............hivi Top Four yetu tutaikamata kweli msimu huu?
Chelsea, Man City, Man United hawawezi drop points nyingi compared to us,
wakati huo huo
"chasing pack" iliyokuwa na Everton na Spurs pekee msimu ule,
safari hii kuna West Ham na Southampton pia.
:coffee:
Cc;
BAK,
Richard,
Balantanda,
Sizinga,
Wandugu Masanja,
Wacha1,
piere.fm,
rubaman....et al
Mkuu, kwanza kheri ya Xmas.
Uwezekano wa Arsenal kuwemo kwenye "top four" upo na unaweza kuwepo kwa matokeo ya ya ushindi kwenye mechi za Arsenal dhidi ya QPR,West Ham na Southampton.
Baada ya hapo Arsenal itakuwa na points 39 na kama inavyozungumzwa tutafanya usajili wa beki, mshambuliaji na mchezaji wa kiungo.
Katika wachezaji hawa nafasi mbili za beki wa kati na kiungo mkabaji ndizo nafasi zenye kupewa kipaumbele maana ALex Song atatuonesha ujasiri wake tutapocheza na West Ham Jumapili ijayo.
Zaidi ya hapo kuna habari za ndani kabisa kwamba Arsenal watasajili mshambuliaji kwa sababu Lucas Podolski anatakiwa na Inter Milan ya Italy na kwa vile nafasi yake imekuwa adimu kwenye first 11 basi anataka kuondoka.
Pia Yaya Sanogo atapelekwa kucheza kwa mkopo kwenye moja ya timu za kwenye PL na hivo kupata uzoefu wa mikikimikiki ya PL.
Hivyo basi ifikapo mwezi ujao tarehe 1 dirisha la usajili litakapofunguliwa kuna wachezaji kadhaa ambao huenda wakasajiliwa na Arsenal - Moussa Sissoko kutoka Newcastle, ambae atasaidia sehemu ya kiungo ambayo ina Mikael Arteta na Mathieu Flamini ambao siku zao za uchezaji zinakaribia mwisho.
Katika mechi na Liverpool Flamini aligundulika kuwa the "weakest link" na kugeuzwa kuwa "windsreen wiper" kuwalinda Philipe Coutinho na Adam Lallana na mpaka mwisho Liverpool wakapata goli la kusawazisha.
Hali hio ni lazima mzee Wenger atakuwa aliiona na ataifanyia kazi kumsajili Sissoko ambae ana miaka 25 na atakuwa ndio Patrick Vieira.
Mwingine ni Paulo Dybala kutoka Palermo ambae atasaidiana na Giroud na Danny Welbeck ambao ndio watakuwa washambuliaji rasmi wa Arsenal baada ya Podolski na Yaya Sanogo kupisha. Dybala anagharimu kama paundi milioni 20 hivi na hizo si nyingi kwa Arsenal kama wanataka kuepuka Europa League.
Mchezaji mwingine ni Sergio Ramos wa Real Madrid ambae amekataa kuongezewa mkataba muda si zaidi ya miaka miwili na inasemwa kwamba wakala wake amewasiliana na Arsenal. Ramos atasaidia sana sehemu ya ulinzi ambayo imepwaya sana.
Morgan Schneiderlin ni mchezai mwingine ambae Arsenal wanaweza kufanya usajili wa kueleweka kwani walikishazungumza na mchezaji huyo mwezi julai mwaka huu lakini timu yake ya Southampton ikamkatalia kuondoka.
Schneiderlin ni mrefu mwepesi na ana nguvu za kukabiliana na wachezaji wengine wa kiungo wa ligi ya Uingereza.
Hivo basi ushindi pekee katika mechi zijazo ndio njia pekee ya kuepuka muanguko mkuu ifikapo tarehe 1 Januari mwaka 2015.