AROBAINI ya CHADEMA:Charles Charles

AROBAINI ya CHADEMA:Charles Charles

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Posts
629
Reaction score
72
Na Charles Charles

“KUZUNGUKA huku na huko kwa CCM ni kutuiga sisi. Tumeanza muda mrefu baada tu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010”, ndivyo anavyosema Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.

Anaongeza kwamba “Chadema ni mwalimu” huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa mwanafunzi anayefuata nyayo kwa mambo yanayofanywa na chama chake hicho. Alikuwa akizungumza na gazeti moja la kila siku nchini kufuatia ziara iliyofanywa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana katika mikoa minne ya Arusha, Geita, Mtwara na Rukwa.

Siku chache baadaye, yeye mwenyewe alifanya ziara katika majimbo matatu ya Temeke, Kigamboni na Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukumbana na hali ngumu kuliko wakati wote uliopita.

Tatizo hilo liliambatana na ‘kudoda’ kwa harambee ya kuchangia kile kinachoitwa kuwa ni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) iliyofanyika jijini Mwanza, na kukitia chama hicho hasara ya shilingi milioni tisa.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliibua tuhuma kwa Dk. Slaa kuwa pamoja na kuwashambulia sana viongozi wenzake wilayani Temeke akisema ni mamluki wa CCM, yeye mwenyewe ana kadi ya chama hicho kinachotawala, jambo alilokiri ni kweli na ataendelea kuitunza katika maisha yake yote.

Tayari hali hiyo imeibua mtafaruku katika chama chake ambapo kuna wanachama, viongozi na wafuasi wake hivi sasa hawana tena imani naye na kuanza kumtilia wasiwasi kwa kusema inawezekana pia ndiye anavujisha siri nyingi za Chadema kwa watu wasiohusika.

Wanadai hata siasa zake za vurugu, uchochezi na uvunjaji wa sheria kwa makusudi unalenga kuifanya Chadema ichukiwe na wananchi. Anataka ionekane kuwa inahamasisha umwagaji wa damu, mkakati ambao unafanyika chini kwa chini kwa kisingizio cha M4C ili wananchi *wasigundue.

Nashukuru kwamba hatimaye wengi wameanza kukielewa chama hicho na siasa zake za kitapeli. Wameanza kukitenga wakiwemo viongozi wake waandamizi kama wenyeviti na makatibu wa wilaya, mikoa, madiwani na kadhalika.

Wamo kwa mfano aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda; aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Morogoro, Rajabu Ali; aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Iramba, Mkumbo; waliokuwa madiwani wa Arusha Mjini ambao ni Rehema Mohammed (Viti Maalum), Frank Takachi (Kata ya Olasiti), Simba Salum (Kata ya Kati) na viongozi wengine lukuki.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Rehema alisema wazi kwamba Chadema ni kama kampuni binafsi ya Dk. Slaa na hivyo anaweza kufanya lolote, wakati wowote na mahali popote ili kukidhi matakwa yake mwenyewe kwa kutumia kisingizio chochote.

Alisema amekuwa akitimua viongozi na kuweka wengine jinsi anavyotaka kwa kuwatuhumu kuwa ni mamluki wa CCM, vinginevyo huwatwisha lawama kwamba wanavunja Katiba ya Chadema ambayo hata hivyo haipo matawini, majimboni, wilayani na mikoani isipokuwa kwake mwenyewe.

Ndiyo maana alikwenda akavuruga uteuzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza kwa kuwapelekea mgombea ambaye alimteua yeye jijini Dar es Salaam. Aligoma kumtambua diwani aliyegombea kwa njia zote halali, akashinda kura za maoni za ndani ya chama akidai kuwa alishavuliwa uanachama.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ndago wilayani Iramba wiki tatu zilizopita, Mkumbo alisema ameamua kuacha uenyekiti wa wilaya wa Chadema na kuingia CCM ili apone moyo wake kuliko kuendelea kunyanyaswa kisiasa na viongozi wake wakuu.

Alisema hawezi kuendelea kuwa mwanachama na hata kiongozi wa Chadema katika ngazi yoyote “kwa vile ni chama kilichojaa majungu, fitina na chuki nyingi”.

Madai hayo yanafanana pia na yale yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda alipohutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini humo.

“Ndani ya Chadema tuliingia kwa bahati mbaya. Ilikuwa kama uko barabarani unasubiri gari na linalotokea unapanda, lakini ukishakuwa ndani unagundua kuwa ni mkweche na kushuka ili usubiri jingine. Tumeshuka na tumepanda gari la kweli linaloitwa CCM”, alisema wakati alipokaribishwa kuzungumza ili kuwawakilisha wenzake wote na kuendelea:

“Nilishikilia chama kizima mkoani, nawahakikishia kuwa hakuna cha maana kinachoendelea kule. Ndani ya Chadema hakuna sera za kumkomboa mlalahoi, badala yake kuna udikteta tu unaofanywa na viongozi wa ngazi za juu”.

Hatua ya kuanza kusambaratika kwa Chadema ilithibitika pia katika ziara ya siku tatu ya Dk. Slaa wilayani Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa* akiwashutumu viongozi wenzake kuwa ni mamluki wa CCM kwa sababu tu mahudhurio aliyoyakuta huko ni hafifu.

Mathalani, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wa Jimbo la Kinondoni walimsotesha ukumbini akiwasubiri kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.47 mchana alipochoka, akafungua kikao hicho na kuzungumza na hao wachache waliofika baada ya wao pia kubembelezwa sana kwa kupigiwa simu zao za mikononi.

Badala ya wajumbe 130 waliotakiwa kuhudhuria ili kujua ni kitu gani wanaambiwa na bosi wao, wale waliofika mkutanoni hadi wakati huo walikuwa chini ya 50 tu huku wakionekana kutokuwa tayari kumsikiliza kwa muda mrefu isipokuwa vinginevyo.

“Chadema ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii ya wajumbe kutafutana kwa simu itaendelea ni hatari wakati wa kuunda Baraza la Mawaziri”, alisema na kukiri: “Bila kujipanga wakati huu hakika hali ni ngumu huko tunakokwenda”.

Kama viongozi waliowekwa madarakani ili kukiongoza chama hicho na kuwa kiungo kati ya wanachama, wapiga kura na uongozi wa juu nao tayari wamekichoka; nani atakiunga mkono na ili iweje?

Nimekuwa nawaambia rafiki zangu kuwa tokea mfumo huu wa vyama vingi vya siasa nchini ulipoanza tena mwaka 1992 ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mpinzani aliyewahi kuwa ‘lulu’ kwa wafuasi wake kama aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR – Mageuzi, Augustine Mrema.

Aliaminiwa na kuungwa mkono kila mahali mijini na vijijini. Aliteka hisia za wengi kuanzia wazee, kina mama na vijana, matajiri na masikini, wasomi pamoja na makundi mengine.

Ndiyo maana gari lake anapomaliza kuhutubia mikutano ya hadhara hasa mijini kama Dar es Salaam lilikuwa likisukumwa na mamia ya vijana, tena kwa hiari na matakwa yao wenyewe hata kwa zaidi ya saa nzima mpaka wanapokuja kusambaratishwa na polisi waliofanya hivyo ili kumlinda dhidi ya vibaka, wezi na waporaji wengine linapoanza giza.

Lakini alipotamba kwa miaka minne akiwa katika hali hiyo kuanzia mwaka 1995 – 1999, Mrema aligundulika kuwa ni ‘msanii’, muongo, mzushi, mchochezi na mtu anayependa zaidi kusifiwa binafsi akitumia kila aina ya ujanja wa kisiasa kwa kuwadanganya wafuasi wake.

Hapo ndipo umaarufu wake wote uliposambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo na kubaki na kikundi kidogo cha watu wenye malengo yao binafsi. Hao bado wanaendelea kumuunga mkono hadi leo na baadhi yao wapo radhi na tayari hata kumfia utadhani kupe linavyong’ang’ania ngozi ya mnyama hususan ng’ombe, mbuzi ama kondoo bila kuiachia hata kama haina damu tena au tayari ameshakufa!

Hivyo ndivyo wanavyofanya wafuasi wa Chadema wakiwemo hadi wasomi, ngumbaru na kadhalika. Wapo ambao pia wamejitokeza kuthibitisha umahiri wao wa kuitetea kwa uongo, uzushi na majungu ya aina zote.

Wanafanya hivyo kwa kupewa matumaini ‘hewa’ na viongozi waandamizi wa chama hicho wakiongozwa na Dk. Slaa mwenye uwezo mkubwa wa ghiliba, uzushi na kufanya kila aina ya siasa za ‘kisanii’.

Wafanya hivyo kwa kusingizia jambo lolote, wakati wowote na mahali popote ili mradi tu wanakidhi matakwa yao wenyewe, watu ambao siku zote wanaishi kwa kutegemea majungu, umbeya na uzandiki wa namna yoyote ile dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali na viongozi wake.

Wamekuwa mahiri wa kuhubiri siasa za kikabila, kikanda na kadhalika kwa kutaka Tanzania itenganishwe kwa utawala wa kimajimbo, ule ambao Mchagga au Mpare kutoka Kilimanjaro hataweza tena kupata uongozi wowote katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Mara au Ruvuma.

Itakuwa marufuku kwa Msukuma kutoka Mwanza, Simiyu, Shinyanga au Tabora kushika uongozi wa ngazi yoyote katika mikoa kama ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Dodoma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na kadhalika.

Hata hivyo hali hiyo imekuwa kinyume baada ya miaka miwili tu ya wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema kudanganywa na kuamini uongo, lakini hivi sasa wameanza kujua ukweli.

Mbali na viongozi waliohama katika mikoa ya Arusha, Singida na Morogoro, watu kama Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Zitto Kabwe naye haelewani kabisa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kutokana na kila mmoja kutaka ateuliwe yeye kuwa mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015.

Mbali na hao, Afisa Mwandamizi wa Kurugenzi ya Sera na Utafiti, Mwita Waitara na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Juliana Sonza nao hawaelewani na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza hilo, John Heche.

Tayari mgogoro huo pia umeanza kuenea nchini ambapo kwa mfano, Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala amesimamishwa uongozi kwa sababu anapinga udikteta, lakini viongozi wa Bavicha wa Mkoa wa Mwanza na sehemu nyingine wanamtaka Dk. Slaa ajiuzulu kwa madai kuwa anakivuruga chama hicho.

Ndiyo maana sasa amechanganyikiwa kiasi cha kupayuka bila mpangilio wowote mdomoni ikiwemo kudai eti CCM inapofanya ziara zake inakuwa inaiiga Chadema, jambo ambalo hata mwendawazimu hawezi kuliamini.

Haiwezekani kwa namna yoyote kuwa viongozi wa CCM ambayo ilianzishwa mwaka 1977 wawe hawajafanya kabisa ziara mpaka walipoiga Chadema wiki tatu zilizopita!

Ndiyo maana Dk. Slaa sasa na ‘vigogo’ wenzake wa kitaifa wamechanganyikiwa baada ya kuanza kususiwa mikutanoni huku viongozi wengine wakisema wamechoshwa na udikteta, kuburuzwa kusikoisha na siasa za kitapeli. *

Ndiyo maana sasa wamechanganyikiwa kuona chama hicho kinakosa mpaka wachangiaji katika harambee zake kama ilivyotokea majuzi jijini Mwanza, kikatumia shilingi milioni 15 kugharamia maandalizi, lakini kikachangiwa shilingi milioni sita tu.

Tayari wimbi kubwa la wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema linazidi kukimbilia CCM baada ya kuchoshwa na siasa za fitina, uzushi, uongo na kila aina ya ghiliba tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2010.

Wanasema waziwazi kuwa “imetosha”, na sasa ‘arobaini’ ya Chadema hatimaye imewadia!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244
 
Honey K mwanangu kwanini hukuweka source kuwa ni kijigazeti uchwara kiitwacho Tazama? Umeogopa watu wasiidharau thread yako nini? Je wajua kuwa katika waandishi wa hovyo nchini hakuna kama huyu changu wa maadili au kanjanja kama Charles Charles? Je wajua kuwa huyu jamaa hana hata cheti cha uandishi zaidi ya kughushi? Je wajua kuwa Charles Charles ni mgonjwa wa njaa anayeweza kumtumikia yoyote mradi mkono uende kinywani? Je wajua kuwa mwandishi wa makala hii ni mtu asiyejua hata hizo siasa ukiachia mbali kuwa na elimu angalau ya kidato cha nne? Kwa wanaosoma makala za huyu mchumia tumbo na kumfahamu, nadhani haandikii imani wala kujua anachoandika zaidi ya kujikomba kwa wanaomlipa. Je wajua kuwa baada ya waandishi kama Muhingo na Salva Rweyemamu kujivua nguo kwa kuendekeza njaa, wapo waandishi wengi na makini wanaolilia mabaki ya mafisadi? Eti Charles Charles ni katibu msaidizi idara ya uhusiano wa kimataifa wa CCM. Kweli CCM imeishiwa na ni bingwa wa kubeba vihiyo walioghushi.
Na Charles Charles

"KUZUNGUKA huku na huko kwa CCM ni kutuiga sisi. Tumeanza muda mrefu baada tu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010", ndivyo anavyosema Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa.

Anaongeza kwamba "Chadema ni mwalimu" huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa mwanafunzi anayefuata nyayo kwa mambo yanayofanywa na chama chake hicho. Alikuwa akizungumza na gazeti moja la kila siku nchini kufuatia ziara iliyofanywa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana katika mikoa minne ya Arusha, Geita, Mtwara na Rukwa.

Siku chache baadaye, yeye mwenyewe alifanya ziara katika majimbo matatu ya Temeke, Kigamboni na Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukumbana na hali ngumu kuliko wakati wote uliopita.

Tatizo hilo liliambatana na ‘kudoda' kwa harambee ya kuchangia kile kinachoitwa kuwa ni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) iliyofanyika jijini Mwanza, na kukitia chama hicho hasara ya shilingi milioni tisa.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliibua tuhuma kwa Dk. Slaa kuwa pamoja na kuwashambulia sana viongozi wenzake wilayani Temeke akisema ni mamluki wa CCM, yeye mwenyewe ana kadi ya chama hicho kinachotawala, jambo alilokiri ni kweli na ataendelea kuitunza katika maisha yake yote.

Tayari hali hiyo imeibua mtafaruku katika chama chake ambapo kuna wanachama, viongozi na wafuasi wake hivi sasa hawana tena imani naye na kuanza kumtilia wasiwasi kwa kusema inawezekana pia ndiye anavujisha siri nyingi za Chadema kwa watu wasiohusika.

Wanadai hata siasa zake za vurugu, uchochezi na uvunjaji wa sheria kwa makusudi unalenga kuifanya Chadema ichukiwe na wananchi. Anataka ionekane kuwa inahamasisha umwagaji wa damu, mkakati ambao unafanyika chini kwa chini kwa kisingizio cha M4C ili wananchi *wasigundue.

Nashukuru kwamba hatimaye wengi wameanza kukielewa chama hicho na siasa zake za kitapeli. Wameanza kukitenga wakiwemo viongozi wake waandamizi kama wenyeviti na makatibu wa wilaya, mikoa, madiwani na kadhalika.

Wamo kwa mfano aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda; aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Morogoro, Rajabu Ali; aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Iramba, Mkumbo; waliokuwa madiwani wa Arusha Mjini ambao ni Rehema Mohammed (Viti Maalum), Frank Takachi (Kata ya Olasiti), Simba Salum (Kata ya Kati) na viongozi wengine lukuki.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Rehema alisema wazi kwamba Chadema ni kama kampuni binafsi ya Dk. Slaa na hivyo anaweza kufanya lolote, wakati wowote na mahali popote ili kukidhi matakwa yake mwenyewe kwa kutumia kisingizio chochote.

Alisema amekuwa akitimua viongozi na kuweka wengine jinsi anavyotaka kwa kuwatuhumu kuwa ni mamluki wa CCM, vinginevyo huwatwisha lawama kwamba wanavunja Katiba ya Chadema ambayo hata hivyo haipo matawini, majimboni, wilayani na mikoani isipokuwa kwake mwenyewe.

Ndiyo maana alikwenda akavuruga uteuzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza kwa kuwapelekea mgombea ambaye alimteua yeye jijini Dar es Salaam. Aligoma kumtambua diwani aliyegombea kwa njia zote halali, akashinda kura za maoni za ndani ya chama akidai kuwa alishavuliwa uanachama.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ndago wilayani Iramba wiki tatu zilizopita, Mkumbo alisema ameamua kuacha uenyekiti wa wilaya wa Chadema na kuingia CCM ili apone moyo wake kuliko kuendelea kunyanyaswa kisiasa na viongozi wake wakuu.

Alisema hawezi kuendelea kuwa mwanachama na hata kiongozi wa Chadema katika ngazi yoyote "kwa vile ni chama kilichojaa majungu, fitina na chuki nyingi".

Madai hayo yanafanana pia na yale yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda alipohutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini humo.

"Ndani ya Chadema tuliingia kwa bahati mbaya. Ilikuwa kama uko barabarani unasubiri gari na linalotokea unapanda, lakini ukishakuwa ndani unagundua kuwa ni mkweche na kushuka ili usubiri jingine. Tumeshuka na tumepanda gari la kweli linaloitwa CCM", alisema wakati alipokaribishwa kuzungumza ili kuwawakilisha wenzake wote na kuendelea:

"Nilishikilia chama kizima mkoani, nawahakikishia kuwa hakuna cha maana kinachoendelea kule. Ndani ya Chadema hakuna sera za kumkomboa mlalahoi, badala yake kuna udikteta tu unaofanywa na viongozi wa ngazi za juu".

Hatua ya kuanza kusambaratika kwa Chadema ilithibitika pia katika ziara ya siku tatu ya Dk. Slaa wilayani Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa* akiwashutumu viongozi wenzake kuwa ni mamluki wa CCM kwa sababu tu mahudhurio aliyoyakuta huko ni hafifu.

Mathalani, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wa Jimbo la Kinondoni walimsotesha ukumbini akiwasubiri kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.47 mchana alipochoka, akafungua kikao hicho na kuzungumza na hao wachache waliofika baada ya wao pia kubembelezwa sana kwa kupigiwa simu zao za mikononi.

Badala ya wajumbe 130 waliotakiwa kuhudhuria ili kujua ni kitu gani wanaambiwa na bosi wao, wale waliofika mkutanoni hadi wakati huo walikuwa chini ya 50 tu huku wakionekana kutokuwa tayari kumsikiliza kwa muda mrefu isipokuwa vinginevyo.

"Chadema ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii ya wajumbe kutafutana kwa simu itaendelea ni hatari wakati wa kuunda Baraza la Mawaziri", alisema na kukiri: "Bila kujipanga wakati huu hakika hali ni ngumu huko tunakokwenda".

Kama viongozi waliowekwa madarakani ili kukiongoza chama hicho na kuwa kiungo kati ya wanachama, wapiga kura na uongozi wa juu nao tayari wamekichoka; nani atakiunga mkono na ili iweje?

Nimekuwa nawaambia rafiki zangu kuwa tokea mfumo huu wa vyama vingi vya siasa nchini ulipoanza tena mwaka 1992 ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mpinzani aliyewahi kuwa ‘lulu' kwa wafuasi wake kama aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR – Mageuzi, Augustine Mrema.

Aliaminiwa na kuungwa mkono kila mahali mijini na vijijini. Aliteka hisia za wengi kuanzia wazee, kina mama na vijana, matajiri na masikini, wasomi pamoja na makundi mengine.

Ndiyo maana gari lake anapomaliza kuhutubia mikutano ya hadhara hasa mijini kama Dar es Salaam lilikuwa likisukumwa na mamia ya vijana, tena kwa hiari na matakwa yao wenyewe hata kwa zaidi ya saa nzima mpaka wanapokuja kusambaratishwa na polisi waliofanya hivyo ili kumlinda dhidi ya vibaka, wezi na waporaji wengine linapoanza giza.

Lakini alipotamba kwa miaka minne akiwa katika hali hiyo kuanzia mwaka 1995 – 1999, Mrema aligundulika kuwa ni ‘msanii', muongo, mzushi, mchochezi na mtu anayependa zaidi kusifiwa binafsi akitumia kila aina ya ujanja wa kisiasa kwa kuwadanganya wafuasi wake.

Hapo ndipo umaarufu wake wote uliposambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo na kubaki na kikundi kidogo cha watu wenye malengo yao binafsi. Hao bado wanaendelea kumuunga mkono hadi leo na baadhi yao wapo radhi na tayari hata kumfia utadhani kupe linavyong'ang'ania ngozi ya mnyama hususan ng'ombe, mbuzi ama kondoo bila kuiachia hata kama haina damu tena au tayari ameshakufa!

Hivyo ndivyo wanavyofanya wafuasi wa Chadema wakiwemo hadi wasomi, ngumbaru na kadhalika. Wapo ambao pia wamejitokeza kuthibitisha umahiri wao wa kuitetea kwa uongo, uzushi na majungu ya aina zote.

Wanafanya hivyo kwa kupewa matumaini ‘hewa' na viongozi waandamizi wa chama hicho wakiongozwa na Dk. Slaa mwenye uwezo mkubwa wa ghiliba, uzushi na kufanya kila aina ya siasa za ‘kisanii'.

Wafanya hivyo kwa kusingizia jambo lolote, wakati wowote na mahali popote ili mradi tu wanakidhi matakwa yao wenyewe, watu ambao siku zote wanaishi kwa kutegemea majungu, umbeya na uzandiki wa namna yoyote ile dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali na viongozi wake.

Wamekuwa mahiri wa kuhubiri siasa za kikabila, kikanda na kadhalika kwa kutaka Tanzania itenganishwe kwa utawala wa kimajimbo, ule ambao Mchagga au Mpare kutoka Kilimanjaro hataweza tena kupata uongozi wowote katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Mara au Ruvuma.

Itakuwa marufuku kwa Msukuma kutoka Mwanza, Simiyu, Shinyanga au Tabora kushika uongozi wa ngazi yoyote katika mikoa kama ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Dodoma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na kadhalika.

Hata hivyo hali hiyo imekuwa kinyume baada ya miaka miwili tu ya wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema kudanganywa na kuamini uongo, lakini hivi sasa wameanza kujua ukweli.

Mbali na viongozi waliohama katika mikoa ya Arusha, Singida na Morogoro, watu kama Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Zitto Kabwe naye haelewani kabisa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kutokana na kila mmoja kutaka ateuliwe yeye kuwa mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015.

Mbali na hao, Afisa Mwandamizi wa Kurugenzi ya Sera na Utafiti, Mwita Waitara na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Juliana Sonza nao hawaelewani na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza hilo, John Heche.

Tayari mgogoro huo pia umeanza kuenea nchini ambapo kwa mfano, Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala amesimamishwa uongozi kwa sababu anapinga udikteta, lakini viongozi wa Bavicha wa Mkoa wa Mwanza na sehemu nyingine wanamtaka Dk. Slaa ajiuzulu kwa madai kuwa anakivuruga chama hicho.

Ndiyo maana sasa amechanganyikiwa kiasi cha kupayuka bila mpangilio wowote mdomoni ikiwemo kudai eti CCM inapofanya ziara zake inakuwa inaiiga Chadema, jambo ambalo hata mwendawazimu hawezi kuliamini.

Haiwezekani kwa namna yoyote kuwa viongozi wa CCM ambayo ilianzishwa mwaka 1977 wawe hawajafanya kabisa ziara mpaka walipoiga Chadema wiki tatu zilizopita!

Ndiyo maana Dk. Slaa sasa na ‘vigogo' wenzake wa kitaifa wamechanganyikiwa baada ya kuanza kususiwa mikutanoni huku viongozi wengine wakisema wamechoshwa na udikteta, kuburuzwa kusikoisha na siasa za kitapeli. *

Ndiyo maana sasa wamechanganyikiwa kuona chama hicho kinakosa mpaka wachangiaji katika harambee zake kama ilivyotokea majuzi jijini Mwanza, kikatumia shilingi milioni 15 kugharamia maandalizi, lakini kikachangiwa shilingi milioni sita tu.

Tayari wimbi kubwa la wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema linazidi kukimbilia CCM baada ya kuchoshwa na siasa za fitina, uzushi, uongo na kila aina ya ghiliba tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2010.

Wanasema waziwazi kuwa "imetosha", na sasa ‘arobaini' ya Chadema hatimaye imewadia!

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya CCM. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244
 
Huyu nae ni kamasi tu.
Ndio vitu gani umeandika hapa na kujitangaza eti umetokea ccm.
Peleka wizi wako kwa mafisadi wenzako.

Kama kuna mafisadi wa mali ya uma basi kuna mafisadi wa habari na wewe ni mmoja wao.
 
“KUZUNGUKA huku na huko kwa CCM ni kutuiga sisi. Tumeanza muda mrefu baada tu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 tumekuwa tukizunguka na kuwaleza wananchi mambo mbalimbali”, ndivyo anavyosema Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa!

Anaongeza kwa kusema kuwa “Chadema ni mwalimu” na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kama mwanafunzi na ndiyo maana siku zote inafuata nyayo kwa mambo yanayofanywa na chama chake hicho. Alikuwa akizungumza na gazeti moja la kila siku nchini kufuatia ziara iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana katika mikoa minne ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha hivi karibuni.

Siku chache baadaye, Dk. Slaa naye alifanya ziara yake katika majimbo matatu ya Temeke, Kigamboni na Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukumbana na hali ngumu kuliko wakati wote uliopita.

Tatizo hilo liliambatana na ‘kudoda’ kwa harambee ya kuchangia kile kinachoitwa kuwa ni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) iliyofanyika jijini Mwanza, na kukitia chama hicho hasara ya shilingi milioni tisa.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliibua tuhuma kwa Dk. Slaa kuwa ingawa alikuwa mstari wa mbele akiwashambulia viongozi wenzake wilayani Temeke akidai ni mamluki wa CCM, yeye mwenyewe bado anamiliki kadi ya chama hicho kinachotawala na anailipia ada, jambo alilosema ni kweli kwamba anayo na ataendelea kuitunza kwa makini yake yote, mapenzi yake yote na uaminifu wake wote!

Alisema kadi hiyo ni mali yake, hivyo ataitunza katika maisha yake yote ili wajukuu zake pia waje waione na kuwaachia usia wa kuwa CCM ni chama alichokitumikia kwa moyo wake wote, akakihama kwa shinikizo litokanalo na uchu wa madaraka, lakini akaendelea kuwa mwanachama mwaminifu kwake hata kama alifanya hivyo kwa siri mpaka majuzi alipokuja kuumbuliwa na Nape na kukiri kuwa ni kweli.

Tayari hali hiyo imeibua mtafaruku katika chama chake ambapo kuna wanachama, viongozi na wafuasi wake hivi sasa hawana tena imani naye yoyote na kuanza kumtilia wasiwasi kwa kusema kwamba inawezekana pia ndiye anavujisha siri nyingi za Chadema kwa CCM.

Wanadai kwamba hata siasa zake za vurugu, uchochezi na uvunjaji wa sheria kwa makusudi unalenga kuifanya Chadema ichukiwe na wananchi. Anataka ionekane kwamba kuendesha harakati zinazolenga kuhamasisha pamoja na kukumbatia umwagaji wa damu, mkakati wa chini kwa chini unaofanyika kwa kivuli cha M4C ili wenye akili kidogo wasijue chochote.

Nashukuru kwamba hatimaye wananchi wameanza kukiogopa chama hicho na siasa zake za kiharakati zinazofanywa zaidi na Dk. Slaa. Wameanza kukitenga wakiwemo viongozi wake muhimu kama wenyeviti na makatibu wa wilaya pamoja na mikoa, madiwani na kadhalika.

Katika hesabu kwa mfano yumo aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda; aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Morogoro, Rajabu Ali, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Iramba, Mkumbo, waliokuwa madiwani wa Arusha ambao ni Rehema Mohammed (Viti Maalum), Frank Takachi (Kata ya Olasiti), Simba Salum (kata ya Kati) na viongozi wengine wengi.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Rehema aliweka wazi kwamba Chadema imegeuzwa kuwa sawa na kampuni binafsi ya Dk. Slaa, hivyo anaweza kufanya lolote, wakati wowote na mahali popote ili mradi anakidhi matakwa yake mwenyewe kwa kutumia kisingizio chochote.

Amekuwa akitimua viongozi na kuweka wengine kadri anavyojisikia yeye kwa kuwatuhumu kuwa ni mamluki wa CCM, vinginevyo huwatwisha lawama kwamba wanakwenda kinyume cha Katiba ya Chadema ambayo hata hivyo kamwe haipo matawini, majimboni, wilayani na mikoani isipokuwa kwake mwenyewe jijini Dar es Salaam.

Ndiyo maana alikwenda akavuruga uteuzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza kwa kuwapelekea mgombea ambaye alimteua yeye jijini Dar es Salaam. Aligoma kumtambua diwani wa chama hicho chenyewe ambaye aligombea kwa njia zote halali, akashinda kura za maoni za ndani na kudai alishavuliwa uanachama na kung’ang’ania matakwa yake.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ndago wilayani Iramba hivi karibuni, Mkumbo alisema ameamua kuacha uenyekiti wa wilaya wa Chadema na kuingia CCM ili apone moyo wake kuliko kuendelea kunyanyaswa kisiasa na viongozi wake wakuu.

Alisema hawezi kamwe kuendelea kuwa mwanachama na hata kiongozi wa Chadema katika ngazi yoyote “kwa sababu ni chama kilichojaa majungu, fitina na chuki nyingi”.

Madai hayo yanafanana kwa kiwango kikubwa na yale yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda aliyezungumza katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini humo, kwa niaba ya wanachama na viongozi wenzake na kubainisha:

“Ndani ya Chadema tuliingia kwa bahati mbaya tu. Ilikuwa ni kama uko barabarani unasubiri gari na linalotokea unapanda, lakini ukishakuwa ndani unagundua kuwa ni mkweche na kushuka ili usbiri jingine. Tumeshuka na tumepanda gari la kweli linaloitwa CCM.

“Nilishikilia chama mkoani na wilayani, nawahakikishia kwamba hakuna cha maana kinachoendelea kule. Ndani ya Chadema hakuna sera za kumkomboa mlalahoi, badala yake kuna udikteta tu unaofanywa na viongozi wa ngazi za juu”.

Kuanza kusambaratika kwa kasi kiasi hicho kwa Chadema kulithibitika waziwazi wakati wa ziara ya siku tatu ya Dk. Slaa wilayani Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa akiwashutumu viongozi wenzake kuwa ni mamluki wa CCM eti kwa sababu tu mahudhurio aliyokuwa akiyakuta huko ni hafifu sana.

Mathalani, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wa Jimbo la Kinondoni walimsotesha ukumbini akiwasubiri tangu saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.47 mchana aliposhindwa kuvumilia, akaona afungue kikao chake hicho na kuongea na hao wachache waliofika baada ya wao pia kubembelezwa sana kwa kupigiwa simu zao za mikononi.

Badala ya wajumbe 130 waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho ili kujua nini wanaambiwa na bosi wao huyo, wale waliokuwa tayari wamefika hadi wakati huo walikuwa ni chini ya 50 tu huku wakionekana kutokuwa tayari kumsikiliza kwa muda mrefu isipokuwa vinginevyo.

“Chadema ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii ya wajumbe kutafutana kwa simu itaendelea ni hatari wakati wa kuunda Baraza la Mawaziri”, alisema na kuendelea: “Haiwezekani Rais aje kutafuta Baraza la Mawaziri kwa njia hiyo. Bila kujipanga wakati huu (hakika hali) itakuwa ngumu huko mbele tunakokwenda”.

Simshangai Dk. Slaa kuwa na roho ngumu kama ya paka kwa kuendelea kufikiria ndoto ya kushinda uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015 huku chama chake kikisambaratika kila mahali. Kiongozi anayefikiri kwa akili timamu kichwani mwake hakika asingeweza kabisa kuzungumzia suala hilo isipokuwa vinginevyo.

Kama viongozi waliowekwa madarakani ili kukiongoza chama hicho na kuwa kiungo kati ya wanachama, wapiga kura na uongozi wa juu nao tayari wanaonyesha kuwa mioyo yao haipo nacho tena, nani ataendelea kukiunga mkono na ili iweje?

Nimekuwa nawaambia rafiki zangu kuwa tokea mfumo huu wa vyama vingi vya siasa nchini ulipoanza tena mwaka 1992 kama inavyosema Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mpinzani hata mmoja aliyewahi kuwa ‘lulu’ kwa wafuasi wake kama aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR – Mageuzi, Augustine Mrema.

Alikuwa kimbilio la wengi na kuungwa mkono kila mahali mijini na vijijini. Aliteka hisia za kina mama na vijana, matajiri na masikini, wasomi na watu waliosoma katika viwango vya kawaida na kadhalika.

Ndiyo maana gari lake akimaliza kuhutubia mikutano ya hadhara hasa mijini kama Dar es Salaam lilikuwa likisukumwa na mamia ya vijana, tena kwa hiari na matakwa yao wenyewe hata kwa zaidi ya saa nzima mpaka wanapokuja kusambaratishwa na polisi waliofanya hivyo ili kumlinda dhidi ya vibaka, wezi na waporaji wengine linapoanza giza.

Lakini baada ya kutamba kwa miaka minne mfululizo akiwa katika hali hiyo kuanzia mwaka 1995 – 1999, Mrema aligunduliwa kuwa ni ‘msanii’, muongo, mzushi, mchochezi na mtu anayependa zaidi kusifiwa binafsi na kutumia kila aina ya ujanja wa kisiasa kuwadanganya wafuasi wake.

Hapo ndipo umaarufu wake wote uliposambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo na kubaki na kikundi kidogo cha watu waliokuwa na maslahi naye wenyewe. Hao wanaendelea kumuunga mkono hadi leo na wengine kati yao wapo radhi na tayari hata kumfia utadhani kupe linavyong’ang’ania kwenye ngozi ya mnyama hususan ng’ombe, mbuzi ama kondoo bila kuiachia hata kama tayari ameshakufa!

Hivyo ndivyo wanavyofanya wafuasi wa Chadema wakiwemo baadhi ya wasomi, ngumbaru na kadhalika. Wengine wamejitokeza mstari wa mbele kuthibitisha umahiri wao wa kuitetea kwa uongo, uzushi na majungu.

Wanafanya hivyo kwa kuelewa matumaini ‘hewa’ wanayolishwa na viongozi mbalimbali wa Chadema hususan Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa ambaye amethibitisha kuwa ana uwezo mkubwa wa ghiliba, uzushi na kufanya kila aina ya siasa za ‘kisanii’ na ‘chafu’.

Amejitokeza kuwa mstari wa mbele kusingizia chochote, wakati wowote na mahali popote ili mradi anakidhi matakwa yake ya kutafuta umaarufu kwa njia zote anazozijua mwenyewe, mtu ambaye siku zote amekuwa akiishi kwa kutegemea majungu, umbeya na uzandiki kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali na viongozi wake wakuu.

Amekuwa tanuru la kupikia uongo, uzushi, fitina na kutengenezea kila aina ya hasira na chuki kwa wananchi, lakini anafanya hivyo siyo kwa ajili ya maslahi ya nchi yake, watu wake wala chama chake ila yake mwenyewe kwa ajili ya tumbo lake na matamanio yake mengine.

Tayari hali imekuwa kinyume baada ya miaka miwili tu ya wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema kukiamini chama hicho kwa mkumbo na kudanganywa na hivyo wengi wao wameanza kukiasi.

Mbali na viongozi waandamizi waliokihama katika mikoa ya Arusha, Singida na Morogoro, mgogoro mzito unaofukuta katika Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam kati ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe dhidi ya Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Zitto Kabwe ni miongoni mwa majanga yanayofukuta chini kwa chini.

Kana kwamba haitoshi, mgogoro mwingine uliopo ni kati ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Heche dhidi ya Afisa wa Kurugenzi ya Sera na Utafiti, Mwita Waitara na Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Sonza.

Tayari pia mgogoro huo umeanza kuenea nchi nzima ambapo kwa mfano, Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala, uongozi wa Bavicha wa Mkoa wa Mwanza mbali na sehemu nyingine, wanamtaka Dk. Slaa ajiuzulu kwa madai kuwa anakivuruga chama hicho.

Ndiyo maana sasa amechanganyikiwa kiasi cha kupayuka bila mpangilio wowote mdomoni ikiwemo kudai eti CCM inapofanya ziara zake inakuwa inaiiga Chadema, jambo ambalo hata mwendawazimu wa akili hawezi kulitangaza.

Haiwezekani kwa namna zote kuwa viongozi wa CCM ambayo ilianzishwa mwaka 1977 wawe hawajafanya kabisa ziara hadi walipoiga Chadema wiki tatu zilizopita!

Ndiyo maana Dk. Slaa sasa amechanganyikiwa baada ya kuanza kususiwa mikutanoni na viongozi wake, wanachama wake na wafuasi wake huku wengine wakisema wamechoshwa na udikteta, kuburuzwa kusikoisha na siasa za kitapeli anazofanya yeye na viongozi wengine wa kitaifa.

Katika hali hiyo na hata vinginevyo ndiyo maana wameanza kukikimbia chama hicho huku wakisema waziwazi kuwa kinasambaratika, na kwamba miaka miwili iliyotumika kwa kuwajaza fitina, uzushi, uongo na kila aina ya ghiliba tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 imetosha, na sasa ‘arobaini’ ya Chadema hatimaye imewadia!
 
Hii thread si imerudiwa?!!. BANGI zikivutwa na jua kali na kuchanganywa na mnazi zinalevya saaaaana!
 
nguvu ulizopoteza hapa ni afadhali ungeenda kuzimalizia hata kwa machangu,upuuzi mtupu!!!
 
Katika hali hiyo na hata vinginevyo ndiyo maana wameanza kukikimbia chama hicho huku wakisema waziwazi kuwa kinasambaratika, na kwamba miaka miwili iliyotumika kwa kuwajaza fitina, uzushi, uongo na kila aina ya ghiliba tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 imetosha, na sasa ‘arobaini' ya Chadema hatimaye imewadia!

Kachukue Posho. Vipi klugaragazwa mahakamani kwa kesi ya kuchonga na hukumu toka Ikulu?
 
Hacha kujitia moyo wewe,dakika 90 ni mwaka 2015,uje uthibitishe uyasemayo,msipokuwa makini Dr slaa atawahisha mazishi yenu,CCM yote plus masalia kama zito mnapambana na mtu mmoja kila siku/
 
PM7 at work, mtakuja na kila aina za Ngonjera hapa, na leo kilicho tokea Makama ya Rufaa ni Msiba mkuu kwenu, na nasikia mlikuwa mmeisha andaa Sherehe ya kukata na shoka,

Hii nchi haiwezi kuendelea kama mtu kama huyu anapoteza muda mwingi kuandika ujinga badala ya kufanya production, wakati China watu wanatafuta muda wa kununua kama upo,
 
Hacha kujitia moyo wewe,dakika 90 ni mwaka 2015,uje uthibitishe uyasemayo,msipokuwa makini Dr slaa atawahisha mazishi yenu,CCM yote plus masalia kama zito mnapambana na mtu mmoja kila siku/

Hawa jamaa leo Lema angeshindwa wangekesha Humu, kwa sasa ni huzuni tupu na mwaka umeisha vibaya sana kwao, masikini

PM7 at work, mtakuja na kila aina za Ngonjera hapa, na leo kilicho tokea Makama ya Rufaa ni Msiba mkuu kwenu, na nasikia mlikuwa mmeisha andaa Sherehe ya kukata na shoka,

Ndiyo hizo ID za mtungu, sasa sijui huyu ni nani katika yale masalia.
 
Tumechoka na wimbo wa kadi kadi. Kila siku kadi kadi. Mna mimba changa nyie mashangingi wa ccm??
 
hizi sio enzi za mrema kila kitu kuhadaa umma,mambo yamebadilika na nakusikitikia kwa mwenendo wako maana utakuja kulaaniwa na wajukuu zako kwa kuendelea kuwatetea majangili wa mali za wazalendo kwa ufitini wako kwa kulipwa kiasi kidogo cha hela ambayo imetokana na ufisadi.

Jifikirie na uchukue hatua mfano hata kule misri rais na familia yake hawakujua kama yangewatokea hayo

hamna wa kuzuia mabadiliko ya TZ kwa sasa
 
GHarama za maisha: Mchele 2500/= (mwaka 2005 ilikuwa 800/=); Sukari 2500/= (mwaka 2005 ilikuwa 600/= hadi 700/=); Nyama kilo moja 6000/=(mwaka 2005 ilikuwa 1200/= hadi 1500/=); S0da 600/= ((mwaka 2005 ilikuwa 150/=); Chumvi paketi 300/=(mwaka 2005 ilikuwa 50/=); Hivi tutafika?
 
KUZUNGUKA huku na huko kwa CCM ni kutuiga sisi. Tumeanza muda mrefu baada tu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 tumekuwa tukizunguka na kuwaleza wananchi mambo mbalimbali, ndivyo anavyosema Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa!

Anaongeza kwa kusema kuwa Chadema ni mwalimu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kama mwanafunzi na ndiyo maana siku zote inafuata nyayo kwa mambo yanayofanywa na chama chake hicho. Alikuwa akizungumza na gazeti moja la kila siku nchini kufuatia ziara iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Kanali Abdulrahman Kinana katika mikoa minne ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha hivi karibuni.

Siku chache baadaye, Dk. Slaa naye alifanya ziara yake katika majimbo matatu ya Temeke, Kigamboni na Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukumbana na hali ngumu kuliko wakati wote uliopita.

Tatizo hilo liliambatana na kudoda kwa harambee ya kuchangia kile kinachoitwa kuwa ni Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) iliyofanyika jijini Mwanza, na kukitia chama hicho hasara ya shilingi milioni tisa.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliibua tuhuma kwa Dk. Slaa kuwa ingawa alikuwa mstari wa mbele akiwashambulia viongozi wenzake wilayani Temeke akidai ni mamluki wa CCM, yeye mwenyewe bado anamiliki kadi ya chama hicho kinachotawala na anailipia ada, jambo alilosema ni kweli kwamba anayo na ataendelea kuitunza kwa makini yake yote, mapenzi yake yote na uaminifu wake wote!

Alisema kadi hiyo ni mali yake, hivyo ataitunza katika maisha yake yote ili wajukuu zake pia waje waione na kuwaachia usia wa kuwa CCM ni chama alichokitumikia kwa moyo wake wote, akakihama kwa shinikizo litokanalo na uchu wa madaraka, lakini akaendelea kuwa mwanachama mwaminifu kwake hata kama alifanya hivyo kwa siri mpaka majuzi alipokuja kuumbuliwa na Nape na kukiri kuwa ni kweli.

Tayari hali hiyo imeibua mtafaruku katika chama chake ambapo kuna wanachama, viongozi na wafuasi wake hivi sasa hawana tena imani naye yoyote na kuanza kumtilia wasiwasi kwa kusema kwamba inawezekana pia ndiye anavujisha siri nyingi za Chadema kwa CCM.

Wanadai kwamba hata siasa zake za vurugu, uchochezi na uvunjaji wa sheria kwa makusudi unalenga kuifanya Chadema ichukiwe na wananchi. Anataka ionekane kwamba kuendesha harakati zinazolenga kuhamasisha pamoja na kukumbatia umwagaji wa damu, mkakati wa chini kwa chini unaofanyika kwa kivuli cha M4C ili wenye akili kidogo wasijue chochote.

Nashukuru kwamba hatimaye wananchi wameanza kukiogopa chama hicho na siasa zake za kiharakati zinazofanywa zaidi na Dk. Slaa. Wameanza kukitenga wakiwemo viongozi wake muhimu kama wenyeviti na makatibu wa wilaya pamoja na mikoa, madiwani na kadhalika.

Katika hesabu kwa mfano yumo aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda; aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Morogoro, Rajabu Ali, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Iramba, Mkumbo, waliokuwa madiwani wa Arusha ambao ni Rehema Mohammed (Viti Maalum), Frank Takachi (Kata ya Olasiti), Simba Salum (kata ya Kati) na viongozi wengine wengi.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Rehema aliweka wazi kwamba Chadema imegeuzwa kuwa sawa na kampuni binafsi ya Dk. Slaa, hivyo anaweza kufanya lolote, wakati wowote na mahali popote ili mradi anakidhi matakwa yake mwenyewe kwa kutumia kisingizio chochote.

Amekuwa akitimua viongozi na kuweka wengine kadri anavyojisikia yeye kwa kuwatuhumu kuwa ni mamluki wa CCM, vinginevyo huwatwisha lawama kwamba wanakwenda kinyume cha Katiba ya Chadema ambayo hata hivyo kamwe haipo matawini, majimboni, wilayani na mikoani isipokuwa kwake mwenyewe jijini Dar es Salaam.

Ndiyo maana alikwenda akavuruga uteuzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza kwa kuwapelekea mgombea ambaye alimteua yeye jijini Dar es Salaam. Aligoma kumtambua diwani wa chama hicho chenyewe ambaye aligombea kwa njia zote halali, akashinda kura za maoni za ndani na kudai alishavuliwa uanachama na kungangania matakwa yake.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ndago wilayani Iramba hivi karibuni, Mkumbo alisema ameamua kuacha uenyekiti wa wilaya wa Chadema na kuingia CCM ili apone moyo wake kuliko kuendelea kunyanyaswa kisiasa na viongozi wake wakuu.

Alisema hawezi kamwe kuendelea kuwa mwanachama na hata kiongozi wa Chadema katika ngazi yoyote kwa sababu ni chama kilichojaa majungu, fitina na chuki nyingi.

Madai hayo yanafanana kwa kiwango kikubwa na yale yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Abel Luanda aliyezungumza katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini humo, kwa niaba ya wanachama na viongozi wenzake na kubainisha:

Ndani ya Chadema tuliingia kwa bahati mbaya tu. Ilikuwa ni kama uko barabarani unasubiri gari na linalotokea unapanda, lakini ukishakuwa ndani unagundua kuwa ni mkweche na kushuka ili usbiri jingine. Tumeshuka na tumepanda gari la kweli linaloitwa CCM.

Nilishikilia chama mkoani na wilayani, nawahakikishia kwamba hakuna cha maana kinachoendelea kule. Ndani ya Chadema hakuna sera za kumkomboa mlalahoi, badala yake kuna udikteta tu unaofanywa na viongozi wa ngazi za juu.

Kuanza kusambaratika kwa kasi kiasi hicho kwa Chadema kulithibitika waziwazi wakati wa ziara ya siku tatu ya Dk. Slaa wilayani Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alikuwa akiwashutumu viongozi wenzake kuwa ni mamluki wa CCM eti kwa sababu tu mahudhurio aliyokuwa akiyakuta huko ni hafifu sana.

Mathalani, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wa Jimbo la Kinondoni walimsotesha ukumbini akiwasubiri tangu saa 4.00 asubuhi hadi saa 6.47 mchana aliposhindwa kuvumilia, akaona afungue kikao chake hicho na kuongea na hao wachache waliofika baada ya wao pia kubembelezwa sana kwa kupigiwa simu zao za mikononi.

Badala ya wajumbe 130 waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho ili kujua nini wanaambiwa na bosi wao huyo, wale waliokuwa tayari wamefika hadi wakati huo walikuwa ni chini ya 50 tu huku wakionekana kutokuwa tayari kumsikiliza kwa muda mrefu isipokuwa vinginevyo.

Chadema ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii ya wajumbe kutafutana kwa simu itaendelea ni hatari wakati wa kuunda Baraza la Mawaziri, alisema na kuendelea: Haiwezekani Rais aje kutafuta Baraza la Mawaziri kwa njia hiyo. Bila kujipanga wakati huu (hakika hali) itakuwa ngumu huko mbele tunakokwenda.

Simshangai Dk. Slaa kuwa na roho ngumu kama ya paka kwa kuendelea kufikiria ndoto ya kushinda uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015 huku chama chake kikisambaratika kila mahali. Kiongozi anayefikiri kwa akili timamu kichwani mwake hakika asingeweza kabisa kuzungumzia suala hilo isipokuwa vinginevyo.

Kama viongozi waliowekwa madarakani ili kukiongoza chama hicho na kuwa kiungo kati ya wanachama, wapiga kura na uongozi wa juu nao tayari wanaonyesha kuwa mioyo yao haipo nacho tena, nani ataendelea kukiunga mkono na ili iweje?

Nimekuwa nawaambia rafiki zangu kuwa tokea mfumo huu wa vyama vingi vya siasa nchini ulipoanza tena mwaka 1992 kama inavyosema Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mpinzani hata mmoja aliyewahi kuwa lulu kwa wafuasi wake kama aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR  Mageuzi, Augustine Mrema.

Alikuwa kimbilio la wengi na kuungwa mkono kila mahali mijini na vijijini. Aliteka hisia za kina mama na vijana, matajiri na masikini, wasomi na watu waliosoma katika viwango vya kawaida na kadhalika.

Ndiyo maana gari lake akimaliza kuhutubia mikutano ya hadhara hasa mijini kama Dar es Salaam lilikuwa likisukumwa na mamia ya vijana, tena kwa hiari na matakwa yao wenyewe hata kwa zaidi ya saa nzima mpaka wanapokuja kusambaratishwa na polisi waliofanya hivyo ili kumlinda dhidi ya vibaka, wezi na waporaji wengine linapoanza giza.

Lakini baada ya kutamba kwa miaka minne mfululizo akiwa katika hali hiyo kuanzia mwaka 1995  1999, Mrema aligunduliwa kuwa ni msanii, muongo, mzushi, mchochezi na mtu anayependa zaidi kusifiwa binafsi na kutumia kila aina ya ujanja wa kisiasa kuwadanganya wafuasi wake.

Hapo ndipo umaarufu wake wote uliposambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo na kubaki na kikundi kidogo cha watu waliokuwa na maslahi naye wenyewe. Hao wanaendelea kumuunga mkono hadi leo na wengine kati yao wapo radhi na tayari hata kumfia utadhani kupe linavyongangania kwenye ngozi ya mnyama hususan ngombe, mbuzi ama kondoo bila kuiachia hata kama tayari ameshakufa!

Hivyo ndivyo wanavyofanya wafuasi wa Chadema wakiwemo baadhi ya wasomi, ngumbaru na kadhalika. Wengine wamejitokeza mstari wa mbele kuthibitisha umahiri wao wa kuitetea kwa uongo, uzushi na majungu.

Wanafanya hivyo kwa kuelewa matumaini hewa wanayolishwa na viongozi mbalimbali wa Chadema hususan Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa ambaye amethibitisha kuwa ana uwezo mkubwa wa ghiliba, uzushi na kufanya kila aina ya siasa za kisanii na chafu.

Amejitokeza kuwa mstari wa mbele kusingizia chochote, wakati wowote na mahali popote ili mradi anakidhi matakwa yake ya kutafuta umaarufu kwa njia zote anazozijua mwenyewe, mtu ambaye siku zote amekuwa akiishi kwa kutegemea majungu, umbeya na uzandiki kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali na viongozi wake wakuu.

Amekuwa tanuru la kupikia uongo, uzushi, fitina na kutengenezea kila aina ya hasira na chuki kwa wananchi, lakini anafanya hivyo siyo kwa ajili ya maslahi ya nchi yake, watu wake wala chama chake ila yake mwenyewe kwa ajili ya tumbo lake na matamanio yake mengine.

Tayari hali imekuwa kinyume baada ya miaka miwili tu ya wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema kukiamini chama hicho kwa mkumbo na kudanganywa na hivyo wengi wao wameanza kukiasi.

Mbali na viongozi waandamizi waliokihama katika mikoa ya Arusha, Singida na Morogoro, mgogoro mzito unaofukuta katika Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam kati ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe dhidi ya Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Zitto Kabwe ni miongoni mwa majanga yanayofukuta chini kwa chini.

Kana kwamba haitoshi, mgogoro mwingine uliopo ni kati ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Heche dhidi ya Afisa wa Kurugenzi ya Sera na Utafiti, Mwita Waitara na Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Sonza.

Tayari pia mgogoro huo umeanza kuenea nchi nzima ambapo kwa mfano, Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Eddo Mwamalala, uongozi wa Bavicha wa Mkoa wa Mwanza mbali na sehemu nyingine, wanamtaka Dk. Slaa ajiuzulu kwa madai kuwa anakivuruga chama hicho.

Ndiyo maana sasa amechanganyikiwa kiasi cha kupayuka bila mpangilio wowote mdomoni ikiwemo kudai eti CCM inapofanya ziara zake inakuwa inaiiga Chadema, jambo ambalo hata mwendawazimu wa akili hawezi kulitangaza.

Haiwezekani kwa namna zote kuwa viongozi wa CCM ambayo ilianzishwa mwaka 1977 wawe hawajafanya kabisa ziara hadi walipoiga Chadema wiki tatu zilizopita!

Ndiyo maana Dk. Slaa sasa amechanganyikiwa baada ya kuanza kususiwa mikutanoni na viongozi wake, wanachama wake na wafuasi wake huku wengine wakisema wamechoshwa na udikteta, kuburuzwa kusikoisha na siasa za kitapeli anazofanya yeye na viongozi wengine wa kitaifa.

Katika hali hiyo na hata vinginevyo ndiyo maana wameanza kukikimbia chama hicho huku wakisema waziwazi kuwa kinasambaratika, na kwamba miaka miwili iliyotumika kwa kuwajaza fitina, uzushi, uongo na kila aina ya ghiliba tokea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 imetosha, na sasa arobaini ya Chadema hatimaye imewadia!

Another masalia at work,haya na wewe unahitaji kusaidiwa ili uache kutumika.shame on you kama vile yalivyomkuta jaji Rwakibalila na kesi ya Mh lema mb,arusha mjini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom