Kuna kitu kimoja bado waandishi wengi hawajajua kuhusu uandishi wa vitabu, usiunguze calories nyingi kufikiria kuandika topic mpya kuhusu kitabu , boresha nakala ya awali uliyotoa. Kuna kitabu nilisoma chenye title "PUBLISHING FOR PROFIT-5TH EDITION", huyu mwandishi katoa nakala moja kwa kuboresha paka kafika 5th edition kwenye hiyo topic. Ukawa unatoa kama movies wanavyotoa especially kwa waandishi wa hadithi ni rahisi sana, kwa mfano kuna hadithi inaitwa "HADI LINI", au "KIZUNGUMKUTI" ni hadithi nzuri sana kama ingetolewa maboresha ya sasa kwasababu imesomwa na watu wengi sana na inge rahisi sana watu kufuatilia kwakuwa wanaijua ilipoishia. Waandishi mnakosa pesa ambazo ni nyingi na ni rahisi kuzipata, kazi hawaiwezi kukupa unachokitaka katika maisha zaidi ya kukufanya uwe mtumwa .
Chukua hii "PROFIT IS BETTER THAN WAGES", faida inabadilika, mshahara haubadiliki kila mwezi ni huo huo ata uwe na jitihada vipi unapokea mshahara ule ule ndani ya mwaka mzima. Unapokea na pesa ambayo ni CONSTANT ndani ya mwaka mzima. Ila ukiwa unatumia muda mwingi kuandika vitabu kwa TITLE NZURI unauwezakano ukapata pesa nyingi sana kwa mwezi na kwa mwaka pia.
Madharani umeandika hadithi inaitwa "BADO ANAISHI", imeifanyia maboresho mwaka mzima kwa kutoa nakala mpya kila mwezi, ni rahisi sana kupata wasomaji wengi kwasababu inakuwa kama series kwenye movie, wengi wataifuatilia kila mwezi na kukufanya utapate pesa nyingi kwa watu kununua. Anza kujifunza kutoa kazi moja kwa mwaka ila ina maboresho kila mwezi. Kila mwaka topic ya hadithi moja, ila maboresho kila mwezi, ukifanya hivyo utajitenga na waandishi wanaosubiri miujiza ya kuuza hadithi moja ambayo haina maboresha ndani ya miezi mitatu au sita, na anafikiria kutoa hadithi mpya mwandishi wa namna hii atakuwa anatumia nguvu nyingi sana kutunga hadithi mpya kuliko anaye boresha nakala ya awali.
Wasomaji wanapenda NEW IDEA kwenye hadithi zako kila mara unapotoa wasione mfanano wa nakala ya awali ata moja, vuta taswira kwenye series hakunaga marudio ni straight forward. Binafsi yangu nilikuwa nafuatialia movie moja inaitwa "QUEEN OF THE SOUTH" kiukweli niliipenda na kuangalia SEASONS 3 na kusubiria ya 4. Geuza idea ya kwenye series weka kwenye uandishi wa vitabu, utapata AUDIENCE wengi kukufuatilia na uwe unatoa kwa wakati ili upate AUDIENCE wengi kukufuatilia kumbuka AUDIENCE wanaambiana wakiona kitabu kizuri somewhere.
Kingine ukiwa kama mwandishi fikiria kutoa AUDIOBOOK pia ili ukamate soko nzima la wapenda hadithi kwa ujumla, kila msomaji anapenda media yake , mngine anapenda kusikiliza, mngine anapenda kusoma. Ukiwa kama mwandishi unayetaka kufika mbali na kufanikiwa kwenye fani yako inakubidi uwe wa kwanza kufanya hivyo ili kuwapa AUDIENCE options ya kuchagua wapendacho.
Kuwa wa kwanza kufanya fani ya uandishi kwa namna ya tofauti na waandishi wengine, kwa lugha nyepesi kuwa wa kwanza sokoni, AUDIENCE wanapenda NEW IDEA. Kuna msemo unasema "NI BORA KUWA WA KWANZA KULIKO KUWA BORA", faida ya kuwa wa kwanza ni rahisi AUDIENCE kukumbuka kirahisi na kushika fikra zako("NI BORA UWE WA KWANZA KWENYE FIKRA ZA AUDIENCE KULKO KUWA BORA SOKONI"). Unaweza ukawa bora sokoni ila haupo kwenye fikra za watu wengi, chukualia mfano wa LG kwenye upande SMARTPHONE, ni bora kwa upande wao ila kwa upande wa wateja hapana, wateja wengi wanapenda SAMSUNG/iPHONE. Kama mimi binafsi yangu kwenye upande wa computer napenda sana DELL, uwezi niambia computer nyingine ambao utanishawishi kununua zaida ya DELL.
Kwaiyo kwenye swala la marketing ni bora uwe wa kwanza kwenye firka za watu wengi kuliko kuwa bora sokoni. Ukiwa kama mwandishi fanya juu chini uwe wa kwanza kwenye fikra za watu kwa kuwa wa kwanza sokoni mwandishi anayeuza vitabu vyake kwa softcopy na audiobook kwa reasonable price. APPLE kipindi wanataka kutoa iPod waliweka mazingira ya iTune, siku wana launch iPod, waka launch pamoja na iTune, APPLE wakatengeneza mabillion ya dollar na kufanya makampuni mengine yafe, kwasababu wamekuwa wakwanza kufanya kitu cha tofauti na wengine.
Kingine kuhusu APPLE ni wame value wateja wao kwa kuwatofautisha na makampuni mengine, mfano mtu ukimwona ana iPHONE, MACBOOK PRO unajua kabisa anapesa au ana maisha mazuri kwasababu kila mtu anajua bei ya bidhaa ya APPLE sokoni, icho kitu kimefanya kampuni ya APPLE kuwa juu zaidi kwa kila bidhaa wanayotoa kwajili wameshawaamisha wateja wao kwamba kila bidhaa yao ni bora, kwaiyo hawana kazi tena ya kuambia wateja nunua blah blah ni nzuri, wala hakunaga promotion kuhusu APPLE products.
Unaweza ukajiuliza kwamba "AUDIENCE WAKO, UNATAKA WATU WENGINE WASEME NINI KUHUSU WAO KUSOMA VITABU VYAKO?"~ Hii mbinu inafaa sana kwa mwandishi anaye andika vitabu vya biashara/ujasiriamali/afya. Ukiweza kuwa value audience wako waonekanaje wakisoma vitabu vyako, utajiweka sehemu nzuir sana kwenye mauzo ya vitabu vyako na kupata mafanikio makubwa na kubadilisha maisha yako kwa ujumla.
"SUCCESS IS MINDSET GAME"
Fikiria AUDIENCE wako muda mwingi, fikria namna ambavyo utaweza kubadilisha fikra zao kwa vitabu vyako especially vya biashara na afya. Fikiria sana kuhusu hilo , litakusaidia kuandika maudhui ambao yatawasaidia kutoka mahali walipo kwa kusoma vitabu vyako, fikiria ambavyo utasaidia watu wengi kwa wao kusoma vitabu vyako. Kuna msemo unasema "ukitaka kufanikiwa katika maisha , saidia watu wengi kutimiza malengo yao". Tumia uandishi kubadilisha maisha ya wengi na kutumiza malengo yao, ukifanya hivyo utapendwa na wengi, utakuwa wa kwanza kwenye fikra zao na kuwafanya wanunua kazi zako kwa wingi kwasababu umeandika kitu ambacho kimewasaidia maisha yao kwa kiasi kikubwa.
Watu wananua SOLUTIONS hawanunua bidhaa wala huduma, uza solutions miongozi mwa watu wengi; fikiria maisha ya sasa unawezaje kutumia uandishi wako kusaidia watu wengi kumitiza malengo yao kwa kuwauzia vitabu vyako.
Watu wanateseka kwenye biashara, hawajui wapi watapata solutions, watu wanateseka na magonjwa hawajui wapi watapata tiba sahihi kwa kutumia mitishamba; kama hiyo sector unaiweza WHY NOT usiandike kiwafikie wengi zaidi na kusidia watu biashara zao au afya zao. Fursa ni nyingi sana ukiwa na smartphone na ukiwa mwandishi wa vitabu.
Pia watu wanateseka kwenye ndoa / mahusiano wewe ni mtaalamu WHY NOT usiandike kitabu na kuuza kwa njia ya mtandao kiwafikiwe wengi zaidi kwa mara moja. Kuna kitabu nilisoma cha mambo ya AFYA, kinaitwa "HOW NOT TO DIE", nilijifunza vitu vingii sana kuhusu afya, nilijua kwanini RED MEAT haifai, na kwanini mtu ule matunda mengi kama umegoma kuacha kula nyama. Nilikunywa dawa kama zote msemo wa watu dar za UTI lakini wapi, nilivyosoma hicho kitabu nilipona kizembe UTI kwa gahrama ndogo sana na sio dawa za hospital, bali ni matunda.
Final word: "KUWA MTU WA KUJARIBU VITU VIPYA KUHUSU FANI YAKO, JIFUNZE KUBORESHA NAMBA UNAVYOFANYA KAZI ZAKO KUHUSU FANI YAKO". Kuna msemo unasema "Mafanikio yapo kwenye kitu unachofanya kila siku, utafanikiwa kama unabadilisha namna ya kufanya".
Be Optimistic, Be first
"Kama unataka kufanikiwa haraka, ongeza speed ya kufeli"~ CEO OF IBM