Antony Mtaka aambiwe kwamba sera ya elimu ni ya kitaifa na siyo mkoa kwa mkoa

Ofisi hii ipo chini ya OR TAMISEMI , tambua hilo kwanza.
Msjukumu ya TAMISEMI yapo clear ,, mojawapo ni kuratibu , kusimamia na kutekeleza shughuli za hizi shule.

Mkuu wa mkoa anayeongelewa hapa ni Ofisi yake
Umesema mwenyewe "URATIBU" Kinachoongoza nchi ni institutions siyo individuals na institutions ni sera ambayo haiwezi kuwa implemented bila laws...Sasa niambie kama kuna sheria ya mkoa...
 
Bila hata kujua kiwango cha elimu ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, mara moja naona makosa ya kiutendaji aliyonayo. Kwanza, yaonekana ni mtu asiyejua kuchagua maneno. Pili, hakujua mchakato upi uboreshe kiwango cha elimu mkoani kwake, siyo ufaulu anaotafuta. Elimu inaendeshwa kitaifa na siyo ki-mkoa.

Haiingii akilini kwamba mkuu wa mkoa anataka kuboresha ufaulu wa wanafunzi kwa kupambana na waziri wa elimu, kwa makambi ya elimu. Ili iweje?

Elimu ni mchakato wa miaka 7 kwa shule za msingi, miaka 4 sekondari, n.k. Kama kuna uzembe ktk miaka ya elimu, Mtaka anawezaje kuboresha uzembe huo kwa makambi ya miezi miwili? Yaani sasa hivi aanze, kufika septemba darasa la 7 wafaulu mtihani. Ni elimu gani hiyo?

Sera ya elimu ipo ili kudhibiti mawazo mfu kama haya ya akina Mtaka.
Too primitive kbsa his police background has blurred his entire brain
 
Naona umefafanua mamlaka ya tawala za kimkoa tu haujaeleza kuhusu sera. UKIELEWA maana ya national curriculum itakusaidia sana kujua jinsi RC alivyoropoka kimakosa.
Kwa kifupi RCs wanatakiwa kutekeleza sera za wizara,juhudi za mkoa sio kuharibu ratiba ya wizara kisera,eg.km sera na taratibu ni kukaa darasani masaa 8, juhudi ya mkoa ni kufanikisha mtoto anakaa hayo masaa sio kumuongezea masaa ni kuharibu taratibu zilizowekwa na wizara.
Excellent
 
Ofcourse kuna vitu tunavifanya kwa mazoea ila tungekuwa strict na tungekamilisha ugatushaji mambo yangekuwa wazi tu na marahisi...
 
Naona umefafanua mamlaka ya tawala za kimkoa tu haujaeleza kuhusu sera. UKIELEWA maana ya national curriculum itakusaidia sana kujua jinsi RC alivyoropoka kimakosa.
Kwa kifupi RCs wanatakiwa kutekeleza sera za wizara,juhudi za mkoa sio kuharibu ratiba ya wizara kisera,eg.km sera na taratibu ni kukaa darasani masaa 8, juhudi ya mkoa ni kufanikisha mtoto anakaa hayo masaa sio kumuongezea masaa ni kuharibu taratibu zilizowekwa na wizara.
Na wala hawatekelezi sera yeyote ile wanatakiwa kuwa facilitators wa watekelezaji wa sheria ya local governments i.e by-laws which is operational level...Mkuu wa Mkoa hasimami budget na budget ndizo zina implement maendeleo yanayotokana na mipango iliyozaliwa na sera, kanuni na miongozo mbalimbali...
 
Umesema mwenyewe "URATIBU" Kinachoongoza nchi ni institutions siyo individuals na institutions ni sera ambayo haiwezi kuwa implemented bila laws...Sasa niambie kama kuna sheria ya mkoa...

Funny qns

SSH ni Rais wa Nchi

Je kuna sheria ya nchi

Wakuu wa mikoa wana Sheria yao , wapo kisheria ujue.

Pia wako guided na sheria za TAWALA ZA MIKOA
 
Funny qns

SSH ni Rais wa Nchi

Je kuna sheria ya nchi
Huijui sheria ya nchi wewe? Ni KATIBA

Na katiba inampa Mh. Rais at her pleasure kuanzisha au kufuta taasisi yeyote ile...Kaisome katiba...Sera zote za nchi zinaitwa constitutional laws...Mawaziri ndiyo wasimamizi wa hizo...

Sheria siifahamu vizuri ila inapokuwa kwenye institutions tutakesha hapa...Japo na zenyewe huwa ni complex zinaitwa tower of Babel na ndiyo maana haishangazi sisi tulioletewa haya na IMF/WB kuna mambo hayaendani na culture yetu ndiyo maana unaona hata Mkuu wa Mkoa anakuja ku realize kuna mambo anatakiwa atumie common sense tu, kumbe tukizingatia utawala wa sheria tunakosea kwakua nchi haiongozwi na common sense inaongozwa na sheria ili sote tuwe one page
 
Just ask yourself msimamizi wa hiyo sheria ya TAWALA ZA MIKOA ni mkuu wa Mkoa?
 
Umesema mwenyewe "URATIBU" Kinachoongoza nchi ni institutions siyo individuals na institutions ni sera ambayo haiwezi kuwa implemented bila laws...Sasa niambie kama kuna sheria ya mkoa...

Funny qns

SSH ni Rais wa Nchi

Je kuna sheria ya nchi
Huijui sheria ya nchi wewe? Ni KATIBA

Na katiba inampa Mh. Rais at her pleasure kuanzisha au kufuta taasisi yeyote ile...Kaisome katiba...Sera zote za nchi zinaitwa constitutional laws...Mawaziri ndiyo wasimamizi wa hizo...

Sheria siifahamu vizuri ila inapokuwa kwenye institutions tutakesha hapa...Japo na zenyewe huwa ni complex zinaitwa tower of Babel na ndiyo maana haishangazi sisi tulioletewa haya na IMF/WB kuna mambo hayaendani na culture yetu ndiyo maana unaona hata Mkuu wa Mkoa anakuja ku realize kuna mambo anatakiwa atumie common sense tu, kumbe tukizingatia utawala wa sheria tunakosea kwakua nchi haiongozwi na common sense inaongozwa na sheria ili sote tuwe one page

MKUU KWA HIYO HUJUI KUWA NAFASI YA MKUU WA MKOA IPO KISHERIA?
 
National Curriculum inatambua shughuli za ziada nje ya muda wa masomo. Curriculum haijapanga muda wa kutoka
Ni kweli national curriculum inatambua shughuli za nje ya darasa eg. michezo,kazi n.k. lakini suala la muda pia lipo,na vipindi vyote vya darasani vina muda maalum uliamuliwa na wanataaluma,ata non curriculum activities zote zina muda.
Taaluma na muda ni kama samaki na maji.
 
HAIJAPANGA MUDA WA KUINGIA NA KUTOKA KUU. NIMEISOMA
 
Funny qns

SSH ni Rais wa Nchi

Je kuna sheria ya nchi

MKUU KWA HIYO HUJUI KUWA NAFASI YA MKUU WA MKOA IPO KISHERIA?
Kila nafasi ipo ki sheria...Sijasema hayo...Hapa tunatafuta kueleweshana maana kuna mambo tunachanganya...Sasa nikuulize Mkuu wa Mkoa akiweka hizo kambi atazi run kwa budget ipi? Accountability itakuaje hapo? Maana haipo kwenye ile flow of budget zilizopitishwa na bunge wala na council kwakua yeye haingii kokote kati ya hizo...unaona sasa hapo? Anapata lift ya wazazi kwakua ni to their interest, sasa hapo hapo fikiria ajija na lingine ambalo halipo ndani ya interest ya raia hali inakuaje? Atawawajibisha kwa sheria, kanuni au mwongozo upi? Umeona sasa shida ilipo?
 
Umesema mwenyewe "URATIBU" Kinachoongoza nchi ni institutions siyo individuals na institutions ni sera ambayo haiwezi kuwa implemented bila laws...Sasa niambie kama kuna sheria ya mkoa...

Wakuu wa Mikoa Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
61.-
(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katika Jamhuri ya Muungano ambaye, bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3), atakuwa ni kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Bara watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

(3) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar baada ya kushauriana na Rais.

(4) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

(5) Pamoja na wajibu na madaraka yake yaliyotajwa kwenye masharti yaliyotangulia ya ibara hii, Mkuu wa Mkoa kwa mkoa wowote katika Tanzania Zanzibar atatekeleza kazi za shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atakazokabidhiwa na Rais wa Zanzibar, na kwa mujibu wa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar 1984 au sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
 
Kila nafasi ipo ki sheria...Sijasema hayo...Hapa tunatafuta kueleweshana maana kuna mambo tunachanganya...Sasa nikuulize Mkuu wa Mkoa akiweka hizo kambi atazi run kwa budget ipi? Accountability itakuaje hapo? Maana haipo kwenye ile flow of budget zilizopitishwa na bunge wala na council kwakua yeye haingii kokote kati ya hizo...unaona sasa hapo? Anapata lift ya wazazi kwakua ni to their interest, sasa hapo hapo fikiria ajija na lingine ambalo halipo ndani ya interest ya raia hali inakuaje? Atawawajibisha kwa sheria, kanuni au mwongozo upi? Umeona sasa shida ilipo?

TAMISEMI ina haya mafungu mkuu. Nkuomba usiitenganishe ofisi ya mkuu wa Mkoa na Tamisemi.
 
Wakuu wa Mikoa Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
61.-
(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katika Jamhuri ya Muungano ambaye, bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3), atakuwa ni kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Bara watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

(3) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar baada ya kushauriana na Rais.

(4) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

(5) Pamoja na wajibu na madaraka yake yaliyotajwa kwenye masharti yaliyotangulia ya ibara hii, Mkuu wa Mkoa kwa mkoa wowote katika Tanzania Zanzibar atatekeleza kazi za shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atakazokabidhiwa na Rais wa Zanzibar, na kwa mujibu wa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar 1984 au sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
ATASIMAMIA hii iwekee bold....Kwahiyo kuratibu utekelezaji ndiyo usimamizi wenyewe lakini usimamizibwake unatokana na shria kanuni na taratibu ambazo atazipata kupitia vyombo vilivyowekwa kisheria kufanya maamuzi na wala yeye si mwamuzi
 
TAMISEMI ina haya mafungu mkuu. Nkuomba usiitenganishe ofisi ya mkuu wa Mkoa na Tamisemi.
Nimeshakuelewesha kwa kadri ya uelewa wangu...Kuwa tu na uhakika serikali ya mtaa/ ni serikali kamili...Na hauina serikali za mikoa...Hii iliisha enzi za Mwinyi kama sikosei Mzee Mkapa alijenga taasisi ambapo ndipo tulianza ugatushaji na kuandika sera tofauti na ordinances pamoja na maazimio na matamko yaliyotuongoza huko kabla...Bado watu wengine wanaishi kwa mawazo hayo ya kikoloni
 
ATASIMAMIA hii iwekee bold....Kwahiyo kuratibu utekelezaji ndiyo usimamizi wenyewe lakini usimamizibwake unatokana na shria kanuni na taratibu ambazo atazipata kupitia vyombo vilivyowekwa kisheria kufanya maamuzi na wala yeye si mwamuzi
Sasa Mtaka kama RC ameamua nini, alichokifanya kipo ndani ya Sera ya elimu na mtaala wa elimu. Hajajitungia mbona mkuu
 
Huku anataka alime Alizeti kagundua haliwezekani kahamia Zabibu, bado Wagogo anataka awaweke kambini. Sifa alizopewa na Media sasa katoka kule Bariadi anajiona na yeye anaweza kumkemea Waziri
 
Sasa Mtaka kama RC ameamua nini, alichokifanya kipo ndani ya Sera ya elimu na mtaala wa elimu. Hajajitungia mbona mkuu
Kwahiyo anasimamia makambi yaliyoanzishwa siyo? Hope we want to clear doubts ili tusaidiane kwenye utawala wa kisheria...Na ujue hata mimi naona point yake ina mashiko tatizo haina legal backings siyo legitimate....
 
Ofisi hii ipo chini ya OR TAMISEMI , tambua hilo kwanza.
Msjukumu ya TAMISEMI yapo clear ,, mojawapo ni kuratibu , kusimamia na kutekeleza shughuli za hizi shule.

Mkuu wa mkoa anayeongelewa hapa ni Ofisi yake
Mkuu acha ubishi usio na maana Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kimuundo ipo Chini ya Serikali Kuu sio TAMISEMI hilo weka akilini mwako.Jukumu kubwa LA Ofisi hiyo ni kuwa kiungo kati ya Serikaliki Kuu na Serikali za Mitaa kwa level ya Mkoa.

Na Wizara ya TAMISEMI kimuundo ipo Serikali Kuu ingawa amepewa Jukumu la kusimamia Serikali za Mitaa,hii maana yake ni kuwa chochote kinachohusu Sekta zilizo chini ya Halmashauri maamuzi ya mwisho yanatoka kwenye Wizara husika,hivyo basi TAMISEMI naye ni coordinator kati ya Wizara mama na Halmashauri za Wilaya/Jiji/Manispaa kwa level ya Kitaifa.

Pia Kumbuka tunapozungumzia Serikali ni Rais na Baraza lake la Mawaziri,sasa huyo Mtaka wako kama huwa anaingia kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri na anakuwa Mwenyekti wa Kikao hicho basi ana Haki kabisa ya kubishana na Waziri mwenyewe dhamana.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom