Apple hawataki tena kutengenezewa Soc na Samsung.

100 others

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
10,683
Reaction score
38,329
Baada ya Samsung kufanya manufacturing ya soc za apple kuanzia processor aina ya APL0098 mnamo mwaka 2007.
APL0278 mnamo mwaka 2008.
APL2298 mwaka 2009 katika iphone 3G.
Na baadaye A series kwa kuanza na A4.
A5 manufactured by samsung
A5X manufactured by samsung.
A6 manufactured by samsung
A6X manufactured by samsung
A7 manufactured by samsung
Apple sikujua waliwaza nini baada ya kutoa A7 kutoka kwa samsung zilizotumika katika iphone 5s,ipad air,ipad mini 2 na ipad mini 3.Walibadili muelekeo wao na kuanza kushirikiana na kampuni la electronics la huko Taiwan linaloitwa TSMC ambapo lilichukua order na kuanza kuzalisha soc kuanzia A8 ambayo ilitumika katika iphone 6 na 6 plus na baadaye katika ipad mini 4 mnamo mwaka wa 2014 sept 9.

2014 oct 16 apple walitambulisha soc yao tena aina ya A8X ambayo ilitengenezwa na TSMC tena na samsung kukosa dili tena.
Soc hii ilitumika katika vifaa kama ipad air 2.

Katika utengenezaji wa A9 hapa apple walitoa order sehemu zote mbili yaani kwa TSMC na Samsung.
A9 ilitumika katika vifaa kama iphone 6s na 6s plus na pia ipad air 2.
Watu wengi walizilinganisha apple A9 ya TSMC na Samsung baadhi ya vyanzo vya habari vinasema kuwa A9 ya TSMC ni bora kuliko ile ya Samsung.
Nahisi hapa ukawa mwisho wa Samsung kutengeneza tena soc za apple.
Kwa sababu kuanzia.
A9x kwenye ipad pro ni manufactured by TSMC.
A10 fussion ni manufactured by TSMC katika iphone 7 na iphone 7 plus 2016.
A10x fussion pia ni manufactured by TSMC katika ipad pro 2nd generation na matoleo mengine ya ipad pro mnamo 2017.

Mpaka sasa nasikia TSMC wameanza kuzalisha A11 chip kwa ajili ya iphone 7s na iphone 8.

Je wanajukwaa mnaonaje apple wataendelea kutoa order kwa samsung kutengeneza chip zao?
Na ni kitu gani kilichopelekea apple wabadili uelekeo na kuanza kuwapa dili nono hilo kwa TSMC na sio Samsung?
Je hilo sio pigo kwa Samsung kukosa dili kama hilo?
Ahsanteni sana.
 
Kaka hili si jukwaa la siasa naona umekosea njia halafu ahsante sana kwa kutambua uwepo wangu ukipenda niite wild spinach.
Pia nadhani ushindani wa kibiashara kuna kipindi apple waliwahi kuituhumu samsung kwa kucopy technology yao wakati wakutengeneza vifaa walivyo order na kuitumia bila idhini yao.
Kuna siku niliwahi fungua ipod nikakuta memory ya hiyo ipod ilikuwa manufactured by samsung.
 
Wengi tunaielewa Samsung kwa upande wa simu na TV, lakini Samsung ni group of companies, wanatengeneza vifaa mbalimbali vya electronics, ujenzi wa majumba, barabara, injini za ndege n.k

Kwa muktadha huo Apple anamuhitaji zaidi Samsung hasa kwenye utengenezaji wa vifaa vya electonics kuliko Samsung anavyomhitaji Apple japo wote wanagombania soko hasa linapokuja suala la simu.
 
Mbaya zaidi huwa kuna mashabiki michuzi wa apple hawaelewi chochote humu,ni wabishi balaa.
 
Mbaya zaidi huwa kuna mashabiki michuzi wa apple hawaelewi chochote humu,ni wabishi balaa.
Apple wana outsource vitu vyao baada ya kufanya designing na kutengeneza prototype.
Kwa hiyo samsung anapelekewa alicho design apple ili azalishe vifaa. Apple anafanya hivyo siyo tu kwa processor almost kwa vifaa vyake vyote vinazalishwa sehemu mbali mbali na vinaenda unganishwa china kuwa simu japo kuna kiwanda kajenga Marekani kwa kazi hiyo tayari.
So designing na technology anafanya mwenyewe uzalishaji ana outsource kwenye makampuni mengine.
 
Ni kweli kabisa that is why vioo vipya vya oled vya iPhone 8 rumors Samsung ndio watavitengeneza.
 
kweli mkuu.
 
Hii ni kawaida kwa kila kampuni.
 
kwa memory mkuu samsung ni best, ni almost monopoly sababu mpinzani wake wa karibu Toshiba sasa hivi ana matatizo mengi sana hivyo tegemea vifaa vyote vinavyohusiana na memory vitengenezwe na Samsung.
 
kwa memory mkuu samsung ni best, ni almost monopoly sababu mpinzani wake wa karibu Toshiba sasa hivi ana matatizo mengi sana hivyo tegemea vifaa vyote vinavyohusiana na memory vitengenezwe na Samsung.
Yah mkuu niliona nhk world news toshba kala hasara kunwa sana
 

mkuu kuna kitu kinaitwa yield rate na manufacturing process,

kila kampuni inapoingia manufacturing process mpya lazma yield rate nayo ibadilike.

yield rate ni kile kiasi kizima kinachobaki, mfano cpu 100 zimetengenezwa then 60 ndio nzima na 40 zimeharibika inamaana yield rate hapo ni 60%

mfano mzuri muangalie intel, generation ya tatu sasa hivi amenasa kwenye 14nm kuanzia broadwell, skylake, kabylake na tetesi cofee lake inayokuja pia itakuwa 14nm, hii ni sababu yield rate yake ya 10nm ni ndogo sanaaa.

Apple aliwapa TSMC na Samsung kwa pamoja sababu kipindi kile yield rate ni ndogo sana ndo 16nm na 14nm zilikuwa zinaingia hivyo ni almost impossible kwa mmoja kutengeneza order zote.

hata mwaka huu mwanzoni kama utakumbuka snapdragon 835 inayotumia 10nm ilikuwa na uhaba sana, samsung alichukua order zote na kina LG na LG G6 ikabidi watumie cpu za mwaka jana za 14nm. mpaka kwenye mwezi wa 6 ndio simu kama oneplus one, Nokia 8, mi 6 etc zikaanza kutoka na sd835.

hivyo hapa itategemea na yield rate ikiwa kubwa baso ujue atapewa tenda mmoja tu ikiwa ndogo wanapewa wote.
 
Mbaya zaidi huwa kuna mashabiki michuzi wa apple hawaelewi chochote humu,ni wabishi balaa.
kwa memory mkuu samsung ni best, ni almost monopoly sababu mpinzani wake wa karibu Toshiba sasa hivi ana matatizo mengi sana hivyo tegemea vifaa vyote vinavyohusiana na memory vitengenezwe na Samsung
Designing, R&D na Software/hardware development ndiyo inaipa Apple edge ( na vitu vingine kama Marketing).
Inaleta picha isiyo ya kweli mkisema Samsung anaongoza kwenye memory. Kivipi? Designing au manufacturing?
 
Designing, R&D na Software/hardware development ndiyo inaipa Apple edge ( na vitu vingine kama Marketing).
Inaleta picha isiyo ya kweli mkisema Samsung anaongoza kwenye memory. Kivipi? Designing au manufacturing?
vyote designing na manufacturing, Apple hafanyi design ya memory na pia Apple usimuhesabu kwenye R&D huwa anatumia tu "visenti" huko. Apple kama kampuni kubwa ya consumer electronics alitakiwa aspend mabilioni ya hela kwa mwaka.
 
vyote designing na manufacturing, Apple hafanyi design ya memory na pia Apple usimuhesabu kwenye R&D huwa anatumia tu "visenti" huko. Apple kama kampuni kubwa ya consumer electronics alitakiwa aspend mabilioni ya hela kwa mwaka.
Nani ame - design Ax series of SoCs au nani ame-design zephyr na Hurricane core architecture? halafu mwaka jana Apple katumia 10.3bn$ na samsung katumia 13bn$, hivyo siyo vijisenti ila tu ni kwamba apple gets more bucks for its R&D.
The issue here is not, spending but innovation (not counting washing machines and things like blenders and cookers).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…