Champions League Draw:
Inafanyika saaza Ulaya 11.45 jioni.
Kuna timu 32 katika makundi manne na kila timu itachaguliwa na timu zingine tatu kufanya kundi lenye timu nne.
Pot 1: Barcelona, Chelsea, Bayern München, Juventus, Benfica, Paris, Zenit, PSV Eindhoven
Pot 2: Real Madrid, Atlético, Porto, Arsenal, Manchester United, Valencia, Bayer Leverkusen, Manchester City
Pot 3: Shakhtar Donetsk, Sevilla, Lyon, Dynamo Kiev, Olympiacos, CSKA Moscow, Galatasaray, Roma
Pot 4: BATE Borisov, Borussia Mönchengladbach, Wolfsburg, Dynamo Zagreb, Maccabi Tel-Aviv, Gent, Malmö, Astana
Je ni timu zipi zinaweza kupangwa na Arsenal?
Arsenal wanaweza kupangwa kundi moja na timu za Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Paris-Saint Germain, Zenit St Petersburg au PSV.
Na kwa kuwa Arsenal wapo kwenye kundi la pili basi hawawezi kupangwa kundi moja na timu za Real Madrid, Atletico Madrid au FC Porto.
Timu yoyote mpya?
Ndio, kuna timu iitwayo Gent ambao ni mabingwa wa Belgium amba ni mabingwa kwa mara ya kwanza nchini humo na pia wanashiriki cl kwa mara ya kwanza.
Pia kuna timu ya Astana kutoka nchini Kazakhstan ambayo nayo ni mara ya kwanza kucheza CL. Timu yoyote itakayokwenda kucheza nchni Kazakhstan itasafiri kwa ndege Zaidi ya masaa tisa kutokea barani Ulaya.
Lini mechi zitachezwa?
Mechi za kwanza: 15/16 September
Mechi za pili: 29/30 September
Mechi za tatu: 20/21 October
Mechi za nne: 3/4 November
Mechi za tano: 24/25 November
Mechi za sita: 8/9 December
Haya basi tujiandae na hio draw baada ya masaa mawili hivi.