Are our men failing us? Labda 'Strong Men' Extinction?

Are our men failing us? Labda 'Strong Men' Extinction?

mimi sitaki kujiaminisha hivyo....
najua wapo wengi tu, ila sisi hatuoni tumpe nani, kwa maana hiyo kosa ni letu.
kati ya vitu sitaki hasa kwa ngazi ya nyumba yangu ni mimi kiwa kichwa cha nyumba, sitaki kabisa

Tatizo tunapendekeza kwanza watu wanaofaa kutuongoza badala ya kuangalia maslahi ya taifa ni yapi kwanza kisha tuangalie nani ana sifa za kuweza kutimiza hayo maslahi then ndio tumteue aingie kwenye kinyang'anyiro lakini sie watz tunachofanya ni kuangalia mtu kwanza alafu ndio tunampa majukumu ya kutuongoza kwa kuangalia kigezo cha anajua kujenga hoja vizuri wakati tunasahau kwamba kule anakokwenda tunachohitaji ni mtu wa kufanya maamuzi na si kubishana.

Mbaya zaidi tunawapa watu madaraka ya kuongoza wizara au taasisi mbalimbali bila kuangalia uzoefu wake katika kuongoza hata taasisi ya watu 15 tu au kuweza kusimamia budget angalau ya milioni 10 kwa mwaka, ukichanganya na kujuana basi balaa anakua anaendeshwa kwa remote control.
 
Okay.

Nimeanzisha hii mada kusudi, kujaribu kuangalia, ni kweli gender ina mantiki kama ilivyodhaniwa na jamii?

Ndio maana nikauliza kuna haja ya kuangalia mambo kwa mtazamo mpya?
Kuondoa dhana za strong men na kuja na mbadala wa partnership.

Wafanye maamuzi kwa kikao gani cha pamoja wanachofanya?

Strong men wameandaliwa kuongoza jamii na manufacturer gani? Na kwa nini strong men na si strong women?

The Bangladeshi women are leading their society and they have plenty of problems. some Scandinavian countries have some very pro-women policies, down to quotas in parastatal boards, they also have their own set of problems.

Hao wanaume waliokosa muelekeo wanalelewa na baba zao tu? Mama zao wako wapi na wameachiaje malezi yazorote kufikia hapa?

Ukifikiria mambo haya in the abstract lazima matatizo yaendelee tu, huwezi kupata suluhisho kwa sababu namna ya unavyofikiria kupata suluhisho ni sehemu ya tatizo.
 
kabla sijasoma michango ya wengine na pengine kuathiri view yangu; naomba kuchangia kama ifuatavyo.
strong men hawajaisha, ila definition ya strong men ndio haiko shared na wote au wengi.

head wa families wapo, lakini kama ilivyo kwa 'strong men', basi hata definition ya family haipo shared na wote.

ilikuwa ni zamani ambapo, kiongozi wa kabila, nchi alikuwa anaona wale anawaongoza kama ni familia yake na anapaswa hasa kuangalia future ya hiyo familia na anajisikia vizuri sana kama akiweza kuacomplish kusecure future nzuri ya hilo kabila au nchi hata kama kwa gharama ya tone lake la mwisho la damu.
Tofauti na sasa ambapo kiongozi ni mnyonyaji wa kundi analoliongoza while securing great future kwa familia yake nikimaanisha BMW (baba mama na watoto) hata kusahau extended family.
Gone are the days when, watu walikuwa wanabembelezwa kuongoza; lakini sasa watu wanaua ili waweze kutawala.

So Kongosho kwa kiwango kikubwa nakubaliana nawe, lakini definition ya strong men lazima iwe clear kwa kweli, maana to some, yule ambaye anaonesha ubabe can be regarded as strong man na kina nyerere wanaweza kuonekana ni wajinga ambao wameshindwa hata kuahakikisha future ya watoto wao inakuwa secured.


exactly
kama watanzania bado hatujawa one familly
tuna makabila,dini,na mengineyo yanayotugawa

tazama Kenya kina Raila ni leaders wa makabila yao,
wanaheshimika in a unique way au unaweza sema in a very unfair way...

sisi bado tunagombania keki ya taifa kwa tofauti zetu...
 
Okay.

Nimeanzisha hii mada kusudi, kujaribu kuangalia, ni kweli gender ina mantiki kama ilivyodhaniwa na jamii?

Ndio maana nikauliza kuna haja ya kuangalia mambo kwa mtazamo mpya?
Kuondoa dhana za strong men na kuja na mbadala wa partnership.

Of course kuna haja. Hapo ndo mzizi mzima wa tatizo ulipo.

Ukishaanza na habari za "baba ndiye kichwa cha familia na kiongozi" tayari una defeat the entire purpose of marriage.

Watu wawili kuwa pamoja na kuongoza familia yao pamoja.

Badala ya viongozi wa familia kuwa wawili wanachekecha mambo na kushauriana unamtoa mmoja anakuwa kama pambo, unambakisha mmoja.

Ushapunguza brainpower ya uongozi wa familia kwa 50%.

Na tushaona how power corrupts, and how absolute power corrupts absolutely.

Unavyozidi kumuweka baba pale juu kama "kichwa cha familia" ndivyo unavyozidi kumpa nguvu za udikteta na unavyozidi kuongeza uwezekano wa maamuzi mabaya kupita bila kupingwa.
 
Sasa unategemea nini
kama vijana wanaona wanaume/wababa wengi wa kuwaiga ni wale walegevu
legevu wanao-lack strong characters, morality and values. Inasikitisha
lakini lazima nao waishie kuwa kama hao wengi.

Kama Jk ndo role model wanaume watatoka wapi Kongosho?
 
Last edited by a moderator:
strongmen are still there!ni huu upepo wa globalization na rise of women kudai equality unafanya sometimes tuconsder the other side.

mfano unaenda kuomba kazi unakuta ofisi inasema equal opportunity! lakin pale hawamaanishi hivyo, wanamaanisha watamconsider zaidi mwanamke kuliko mwanaume.na hii imeinga kwenye nyanja zote za jamii.

tunafanya kuwaprotect in almost everything nowadays kwa maana mnadai haki zenu zimeminywa na mnalalama sana mpaka kuandamana.sasa kwa men inakua kero tunaona ngoja tuwape opportunity ya kufanya maamuzi,tumejaribu kwa spika wetu nadhani tumeona, mh.sitta na wenzake walichujwa kisa waliambiwa sasa ni zamu ya wanawake na matokeo yake tunayaona.

ifike wakati wanawake mkubali nafasi zenu ili tuact kama strongmen kwani malalamiko yenu yamezidi
 
TZ imekumbwa na magonjwa mengi sana ikiwemo
UDINI
UKABILA
UVYAMA
sasa tutahamia UJINSIA
 
Back
Top Bottom