GE2025 Apaikunda aongoza kura za maoni udiwani kata ya Mawenzi

GE2025 Apaikunda aongoza kura za maoni udiwani kata ya Mawenzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,608

Diwani aliyemaliza muda wake wa Mawenzi, Jimbo la Moshi Mjini, Apaikunda Naburi ameongoza kura za maoni katika kata hiyo kwa kupata kura 58 kati ya 94 zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo, katika uchaguzi huo uliofanyika leo Jumatatu, Agosti 4, 2025, Katibu wa CCM Kata ya Mawenzi, Jolitha John amesema Apaikunda amepata kura 58 akifuatiwa na Said Mndeme (29) na Abdi Mohamed (6) huku kura moja ikiharibika.

Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Mujibu Abeid amesema pamoja na matokeo yaliyotangazwa na msimamizi hayo siyo uamuzi wa mwisho, uamuzi utatoka vikao vya juu.
 
Back
Top Bottom