Apewa talaka kisa jina la kwenye kanga.

YNNAH

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,702
969
Dada mmoja alikuwa kwenye mishemishe zake,mara akaona kanga inaning'inia dukani ikamvutia na kwenda kuinunua. Bila kuisoma jina akampelekea mama mkwe wake,kisha akaondoka zake. Huku nyuma mama mkwe akaifungua ile kanga na kukuta imeandikwa "GUBU LA MAMA MKWE LIMENICHOSHA". Akampigia simu mwanae na kumueleza amwambie mkewe kwamba ujumbe wake nimeupata,mume akamuuliza mume umemwambia nini mama yangu?,mke akahamaki,akhuuu!! Sijamwambia kitu,kulikoni kwani? Mara akaingia mtu na ile kanga na kumwambia yule mume kwamba ujumbe wenyewe ni huu hapa. Palepale yule mume akampa talaka mkewe. Kadri mke alivyojieleza mume hakumuelewa. Je,hii ni halali?
 
hakuna mwanamke anae nunua khanga eti bila kusoma imeandikwa nini

huyo ni muongo na mnafiki....

alikusudia kumpa vijembe mama mkwe wake na imemrudia sasa
 
  • Thanks
Reactions: Taz
tabu ya kuwa na wakwe wanaojua kusoma.
Heri yetu, hajui hata 'a'
kwanza nikiongea kiswahili ananiona msomi.
 
Yanatokea sana tu. Namkumbuka dada mmoja aliyetwangwa nyekundu kwa kuvaa kanga yenye jina SIKUTAKI TENA, kumbe masikini ile kanga alipewa zawadi/alikuwa nayo, hata kabla ya kuolewa. Mume hakuuliza ilikuwaje, akatoa nyekundu moja kwa moja.
 
nana amini hao wanaume wanakuwa wamepata visingizio vya kuwaacha wake zao,kuna wanaume wengine,kitu kidogo tu talaka.
 
Utata mtupu. Upeleke zawadi bila kuifahamu qa undani? Ni utata Mtupu

Bazazi na Bazazi!
 
Dada mmoja alikuwa kwenye mishemishe zake,mara akaona kanga inaning'inia dukani ikamvutia na kwenda kuinunua. Bila kuisoma jina akampelekea mama mkwe wake,kisha akaondoka zake. Huku nyuma mama mkwe akaifungua ile kanga na kukuta imeandikwa "GUBU LA MAMA MKWE LIMENICHOSHA". Akampigia simu mwanae na kumueleza amwambie mkewe kwamba ujumbe wake nimeupata,mume akamuuliza mume umemwambia nini mama yangu?,mke akahamaki,akhuuu!! Sijamwambia kitu,kulikoni kwani? Mara akaingia mtu na ile kanga na kumwambia yule mume kwamba ujumbe wenyewe ni huu hapa. Palepale yule mume akampa talaka mkewe. Kadri mke alivyojieleza mume hakumuelewa. Je,hii ni halali?

sio halali hata kidogo! hata km ingekuwa huyo dada amefanyakusudi kwa mkwewe lakn haikumpasa mume kumpa talaka! huyo mume hakuwa anampenda kidhati mkewe,alikuwa anamtaftia sababu cku nyingi tu! wanaume wa hivyo ni hatari sana!
 
Back
Top Bottom