Are spies made or born?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Special thread for discussing espionage business and other closely related issues:

Bila shaka wote mu wazima wa afya humu JF.

Kama ambavyo heading inavyojielezea hapo juu ni swali nililokuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa kama uwezo wa hawa watu (spies/intelligence officers) huwa ni wa mafunzo au wanazaliwa wakiwa tayari ni spies?

Ninawasilisha mjadala.
==========

Mchango kutoka kwa mdau
Niliwahi kutaja sifa za mtu anaefaa kuwa jasusi..nitazirejea kwa kifupi..

1. Jasusi lazima awe na kumbukumbu.. Hii ni sifa muhimu sana lazima akili yake iwe ina rekodi kila jambo na kila hatua anayopitia na kwa usahihi.. Kuanzia asubuhi ambo yoote unayofanya/unakpita unarekodi kisha jioni unaandika report ya kila kitu bila kuacha na pia ukiulizwa jambo lililotokea wiki mbili zilizopita ulikumbuke kwa usahihi na kwa mapaa yake.. Kuna watu hawana kumbukumbu yaani hata kushika namba 5 za simu hawezi.. Binafsi sina jina la mtu yeyote kwenye simu yangu bali namba tu na ninajua namba hii ni ya nani na hata kuitaja.. Niliifundisha akili katika hilo.. So, kumbukumbu ni sifa muhimu.

2. Lazima Jasusi afikiri kuwa mantiki (logic).. Lazima ujiulize kwanini hiki kiko hivi na ninaweza vipi kukibadilisha katika muonekano huu na kikawa kitu kingine, kufikiri kwa logic ni muhimu sana na katika kufikiri lazima ujiulize; Why, who, where, what etc... Ukiwa mtu wa kukurupuka lazima uumie..

3. Lazima awe mtu wa kuchunguza (observation).. Haijalishi mahali alipo lazima achunguze mazingira na nini kinaendelea.. Ukiingia ndani ya nyumba lazima uichunguze kwa muda mfupi na kwa umahiri mkubwa ujue ina milango mingapi, madirisha, nk nk.. Akili lazima iwe ina rekodi na lazima uangalie escape route iwapo kutatokea shida mlango ulioingia sio wa kuutegema sana..

4. Jasusi lazima ajue kubadilika kulingana na mazingira au eneo alilopo.. Awajue watu wanaomzunguka wanataka nini na ni wa aina gani.. Jasusi lazima ajue kucheza na hisia za watu (sifa muhimu sana hii).

5. Jasusi lazima ajue kusikiliza milango yote 7 ya fahamu (sio 5 ni 7).. Katika ubongo wa mwanadamu kuna maelekezo mengi sana yanayomuonya mtu juu ya jambo flan (wengine wanaita machale). Machale haya humuonya mtu juu ya hatari iliyo mbele so ni lazima jasusi ajue namna ya kusukiliza milango yake yote na kuchukua hata inayostahili kama yu katika hatari!

Hapo ni baadhi ya sifa anazopaswa kuwa nazo jasusi.. Sasa ukiangalia sifa hizo hakuna hata moja hapo ianayofundishwa darasani zote ni za kuzaliwa... Na kwa kweli wote tunazaliwa tukiwa pure isipokuwa tunajaza uchafu mwingi kwenye ubongo na kuharibu nguvu ya akili... Hata katika maisha ya mtu wa kawaida tu, sifa hizo hapo juu ni muhimu sana.. Huwezi kuyatawala mazingira kama huna utulivu wa akili.... The mind is a good servant but a terrible master. Lazima akili yako uitawale na uitume ifanya jambo flani sio yenyewe ikutume wewe kufanya jambo flani..

Sasa ukiwa na sifa hizo hapo juu na zingine ambazo sijazitaja kisha ukaingizwa darasani na kunolewa sawa sawa, lazima ufanye mambo makubwa..

Ndugu zangu, mambo haya huwa hayaji hivi hivi.

Ni lazima ujitume katika kuhakikisha akili yako inakuwa sawa muda wote na u-keep low profile, upayukaji hauhusiki, majigambo, n.k. Ukiishi kama mastaa wa movie huwezi chukua round katika game hii...

Kwenda kwenye vyuo vya mafunzo haya. Huko unaongezewa mbinu mfano za kutumia silaha za aina zote, namna ya kujihami, namna ya kugoma kuhojiwa iwapo utakamatwa.

Mazingira ya ujasusi yamezungukwa na hatari, ukiwa, upweke na kivuli so ni lazima jasusi ajifunze mbinu zoe za awali za kazi hii (trade craft).

Kwahiyo naweza kusema kuwa watu hawa sifa kubwa ni zile za kuzaliwa kisha wanaingizwa darasani/vyuoni ili kupewa mafunzo kufit mahitaji yaliyopo.

Nimalize kwa kunukuu maneno ya mwalimu wangu:

1. When you control your thoughts, you control your mind. When you control your mind you control your life; and once you reach a stage of being in total control of your life you become the master of your own destine.

2. Always life favors the prepared mind

3. In life there is no mistakes but lessons... Sometime pain can be a good teacher.

NB: Mwambieni Invisible auweke uzii huu sticky maana kuna muda nautafuta siupati
 
Katika uasilia, angalia mfano wa wadudu wadogo mfano sisimizi na jamii yake, nyuki nk.

Utajifunza kuwa askari huzaliwa.

Ukiwa na bahati ukaonwa na kutimiza vigezo vingine utapatiwa mafunzo...

Tunao 'askari' wengi mitaani lakini hawakubahatika kuonwa au kupata mafunzo ama vigezo havikukamilika lakini ikiwaona tu utahisi wangefaa kazi ya uaskari...

Kwa 'spies' vivyo hivyo lakini lazima uwe 'flexible' na 'little more intelligent'. Vyoye hivi ni kwa kuzaliwa, mafunzo huwaongezea uweledi...

Kujibu swali, '...spies are born and made...'

However: Katika nchi corrupt kuna uwezekano wa kukuta spies wasiostahili, yaani ambao IQ zao zipo chini sana...
 
Nadhani huwa kunakuwa na vyuo vya kuwasuka hawa jamaa..sasa kama hao wa secondary wanakuwa wapitaje katika hivi vyuo?
Wanajua wao wanawatrain muda gani, mtu unaandaliwa kufanya kitu fulani mapema, ndio maana form three unachagua science, form five unachukua PCB ili Chuo ukasomee Udaktari, uwezi ukachukua HGL form five Chuo ukataka ukasomee Udaktari, maandalizi ni mapema, ingawa kwa hawa watu ni wao wanaokuappriciate na kukuingiza humo taratiibu mpaka unaiva na kuwafaa, sio unajiingiza mwenyewe, unaamua kusomea mwenyewe au kama unavyoenda kuomba kazi Bank, no, unaweza ukawa hata mtu mwenye Masters, wasikufagilie, kwa kuwa hauwafai, lakini wakamtrain form four leaver akawafaa, but unafuatiliwa muda sana mpaka kuingizwa huku, hawakurupuki, yawezekana anayekufuatilia ni mwanafunzi mwenzako ama Mwalimu wako ambaye naye yumo tayari
 
Sasa nimeanza kupata picha kwa mbaaaali lakini bado ninajiuliza how do they get to train teenagers? Au hawa wanafunzi wanakuwa recruited unknowingly?
 
Katika uasilia, angalia mfano wa wadudu wadogo mfano sisimizi na jamii yake, nyuki nk.

Utajifunza kuwa askari huzaliwa.

Ukiwa na bahati ukaonwa na kutimiza vigezo vingine utapatiwa mafunzo...

Tunao 'askari' wengi mitaani lakini hawakubahatika kuonwa au kupata mafunzo ama vigezo havikukamilika lakini ikiwaona tu utahisi wangefaa kazi ya uaskari...

Kwa 'spies' vivyo hivyo lakini lazima uwe 'flexible' na 'little more intelligent'. Vyoye hivi ni kwa kuzaliwa, mafunzo huwaongezea uweledi...

Kujibu swali, '...spies are born and made...'

However: Katika nchi corrupt kuna uwezekano wa kukuta spies wasiostahili, yaani ambao IQ zao zipo chini sana...

Thanks mkuu nimepata uelewa kidogo hapo!
 
Mkuu wale jamaa kwa nchi za wenzetu huwa wanazaliwa wakiwa na baadhi ya attributes/tabia fulani hivi kisha wanaongezewa tradecraft/ujuzi wa kimafunzo...baada ya hapo weeee wanakuwa ni moto wa kuotea mbali...!

Daaah kweli balaaa..nimekusoma mkuu!
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom