.