ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
26/03/2013
"Una wazo la kiteknolojia? Unataka kutengeza utajiri ukiwa ungali mdogo? We fanya tu" hayo ni maneno ya bwana mdogo Nick D'Aloisio mwenye umri wa miaka 17 ambayo aliyoyasema katika mahojiano na shirika la habari la Reuters, dogo huyu ambaye ameuza hisa ya app yakeya habari iliyoko kwenye iPhone inayojulikana kama Summly kwa jumla ya $30,0000,000. Fedha hizi ni sawa na Bilioni 49 za Kitanzania.
Summly hivi karibuni ni moja kati ya app zilizotarajiwa kunufaika kwa kupata wasomaji zaidi kufuatia huduma ya Google Reader kutangazwa kusitishwa na Google ifikapo mwezi wa saba. Wanunuzi wa app hiyo ni moja kati ya kampuni vigogo katika ulimwengu wa teknolojia yaani Yahoo. Nick anayeishi katika jiji la London hakuruhusiwa kuingia mkataba mwenyewe na hivyo mwanasheria wake pamoja na wazazi walimualikisha katika "dili" hiyo, Nick D'Aloisio pia ameajiriwa na kampuni ya Yahoo wakati bado anaendelea na masomo shuleni.
Chanzo cha Nick kuwa na wazo la kutengeza app lilikuja alipokuwa anakabiliwa na mtihani wa historia, ambapo utaratibu wa Google kutafuta jambo moja na hivyo kupata matokea mbali mbali kutoka website tofauti kulimfanya dogo huyu kutofurahishwa na jambo hili, hivyo wazo likamjia kwa nini asitengeneza app itakayojumuisha au kuweka pamoja chochote unachokitafuta kwenye mtandao. Huu ndio ukawa mwanzo wa Nick kuanza kujifunza kutengeneza app.
Kwa mujibu wa Reuters hii ni app ya pili ambayo Nick ameitengeneza, ya kwanza ilikuwa ni Trimit ambapo mwaka jana ilinunuliwa na bilionea wa Hong Kong Li Ka Shing kwa £250,000 sawa na Shilingi milioni 404. App ya Summly ilianza kutumiaka kwenye iOS miezi minne tu iliyopita na kuchaguliwa kuwa moja kati ya app kivutio kwa namna inavyofanya kazi. Matarajiri na kampuni za habari kadhaa zilivutiwa na app hiyo akiwemo mwanahabari bilionea Ruppert Murdoch na mcheza sinema wa Hollywood Ashton Kutcher.
Nick atakuwa ni muajiriwa mdogo kuliko wote wa Yahoo, msemaji wa Yahoo ambaye ni makamu wa Rais wa Mobile na Bidhaa zinazochipukia amesema Nick atabaki London na ataendelea na masomo yake King's College ingawa ameshaajiriwa na Yahoo, ajira hiyo ni sehemu ya "dili" kati ya Yahoo na Nick D'Aloisio wakati wa mauzi ya Summly. Kufuatia ununuzi wa app hiyo thamani ya hisa ya Yahoo imeongezeka kwa Senti 29 za Kimarekani na kufikia $23.45. Yahoo wamesema wataizima na ukitoa sokoni app hiyo lakini watatumia ufanyaji kazi wake kwenye app yao wenyewe. Mara baada ya Yahoo kutangaza habari hizi tulitinga kwenye iOS AppStore kuiangalia kama ingali ipo app hiyo, matokeo ni kwamba app hiyo imeshaondolewa tayari.
Chanzo: Gajetek Habari: App Yamtoa Dogo na Kuwa Milionea