Bila shaka wote mu wazima wa afya..kama heading inavyojielezea hapo juu ni swali nililokuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa kama uwezo wa hawa watu huwa ni wa mafunzo au wanazaliwa wakiwa tayari na hizi attributes?
Ninawasilisha+++
it is both
dah!
mara nyingi kunakuwepo na viashiria ambavyo vinaweza onekana tangu udogoni.
viashiria hivi vinaweza kuwa kutambuliwa na mtu wa familia ambaye tayari yuko kwenye system. ikitokea hivi na huyo mtu wa familia akaona utafaa basi anaweza akawa "anakulea" na kukujenga ili baadae iwe rahisi kukushawishi kuingia huko.
aidha viashiria hivi vinaweza kuonekana katika mfumo wa makuzi na elimu, mfano mwalimu wako, jirani yako, ndugu wa rafiki yako n.k.
pia wapo wataalamu kutoka ofisi kuu ambao nao wanajukumu la kutambua vipaji (potential candidates).
baada ya "kuonekana" unafaa inakuja ushawishi na kukujengea mazingira ya utakapo fuatwa na kuombwa kujiunga usisite kukubali. miaka ya awali chuo kikuu na jkt vilikuwa viwanja vya mawindo kwa watu wa "taaluma". mkufunzi kutoka makao makuu alikuwa na "warsha" ya siku moja na wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuwaelezea umuhimu wa usalama hii ilikuwa ni mbinu ya kuwatayarisha wanafunzi kifikra ili wanapofuatwa wasisite kujiunga (ikumbukwe wakati huo chuo kikuu kilikuwa kimoja tu, hivyo hapo ndio palikuwa na jumuiko la wasomi wetu). idm mzumbe pia ulikuwa uwanja wa ajira(ingawa wakati huo haikuwa chuo kikuu)
kwa maneno mengine mtu anazaliwa na viashiria lakini viashiria hivyo lazima viboreshwe. usisahau kila sehemu hawa watu wapo kuanzia walimu, madaktari, wahandisi, wachumi, wahasibu, viongozi wa dini, wanasiasa nk. hata watu wasio na taaluma mahususi pia wapo. japokuwa kama alivyosema mchangiaji moja hapo juu sio kila mwenye viashiria ameajiriwa au ameonwa. wengine wanaviashiria husika lakini mazingira ya malezi/makuzi yao yamefanya wawe na viashiria vingine vyenye nguvu zaidi hivyo kuwa disqualify.
naamini nimekusaidia kidogo
Mi kinachonishangazaga kuhusu watu wa aina hii, jinsi wanavyojua kufanya kazi yao, ni pale mtu anapojifanya kichaa, ombaomba, shoeshiner, mvuta bhangi n.k ile kupata information fulani, unakuta mtu katokea Mwanza anakuja kujifanya kichaa Dar, hakuna anayemjua, anaifanya kazi yake saaafi, akimaliza anarudi alipokuwa(ofisini Mwanza), kuna mtu alishakwepwa na mtu posta ambaye alishawahi kuwa kama kichaa mtaani kwao kwa muda then akatoweka ghafla, yaani watu walishangaa mtaa ghafla umepata kichaa wasiyemjua, wakawa wanampampa vyakula vyakula,muda mfupi baadae ghafla akatoweka, siku hiyoaliyomuona posta alitaka amfuate amsalimie, akakwepwa, alimshangaa cause alikuwa amepiga nguo smart za ofisi, akajua yule hakuwa kichaa kweli kuna mtu alikuja kumfuatilia mtaani kwao, alipowaambia wenzie mtaani hawakuamini, eti yule kichaa kamkuta that smart mjini wakati alikuwa anavaa nguo chafuchafu na kulala nje mtaani kwao
Sasa yale makeke kama ya kucheza na gadgets, dead drops, planting and clearing surveillance bugs, surveillance detection techniques na tailing a subject hizo ni mpaka uingie huko chuoni kwao au unafuliwa mtaani ambapo ndio kama field zao?
Mambo kwa hatua (awamu), mtoto hukaa, hutambaa, husimama, hutembea, hukimbia nk. Kwa hatua/awamu muda muafaka ukifika.
Unalidhalilisha jina unalotumia kwa swali unalouliza au kushangaa!
Halafu usipekenyue saana... "Utapata homa ya dengue bure!,"
Mostly born n' made
Kweli inahitaji moyo wa ajabu sana na akili nyingi kweli kweli aisee! Kwenda kujifanya kichaa sehemu si kanzi ndogo atii.
Kweli inahitaji moyo wa ajabu sana na akili nyingi kweli kweli aisee! Kwenda kujifanya kichaa sehemu si kanzi ndogo atii.