Kiukweli si vyema na sipendi kuwatukana wazee....... Lakini Arfi ni Mpumbavu
habari za siku nyingi mkuu .Dhambi ya usaliti itawatafuna hadi kaburini.shetani hanaga jema.hutafuna hata mawakala wake
Kiukweli si vyema na sipendi kuwatukana wazee....... Lakini Arfi ni Mpumbavu
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Ndg.Said Amour Arfi ambaye alijiunga na Chama cha mapinduzi (CCM) hivi karibuni amesema anafikiria kujiondoa CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani (hakukitaja jina), kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli ndani ya CCM.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu, Arfi amesema alijiondoa CCM mwaka 2000 na kujiunga na TLP kwa sababu CCM haikua na demokrasia, hivyo alitegemea miaka 15 aliyokaa nje ya CCM ingeweza kuibadilisha lakini hadi sasa hali ni ileile.
Arfi alitupwa nje kwenye kura za maoni ndani ya CCM kupitia jimbo la Mpanda Kati ambalo ameliongoza kwa miaka 10. Hata hivyo anafikiria kutetea kiti chake hicho cha ubunge kupitia chama kingine nje ya CCM. Watafiti wa masuala ya siasa wanasema huenda akajiunga na ACT wazalendo.
Arfi alikuwa mwanachama wa CCM hadi mwaka 2000 alipoondoka na kujiunga na TLP. Mwaka 2005 alijiondoa TLP na kujiunga CHADEMA ambapo alipata fursa ya kugombea Ubunge na kushinda kwa vipindi viwili mfululizo.
Mwaka huu alijiondoa CHADEMA na kurudi CCM, lakini ameangushwa kwenye kura za maoni na hivyo anafikiria kuondoka CCM na kujiunga na chama kingine cha upinzani ambacho hakukitaja.
Mwaka wa kufa Nyani miti yote uteleza...
Atatuliaje na maslahi hayajakaa sawa mkuu🙂...Tanzania yetu imejaaa wanasiasa masilahi! Hakuna 'visheni' wala 'falsafa'.
Atajuta kuondoka CHADEMA, mpuuzi huyu. Ni heri kuondoka chama tawala na kuja upinzani kuliko kuondoka upinzani kwenda tawala....huyu mzee ubunge atausikia redioni na TV. Acha dunia imfunze, ndio ajue CCM walikuwa wanamrubuni akadhani wanampenda akasaliti CHADEMA. Na akome!!!
​Posho za Bunge la katiba zilimdanganya SISIEM wakamuhadaa
awenasubira huenda wakamfikiria vip maalum
Ni hofu hiyo mkuu anatafuta basi litakalomrudisha mjengoni.
shikamoo ccm. Maana kwenye bunge la katiba alijifanya kidume eti anatetea wananchi. Ametumika kama ile mipira sasa hana la kufanya. Ccm ndivyo wanavyowaua kisiasa kwa vipande vya pesa
Hasira hasara...Pole Arfi...
Hope ni kqti ya wale 38,000 waliojiunga CCM na wameanza kurudisha kadi.Ikifika October 2015 nadhani watakuwa wamekwisha
Unafiki na undumilakuwili unamsumbua huyu arfi. Wanampanda mkataeni huyo
Kwani hajui chama kinachopokea wanaokatwa tu? Arudi tu asione aibu