donniebrasco
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 887
- 774
Hauwezi kuficha ukweli. Magaidi wote niliowai kusikia matukio yao ni waislamu. Lililotokea sio tukio la kigaidi, usichanganye mambo mkuu. Haikua sahihi kuleta imaginations za ugaidi kwenye hili swala.
Ni kweli si sawa kuhusianisha ugaidi kwenye hili suala lakini tuko kwenye wakati mbaya kwa mfano huyo mtuhumiwa asingejulikana/ kupatikana tungeweza kuwa tunaongea habari nyingine hapa, tena kwa kuwa tukio limetokea kanisani naamini kabisa ingekuwa habari mbaya sana,tumshukuru MWENYEZI mtuhumiwa amepatikana.
Sasa wewe usichanganye mambo kwanza kamsome CARLOS THE JACKAL ( ILICH RAMIREZ SANCHEZ) hako ni kamfano ili kakuweke sawa tu
Ukijua kabisa maana ya Ugaidi WAZUNGU( wengi wao sana hawakuwa waislamu) WAMEEUA sana katika historia yao kwa ajili ya masilahi yao na ndio MAGAIDI WAKUBWA KULIKO WOTE
Waafrika mamilioni kadhaa waliuliwa na wazungu wakati wa ukoloni
Mifano wabelgiji waliua watu zaidi ya milioni kumi ZAIRE, Waingereza waliua sana MAUMAU na kwenye makoloni yao mengine, Wajerumani pia Tanzania yaani mifano ni mingi sana, na sio Afrika tu wamefanya huo UGAIDI DUNIA NZIMA.
Yaani kwa nielewavyo hata UKOLONI NI UGAIDI TU.
Kutest mabomu ya nuklia kule Australia na kuua watu asili wa kule ni UGAIDI tu.
MAREKANI Wameuua watu wengi sana na kufanya dhuluma nyingi sana duniani huo NI UGAIDI MKUBWA NA NDIO WA MWANZO KWA KARNE HIZI kwa maana ukawasababisha baadhi ya watu waanze kuwashambulia kwa namna hii ambayo sasa ndo tunalazimishwa kuielewa kuwa ndo UGAIDI na ndio maana wewe umejikuta ukisema wote uliowasikia ni waislamu, maana wametaka dunia nzima watu wajue hivyo ili wao wapate pa kujificha,
hawa watu ni hatari sana wamezunguka dunia nzima kufanya dhuluma kwa mabavu yaani kwa UGAIDI ama kwa wizi wa kijanjajanja ili kuendeleza nchi zao tena kwa miaka mingi.
NA HATA WAZEE WETU WAKATI WA UKOLONI WALIPOKUWA WANAWAPINGA WALIITWA MAGAIDI, HUKU WAO WAKIJIONA SIO MAGAIDI KWETU...
Naamini umenielewa ndugu