Apigwa risasi nje ya Kanisa Ubungo

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Mkazi mmoja wa maeneo ya Ubungo Kibangu Jijini Dar mapema leo amepata ajali ya kupigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati akiwa anaingia Kanisani Parokia ya Kibangu.

Kwa bahati nzuri, risasi zilimlenga maeneo ya begani na ubavuni hivyo jamaa kwa mshtuko ama kupoteza damu nyingi kulimfanya azimie papo hapo.

Watu waliokuwa maeneo hayo baada ya kumwona mfyatua risasi ambaye hakuwa na usafiri wowote, walianza kumkimbiza na kumpigia kelele za mwizi hadi kumtia mikononi na hatimaye kumkabidhi kwa Polisi.

Hata hivyo inahisiwa kuwa huenda ni ugomvi wa kifamilia.

======
Mkazi wa Ubungo, Kibangu amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi wakati akitaka kuingia katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Kibangu, wilayani Ubungo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Akisimulia tukio hilo, mfanyakazi wa kanisa hilo, George Ng’atigwa amesema aliyejeruhiwa ni muumini wa kanisa hilo aliyemtaja kwa jina la Adrian Mpande.

Amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 asubuhi wakati muumini huyo alikuwa nje ya kanisa akisubiri muda ufike ili aingie kanisani.

“Mara akatokea mtu mwenye bastora akampiga risasi ubavuni na mkononi akaanguka na kuzimia,” amesema.

Amesema baada ya kutekeleza unyama huo, mtu huyo ambaye alifika kanisani hapo akitembea kwa miguu, alikimbia.

Amesema watu waliokaribu na kanisa hilo walimfukuza huku wakipiga mayowe na baada ya muda mfupi alikamatwa.

“Inaonekana alikamatwa baada ya bastora yake kuishiwa risasi kwa kuwa wakati anakimbia hakuwa akiwatishia waliokuwa wakimfukuza,”amesema.

Amesema baada ya kukamatwa,walifanya mawasiliano na Polisi ambao walifika baada ya muda mfupi na kuondoka naye.

Alisema alijeruhiwa kwa risasi alipata huduma ya kwanza katika zahanati iliyopo jirani na kanisa hilo na baadaye kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akifafanua, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kaganda alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba huo ni ugomvi wa kifamilia.

“Mtuhumiwa tunaye tunaendelea kumhoji na aliyepigwa risasi anaendelea vizuri na Matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Silaha, binafsi serikali itangaze zikabidhiwe makao makuu polisi ili tujue tatizo liko wapo!
 
Duh, kama wamemdaka Mungu mkubwa...maana inaonyesha kuwa sio 'mkali wa hizi kazi'

Hofu yangu ilikuwa usikute wale jamaa wa Rufiji/Kibiti wamejongea.
 
mwenye miwani ndio kaamtia mwenzie mkwaju...nilikuwa natoka makoka ndio nimi nikachukua picha kidogo

20229149_369943693421130_5407867311937929914_n.jpg
 
Back
Top Bottom