Aolewe au aendelee kuwa single at 40?

Aolewe au aendelee kuwa single at 40?

Habari za mchana wakuu,

Kuna rafiki yangu ambaye hana bahati ya kupendwa na mtu wa dini yake. Wakati anasoma chuo alibahatika kupendana na kijana mmoja ambaye alikuwa tayari kufunga ndoa na huyo binti watakapo hitimu masomo na kupata kazi.

Vijana wale walimaliza masomo yao vizuri na kila mmoja alibahatika kupata kazi hapa Dar. Katika harakati za maandalizi ya kufunga ndoa yule kijana alienda kujitambulisha nyumbani kwa yule msichana lakini familiaya mwanamke alikataa na kuwa mtoto wao hawezi kuolewa na mwanaume wa dini tofauti. Kwa sababu hiyo yule ikabidi waachane kwa huzuni na majonzi makubwa.

Baada ya miaka kadhaa yule kijana alimpata wa dini yake wakafunga ndoa. Kimbembe kikawa kwa binti. Kila mwanaume anayetaka kumuoa anakuwani dini tofauti na yake. Sasa hivi ana umri wa miaka 40 hana mtoto, rafiki wa kiume wala mchumba. Amekuwa akijiuliza kwa nini imekuwa hivyo na kujilaumu kuzaliwa mwanamke sababu angekuwa mwanaume anaamini angekuwa na familia kwani wanaume wao wanatafutwa. Familia yake inamshauri atafute mwanaume ili azae naye apate hata mtoto. Anajiuliza kwa nini familia inakubali mimi niwe mzinifu lakini hawakubali mimi niwe na ndoa inayotambulika?

Hivi karibuni rafiki yake wa toka mwaka 2005 ambaye anaishi marekani amemuomba awe mchumba wake ''taking friendship to the next level'' lakini huyo dada amekataa sababu ya dini. Ameamua kubaki single sababu hana jinsi. Amekuwa mtu wa huzuni muda mwingi kwani ndoto zake za kuwa na familia kama zinayoyoma.

Jamani huyo dada yuko njia panda hajui la kufanya. Mimi nimemuambia afanye maamuzi magumu kama niliyofanya mimi. Kwani nililkuwa napata wachumba wa kikirsto mwanzo mwisho hatimaye nikakata shauri kuwa naolewa na wa dini tofauti. Familia ilinitenga mpaka baba yangu akasema hataki kuniona. Baada yamiaka kadhaa ya ndoa yetu eti sasa ananiona kama mimi ndio mtoto wake mwenye akili kwani nimekuwa msaada mkubwa kwa familia.

Haya mambo huwa nimagumu sana lakini mkisimama imara mnaweza kufanikiwa. Nina mifano mingi ambayo wazazi wanakuwa wagumu lakini baadae wanalainika.

Karibuni wanajamvi kwa ushauri, na wale ambao wamepitia haya mnaobwa kutoa uzoefu wenu hapa

Shukrani
Anayeoa haoi dini. Kama dini ikiwa kikwazo iache karibu kuwa RAIA WA SERIKALI TUKUFU YA UFALME WA MUNGU. Hapo hapana ugomvi, wote watakaokuwa wamekwazwa na maamuzi yako, watakuwa hadhira yako kwa kushuhudia mabadiliko, hadi mwishoni watakukubali na kukusifu.
 
Anayeoa haoi dini. Kama dini ikiwa kikwazo iache karibu kuwa RAIA WA SERIKALI TUKUFU YA UFALME WA MUNGU. Hapo hapana ugomvi, wote watakaokuwa wamekwazwa na maamuzi yako, watakuwa hadhira yako kwa kushuhudia mabadiliko, hadi mwishoni watakukubali na kukusifu.
Wakati mwingine wanaoukimbia wajibu, wana uwalakini. Akapimwe vipimo vya Daktari vyaweza kuumaliza mjadala kuwa huyo kuwa hivyo ndiyo nafuu yake.
 
Una ramli ya kujua penzi la kweli na la kinafiki?
Ahaa basi wape moyo....frankly speeking that is a totally blind love trust me hakunaga mapenzi ya kukutana uzeeni...The sparks of love always live in the youngest blood ...niliwahi soma vitabu vya wanasayansi flani wa wa genetics ...ngoja nirudi library nikipata citation ya kitabu nitakutumia usearch kwenye net watu wamefanya research
 
sio kweli kuwa anapata wa dini tofauti tu
itakuwa ameweka vigezo vinavyofikiwa na hao wa dini tofauti na hata wewe ulikuwa hivyo bila shaka

sasa kama yuko sirias kweli kwenye suala hilo mlete kwangu Mimi nimuoe fasta bila kuchelewa
 
Hii ni kuruhusu watu wengine wakufanyie maamuzi hata kama ni familia wakati mwisho wake everything kinakuwa mkononi mwako na mzigo wako wala sio familia tena. Mwambie aolewe, 40 yrs old is not too late she can still make a family and live her dreams.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom