Arsenal (The Gunners) | Special Thread



Og mazoezini kabla ya mtanange wa kesho




Ramsey and Carzola















Prof kama kawa .. .... #COYG


 
Naomba kesho lisitutokee lililowatokea Manchester city,Chelsea, Spurs, Southampton leo. Mungu ibariki Arsenal
 
Acha kumbwera kaka...hao albino ni timu ndogo sana..

Ebana timu ndogo zimetowa watu kamasi na machozi jana na leo respectively. Lolote linaweza kutokea mkuu. FA CUP ni mashindano ya maajabu.
 
Ni fursa nyingine ya kunyanyua kombe la FA natumain kesho Prof atapanga kikosi cha maana na sio makinda
 
Haya Bolton Wanderers nao wamewakalia kooni Liverpool Anfield. Tusijeshangaa big teams zote zikiondolewa katika raundi hii. Tunatakiwa kuweka kikosi kikali kesho Kos, Cazorla, Alexis lazima waanze kama kupumzishwa iwe dakika za mwishoni tukiwa tunaongoza kwa big margin
 

Hii ndoo naona tukibaki nayo tena kwa mara nyingine, ingawa kuna surprises nyingi FA, nina matumaini tutatoboa!
 
.....Work Permit ya UK ndio shida,
yale yale ya Joel Campbell akaishia Ugiriki.
:ranger:

Mkuu heshima mbele.

"Work Permit" sio tatizo sana kwasababu Arsenal wamelipa kiasi cha kama paundi 14.5 milioni na Gabriel ni "special talent" hivyo anaingia moja kwa moja kwenye category ya msamaha kwenye kanuni za usajili za FA ya Uingereza.

Mchezaji kama ni "special talent" na gharama za usajili wake zinazidi kiasi cha paundi milioni 10, basi hawezi kukosa hio "work permit" pamoja na kwamba hajawahi kuchezea Brazili nchi alikozaliwa.

Arsenal wana wanasheria wao na wanawalipa kwa ajili ya kuingia "front" kutetea hoja kama hii ya sasa kuhusu Gabriel Paulista.

Sasa kwa kuwa kanuni za FA ya Uingereza pia zinazuia mchezaji wa nje ya bara la Ulaya kucheza ligi nchini humo kama hajachezea nchi yake zaidi ya asilimia 75 ya mechi za kimataifa huwa kuna njia ya kukata rufaa au appeal ambayo ndio Arsenal watatumia ili Gabriel aweze kucheza.

Wenger huwa hafungui tu kitabu cha hundi kama hana uhakika wa kumpata mchezaji amtakae.
 
Reactions: BAK


Paulista says his final goodbyes to the Villarreal fans
as he is given a yellow submarine as a farewell present





Villarreal players line up for a squad photo with Paulista
at the front with his submarine






Paulista embraces Villarreal captain Bruno Soriano
- with the latter presenting him with his farewell gift


Prof anajidhatiti kufunga biashara kule nyuma #COYG
 
Wakuu tupo away kutetea FA Cup kama kawa, mtanange utakuwa wa kukata na shoka nasikia team #Team Mburukenge wapo gado ati wanachubiri matokeo, wajitokeza tu chichi huwa hatutegemei bungs kama Manure, Chelsick ala Mancs tunapiga kitale kitakatifu Bring them on ... ... ... kick off 16:00 hrs GMT


 
Mkuu Wacha1

Nami nipo hapa leo.

Santiago Cazorla leo yupo bench wakati Mesut Ozil anaanza.

Timu:

Arsenal:

Szczesny, Chambers, Koscielny, Monreal, Gibbs, Flamini, Walcott, Ramsey, Ozil, Rosicky, na Giroud.

Nje kuna Mertesacker, Sanchez, Cazorla, Martinez, Coquelin, Akpom, na dogo Hector Bellerin.

Brighton:

Stockdale, Bruno, Greer, Dunk, Bennett, Holla, Ince, Calderon, Forster-Caskey, Baldock, na O'Grady.

Uwanja ni wa AMEX.

Mwamuzi ni kijana Michael Oliver ambae anatoka mji wa Northumberland.
 

Leo naona flamini anaanza
 

Hahaahhaha
 
Leo naona flamini anaanza

Good observation.

Hapa ndio mara nyingi mzee Wenger huwa anakosea anapofanya approach yake kwa hizi timu ndogondogo.

Afadhali Jose jana kakiri kwamba kufungwa na Bradford City ilikuwa ni "aibu" lakini Man City walishuka kucheza na Middlesborough wakitokea Qatar halafu baada ya kutundikwa 2-0 wakasingizia uchovu - hi si dharau hio?

Wenger angepanga timu yake ileile ya kawaida, Flamini leo atakuwa na kazi ya kudhibiti hawa vijana pale katikati.

Lakini nafikiri watatumia mtindo wa 4-4-1-1 Ramsey akiwa nyuma ya Giroud ambae ataachwa mbele peke yake na baadae watabadilisha kuwa 4-1-4-1 watakapofanya mabadiliko kutegemea na matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…