Ardhi yetu hatujaweza kuitumia vizuri...

swadakta mkuu umenena vyema watu wanajuhudi sana ila wakati mwingine wandondoshwa na waliopo juu, awali ya yote ni masoko nikiwa ka mtu wa masoko hili ni jambo ambalo naliona na si kilamtu anaweza tafuta masoko unadhani mtu aliye mbinga anaweza/anaufahamu wa masoko ya nje? ni wakati serikali nayo iwatafutie wananchi wake masoko ya uhakika ya nje na ndani ya nchi ambayo yatawafaa wakulima. isijekuwa ka yale ya mihogo ya Lushoto (japo walikuja pata soko baadae ila sijui soko linaendeleaje) pia pembejeo si ziwe dar na miji mikubwa ambako hakuna hata mashamba. pembejeo ziwe kwa walengwa na kwa muda mwafaka, Mengine umeyasema mkuu nadhani serikali yetu nayo itoe macho pima
Mkuu wanaouza mazao yote ni wafanyabiashara wakubwa ambao hununua na kuandaliwa huko huko mashambani na kuletwa mjini tayari kusafirishwa
Jukumu la serikali ni kuhakikisha inaangalia ubora na kutoa vibali kiurahisi ili nao wapate kodi yao
Uchumi tunao tumeukalia

Mkuu ni serikali ndio inashindwa kusaidia wananchi kwa kuharakisha vibali
 
Mkuu technology siku hizi imekwenda mbali, kuna majembe ya palizi yanayotumia diesel. Si makubwa ni kama kwanja na tank unalibeba mgongoni.
Unaweza kupalilia heka moja kwa siku moja.

Vitu kama hivi vingeletwa na kuuzwa kwa wakulima kupitia wizara ya kilimo vingebadilisha kabisa ulimaji wetu.
Ndio maaana nikasema nakuja kumalizia pandiko langu, anyway nilikuwa najenga hoja kumjibu mdau namna gani technologia ambavyo Ni kikwazo kwenye kilimo chetu kuwa Cha kishindani......
Maaaana huwezi Lima mpunga hekari 800+ huna bila nyenzo stahiki ukategemea utavuna mazao ya kutosha...
Ukivuna kidogo maaana yake sokoni Bei yako itakuwa juu kuliko waliovuna Sana(mavuno÷gharama=Bei) efficiency in productions led to fall in product/unit cost, ndio maaana Thailand wanaweza kuja kuuza mcheza tz ukawa na Bei ndongo kuliko wa Moro japokuwa wanalipa na import levies
 
Suluhisho la kilimo chetu ni processing. Kama tutaendelea kuuza mazao ghafi, kilimo hakilipi. Niliwahi kulima tikiti. Matunda yalikubali vizuri. Nikapakia fuso nikaingia nayo sokoni buguruni. Kilichotokea hskifai kuandika hapa. Mwaka jana nilivuna vitunguu magunia 700@ kg 100. Nikikuambia mapato yake utanitukana.
Matikiti ilikuwaje mkuu...kwanza tuanzie happykilimo Cha Tanzania kunahitajika uwe na moyo wa plastiki....
 
Back
Top Bottom