Bradha
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 8,787
- 45,248
lini?Sirikali imetoa milioni hamsini (50million/=) kila kijiji mmezifanyia nini?
Tuanzie hapo kwanza.
lini?Sirikali imetoa milioni hamsini (50million/=) kila kijiji mmezifanyia nini?
Tuanzie hapo kwanza.
Hivi unaanzaje kuuza mazao nje bila support ya serikali. Kwa point yako hapo juu ningehoji kazi ya serikali kwa wakulima wa ndani, mara ngapi serikali inapiga marufuku uuzwaji wa mazao nje!?.
Haya yanawezekana kutokana na diplomasia iliyopo kati ya pande mbili, angalia jinsi wafanyabiashara wa China na USA walivyokuwa na hali tete kisa serikali zao. Hapa kwetu serikali ikipiga marufuku kuagiza magari toka japan ni nani ataweza bishana nayo!?.Ni kama unavyoagiza gari Japan. Unahitaji serikali ikutafutie mtu anayeuza gari? Hapana.
Kama kwa mfano unataka kuuza vitunguu nje unafanya utafiti mtandaoni kuhusu wananuzi wa vitunguu Comoro etc. Kisha unatafuta kibali kama kinatakiwa, unapanga usafiri wa mzigo, na unapekeka (baada ya kupokea fedha ambazo mnunuzi atakuwa ametuma kwenye akaunti yako.
Si vema kusubiri serikali kwa kila kitu.
Umeshaonja Maganjo? Ni somber safi sana na packaging ni bomba. Wanapack kwenye plastic bag ndani alafu paper bag juu ina nembo na maelezo juu ya kilimo cha unga unaokula.Iwisa wapo juu hata Tesco wanauza pia na unapata kila mahali mpaka Amazon
Hili la Bakhressa kuna wakati aliingiza na UK na watu waliishambulia container halikuchukua masaa liliisha
Sijawahi kusikia tena kaleta sijui huwa tunakwama wapi
Watu walivyogombania sikutegemea ndio utakuwa mwanzo na mwisho wake
Kwa biashara kwa kweli tuko nyuma sana
Sijawahi kuula huo kwa kweliUmeshaonja Maganjo? Ni somber safi sana na packaging ni bomba. Wanapack kwenye plastic bag ndani alafu paper bag juu ina nembo na maelezo juu ya kilimo cha unga unaokula.
Kama kuna atakaewaza kupeleka unga wa Ugali Ulaya una pesa sana.
Nakubalia na wewe moja kwa moja kwenye suala la serilkali kusaidia kusaidia kutafuta masoko nje na ndani ya nchi.......Na mimi nakubaliana na wewe. Labda nianze kutoa angalizo: Hawa wanaobeza ujenzi wa reli ya kisasa wamesoma thread yako?
Back to the topic: Kuna mchangiaji mmoja kasema kuna nchi wakulima wanatafuta masoko wenyewe, hivyo si jukumu la serikali kuwatafutia! Mimi nitatofautiana naye kidogo, japo sipingi kuwa yuko sahihi. Serikali nzuri ni ile inayojua weaknesses za raia wake na kuzifanyia kazi. Hili la wakulima kutokuwa na knowledge ya masoko bado serikali inaweza kusaidia. Kwa mfano mabalozi wa Tanzania walioko ughaibuni kufanya uchunguzi wa demand ya mazao mbalimbali na kuja info zitazosaidia wakulima wetu. Vinginevyo thread yako ni nzuri sana na Tanzania kama kweli tunataka maendeleo ni basi tuwekeze kwenye kilimo. Tuna ardhi na hali ya hewa nzuri sana. Na zaidi uwekezaji wa kilimo hauhitaji mtaji mkubwa na complex technology kama uwekezaji mwingine. Hata hii inayoitwa Bandari ya Bagamoyo na mazagazaga yake yote (huku tukiwa tumeweka reheni ardhi yetu) haina faida na si rahisi kama kilimo. Kuna mradi kama wa Lower Moshi irrigation (ukulima wa mpunga) uliojengwa kwa msaada wa Japan. Mwanzoni ulibadilisha familia nyingi zilizopata bahati ya kuwa kwenye ule mradi na ufukura ukawa umepunguzwa kwa kiwango kikubwa. Lakini baada ya Japan kuondoka, sisi wabongo tumeshindwa kuundeleza na umekufa kabisa.
Mkuu technology siku hizi imekwenda mbali, kuna majembe ya palizi yanayotumia diesel. Si makubwa ni kama kwanja na tank unalibeba mgongoni.Nakubalia na wewe moja kwa moja kwenye suala la serilkali kusaidia kusaidia kutafuta masoko nje na ndani ya nchi.......
Ila kidogo ninatofautiana na wewe kusema kuwa kilimo hakihitaji mtaji mkubwa na complex technology........
Moja ya changamoto kubwa kabisa inayowapata wakulima wanaolima mashamba makubwa (hela 80 na kuendelea) hapa tz, (siyo namna ya kuyalima/trekta,mbegu na madawa vipo angalau) ishu Ni
*PALIZI, kwa shamba lote kwa wakati(kumbuka llimelimwa kwa trekta sasa unapalilia kwa jembe mkono) humu ukishindana na mvua,muda na magugu yanayoendelea kukuwa kwa Kasi na kuasili kuwaji wa mazao husika.
*UVUNAJI, bado tunavuna kwa mkono mazao karibu yote tunayolima inchini, kwa shamba la hekari 100+ gharama za kuvuna kwa mkono zinakuwa juu Sana ukisema uwekeka watu wengi ili kuvuna kwa haraka na ndani ya muda, vinginevyo mazao mengi Sana yanaharikia shambani(kwa upepo,wadudu/ndege,jua na mvua)... Morogoro watu huwa walia mpunga kipindi Cha kuvuna mvua ndo zinapamaba Moto...
*Miundo mbinu ya kuhifadhia mazao Ni duni,hivyo mazoa mengi Sana pia hupotea hapa
********Nakuja kumalizia*********
mkuu umesema vyema ila kunawatu wanlima sana tena sana hasa haya mahindi ila soko lipo bei ndogo na mipaka ikifungwa bei ndo inakuwa ya kutupwa ka mtu alilima kwaajili ya biashara anasota kwa muda mpaka mipaka ifunguliwe, serikali inashauri wauze finish goods it ok ila mfanya biashara ambae kashapigika na anawaza hela tuu baada ya soko kufunguliwa atawaza hayooo? hata kama utaratibu bado haujawa mzuri kihivyo kwahiyo kunamengi ya kuangalia tupeleke bidhaa ya mwishoUshauri :
1. Kutafuta soko la ndani na nje. Jinsi tutakavyoweza kusafirisha local products national wide.
2. Jinsi ya kutoa mafunzo ya kilimo bora kwa wanaotaka kuanzisha kilimo cha biashara
3. Kuleta simple farming tools, kusema ukweli kilimo cha jembe la mkono kimepitwa na wakati.
4. Tatizo lingine walimu wanaofundisha masomo ya mifugo na kilimo wanatumia akili za miaka ya 1980 kufundisha miaka hii ya 2019.
5. Lingine walimu wanaofundisha masomo ya mifugo na kilimo wao wenyewe unakuta hawalimi wala kufuga hata njiwa.
6. Tatizo lingine ni kuwa na mbadiliko wa mawazo{Mindset}¶
7. Lingine watunga sera, wengi hawana uelewa ktk Maswala ya aridhi, mifugo na kilimo. Mfano mnauona Kati ya wafugaji na wakulima kugombania aridhi na wakati aridhi ni kubwa ila haijapangiwa matumizi vizuri..
8. Kingine vijana hawaaminiwi na serikali pamoja na wazazi ktk kujihusisha na Maswala ya kiuchumi. Wahindi na waarabu kijana akifika miaka 18 upewa majukumu ya kukikwamua kiuchumi tofauti na waafrika.
View attachment 1104354
Umiliki wa ardhi Afrika uliingiliwa na utawala wa kikoloni. Baada ya kupata uhuru nchi nyingi zilishindwa kurudisha ardhi kwa wananchi. Kutokana na misimamo imara ya Baba wa Taifa Tanzania hatuna hali hiyo. RIP.
Tatizo kwetu kiko kwenye matumizi ya ardhi hii. Hii nguvu kazi ya vijana 50% ingetumia ardhi kuzalisha mazao tungeweza za kusambaza matunda, nafaka na mboga Afrika nzima.
Tatizo la kwanza ni masoko, wakishalima watauza wapi? Barabara zetu kwa sasa zinapitika wakati wa jua na mvua kwa 70%. Ni mipango tu ya kuweza kuweza kuzungusha mazao mtu wa Kigoma aweze kununua pears na apple kutoka Lushoto sokoni, wa Mwanza anunue samaki changu dukani, wa Mtwatra ale kabichi na nyanya kutoka Iringa.
Lingine ni elimu ya kilimo. Mafunzo ya kilimo kwa vijana hasa wale ambao haw kusomea kilimo waweze kupata mwongozo.
Makampuni kama GAPEX yalifanya kazi nzuri sana ya kununua mazao kwa wakulima na kuuza nje.mkuu umesema vyema ila kunawatu wanlima sana tena sana hasa haya mahindi ila soko lipo bei ndogo na mipaka ikifungwa bei ndo inakuwa ya kutupwa ka mtu alilima kwaajili ya biashara anasota kwa muda mpaka mipaka ifunguliwe, serikali inashauri wauze finish goods it ok ila mfanya biashara ambae kashapigika na anawaza hela tuu baada ya soko kufunguliwa atawaza hayooo? hata kama utaratibu bado haujawa mzuri kihivyo kwahiyo kunamengi ya kuangalia tupeleke bidhaa ya mwisho
swadakta kabisa ila wengi hatujui mtu yupo shamba huko toka januari mpaka May leo hata akisikia soko la nje anaona giza anajua kuuza na kwenda, serikali iandae mazingira ama ifanye hiyo kazi ya kuyanunua na kuyasafirisha yenyeweMakampuni kama GAPEX yalifanya kazi nzuri sana ya kununua mazao kwa wakulima na kuuza nje.
Hizi si enzi za ujamaa tena, tuwaze biashara ya kununua mazao na kuyasafirisha.
Mazao kama mhogo yana soko sana nchi za nje.
We need education, capital and exposure.
Pia National Milling ilikua muhimu. Fikiria mahindi yakitwangwa na kusagwa na unga kuhifadhiwa kwa ujazo wa kilo 2, 5, 10, 20... ni rahisi kuuzika na pia kuu hifadhi kuliko mahindi kuharibika.Capital is not a problem if you have a bankable business plan.