Antony Komu na Said Kubenea waivua nguo CHADEMA

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
Wabunge wanamageuzi wa siku nyingi nchini wamegoma kuhama CHADEMA sasa wameamua kushughulika na Mbowe na vijana wake. Nasikia harufu ya Damu ndani ya CHADEMA

Sikiliza sauti ya Mbunge Komu na Kubenea wakijadili.

Wapenda mabadiliko wote wanapaswa kuwaunga mkono wabunge hawa. Wasiojielewa wataaminishwa kuwa hawa ni mamluki

 
Wabunge wanamageuzi wa siku nyingi nchini wamegoma kuhama CHADEMA sasa wameamua kushughulika na Mbowe na vijana wake. Nasikia harufu ya Damu ndani ya CHADEMA

Sikiliza sauti ya Mbunge Komu na Kubenea wakijadili.

Wapenda mabadiliko wote wanapaswa kuwaunga mkono wabunge hawa. Nyumbu wataaminishwa kuwa hawa ni mamlukiView attachment 897662
Umesahau kuweka namba ya simu mkuu.
 
kinachoendelea ndani ya chadema kinasikitisha sana. Mbowe alitakiwa awe ameshajiuzulu siku nyingi ili upinzani upone.
Mbona wote wanaojiuzulu wanatoa sababu tofauti hawasemi kuwa Mbowe ndiye tatizo. Fuatilia maelezo yao hakuna anayesema anahama kwadababu ya Mbowe
 
HAMA-HAMA ISIWAFEDHEHESHE, TUJADILI HILI LA KUBENEA NA KOMU; sio JINAI pekee huu ni UASI dhidi ya taasisi; Kupanga njama za kumdhuru Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob. Tena wanakwenda mbali na kupanga namna ya kumshughulikia mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kuomba hata TAKUKURU wamfikie!

Hayo ni maneno kati ya mbunge wa Ubungo Saed Kubenea na mbunge wa Moshi Vijijini Anthony KOMU wakijadili namna sahihi ya kumaliza nguvu za Freeman Mbowe kwa kuteka na kujeruhi au kuwaua kabisa watu wa karibu yake, akitajwa meya wa manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob kwa sababu ni sehemu ya hao watu wa karibu!

Nilipoanza kupoteza imani yangu na Saed Kubenea! January 2, 2017 binafsi ndio ilikuwa mwisho wa kusoma magazeti yanayotokana na Kampuni yoyote ya Saed Kubenea. Nilipoteza imani yangu kwake baada ya kusaidia kupotea na kutokomea kwa Ben Saanane. Kubenea ametupotezea Saanane wetu kwa sababu ya chuki zake vs BEN.

Alileta kupitia gazeti la Mwanahalisi taarifa za UDAKU, umbea na uzandiki, habari za uchochoroni, bils kuwa na ushahidi wa kimantiki. Yote ilitokana na chuki yake kwa Saanane. Kubenea akasema kwenye habari hiyo kwamba waliokota karatasi iliyorushwa mlangoni katika ofisi yao (chanzo cha habari) na kuamua kutumia karatasi hiyo kuandika habari yenye kuonesha BEN kaonekana kijiweni.

Huyu Kubenea alikuwa na mtafaruku na BEN, hadi kufikia kumfungia Saanane kutotumia mtandao wa Mwanahalisi online, akaondoa akaunti ya BEN katika Server ya mtandao huo. Hapo Mwanahalisi wametumia siku saba kuandaa wasomaji (ukizingatia ndio wakati tunapiga kelele za Ben Saanane) ndio baadae wakaamua kuleta hiyo habari kwa data za kuokota mlangoni. "Ben aonekana akirandaranda mtaani"

Kwanini tusiamini kwamba anahusika kwa namna yoyote kutekwa kwa BEN? kama hana uhusiano, basi alishiriki kuendelea kumpoteza BEN baada ya hiyo habari yake kuchapishwa. Kwa sababu, wakati tukiwa katika taharuki ya wapi alipo BEN, Kubenea akajitokeza na gazeti lake na kuandika ambayo aliandika, upepo wa CCM ukahamia "Kubenea amesema Saanane yupo"

Njama za Kubenea na KOMU dhidi ya Mbowe na Meya Boniface Jacob! Hii yote ni sababu mbili kubwa, ndio msingi wa kuanza kujenga hizi mbinu za mauaji, kuteka na mashtaka! 1. Ubunge Jimbo la Ubungo 2020; 2. Uenyekiti wa CHADEMA 2019; HIZI ndio sababu za msingi za kwanini Kubenea ni butter sana kwa Freeman na yoyote anaemtetea!

KUBENEA nafahamu, anaamini Bonny ni 'threat' Ubungo come 2020, Anaamini Ubungo kwake ni ngumu, hivyo Bonny kwake ni tatizo (ndani ya chama). And yoyote ambaye ni rafiki wa Bonny kwake ni adui mkubwa. Si-Shangai hizi 'allegations' za kupotezwa. NA; Kuhusu uenyekiti wa CHADEMA, Kubenea ni kati ya watu wasiompenda na kuhitaji uwepo wa Mbowe. Ni mtu ambaye anahitaji yeye au mwingine kurios kwenye sideline yake kuwa mwenyekiti wa CHADEMA.

Ukisikiliza maongezi ya Kubenea katika clip hiyo ni wazi kuna msukumo mkubwa na nguvu kutoka lernte dola. Ni mtu ambaye anataka kupambana na Freeman kwa gharama yoyote. Ukisikiliza vyema, Kubenea anamsilkiliza KOMU wakati akipewa mkakati wa kumuangamiza Mbowe, ni kumharibia watu wake wa karibu wenye kuaminika. Anaetajwa hapo ni Boniface Jacob.

Wanakwenda mbele na kusema "Magufuli ni dhaifu kwa sababu ameshindwa kumshughulikia Mbowe kwa akili" wanatoa ushauri Mbowe ashughulikiwe na TAKUKURU, kupitia vitabu vya CAG. katika Sauti hizo za Kubenea na KOMU wanasema Mbowe ni rahisi kupambana nae kama tu utaweza kumfikia, unamfikia kwa kuangamiza watu wake wa karibu. Wakamatwe, wafungwe, au wauwawe, anatajwa Meya Bonny hapo.

Kwanini Kubenea anamchukia Mbowe?

Uamuzi wa Baraza Kuu wa kuwaondoa wabunge na madiwani kutoka makao makuu, wasipewe ukurugenzi, wakafanye kazi kwenye majimbo na kata (Lissu na Mbowe excluded) hapo ndio mtufuano ulianza. Kati ya ambao waliondolewa katika ukurugenzi wa makao makuu ni KOMU, Lwakatare na Waitara. Hapa Kubenea akaamua kuungana na kundi hili kulalamika, wakisema Mbowe kawaondoa makao makuu kimkakati.

Maslahi ya Kubenea ni yapi ndani ya CHADEMA?

KUBENEA nu mbunge wa Ubungo. Lakini pia ni Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers. Yeye (Kubenea) na KOMU wote ni wakurugenzi wa kampuni hiyo. Ni watu ambao wameoa sehemu moja (nyumba moja) Kwa mtazamo huo, ni wazi watu hawa wanayo maslahi ya pamoja ambayo yanawakutanisha. Wakihitaji kuwa na nguvu ndani ya CHADEMA na ushawishi makao makuu kwa maslahi ya kisiasa au binafsi au mengine ambayo yapo nje ya uwezo wangu.

Wakati huo wa marekebisho ya muundo wa utawala makao makuu, ndio wakati Esther Daffi (mzazi mwenzake na Kubenea) alipoondolewa makao makuu, nyuma yake (2015) amekosa uteuzi wa viti maalum. Nafasi akachukua Jesca Kishoa. Shughuli ikaanzia hapa. Kubenea na wengine ambao ni waathirika wa mabadiliko ya muundo wa utawala makao makuu wakatengeneza kikundi cha kumuondoa Mbowe madarakani. Kikundi hiki kinajulikana. Na dhamira yao inaongonzwa na Kubenea akisema "Mbowe amechoka, aondoke waje watu wengine"

Hapa sasa ndio mwanzo kuanza kuzaliwa makundi mengi ya vijana kwenye mitandao kijamii. Makundi yenye kumuunga mkono Kubenea. Moja kati ya kundi hilo ni "FRIENDS OF BAVICHA ORIGINAL" kundi ambalo nimekula 'kifungo cha maisha' kutorejeshwa humo. Kubenea amekuwa akitumia makundi hayo kusambaza propaganda na porojo kwamba anaonewa, anachafuliwa na kuonesha mchango wake hauna thamani. Amekuwa kiumbe wa kutafuta huruma kwa wanachama. Kidogo afanikiwe kabla ya kushtukiwa.

Kubenea na makundi yake hayo kwenye mtandao wa kijamii wa whatsApp wanamshambulia Mbowe na yoyote ambaye atathubutu Kumtetea Freeman kwa namna yoyote, hata kwa kutumia 'emoji' ni watu wa kali, hawakawii kukuita "mlamba NYAYO" ukiwakamata koromeo Kwenye hoja zako. Hata wakati ule Kubenea kavujishasha barua yake ya kujieleza kwenye kwa KM ni watu hawa walisema "Kubenea anachafuliwa"

Kubenea na Tuhuma za kuhama CHADEMA kwenda CCM..

Hizi sio tuhuma za leo, ni tuhuma zimetembea kwa muda mrefu. Ingawa ameendelea kuzikanusha. Amewajibika mara kadhaa kukanusha kuhamia CCM lakini bado anatajwa ni kati ya wabunge ambao wanakaribia "kujiuza". Hata shughuli za chama kushiriki ni kwa nadra sana. Aghalabu kumkuta anatenda kwa niaba ya CHADEMA.

KUBENEA amewahi kupewa barua ya kujieleza kutoka kwa katibu mkuu wa CHADEMA ambayo ilikuwa na tuhuma kadhaa zikiwepo kukiuka maamuzi ya kamati kuu na kuyapinga hadharani. Alituhumiwa pia kuzuia zoezi la CHADEMA ni msingi jimboni kwake. Anatajwa kuwa sehemu ya watu waliokwisha na kuchelewesha zoezi hilo sana.

Amekuwa mtu wa kupinga maamuzi yote ya kamati kuu na uongozi, alipinga maamuzi ya katibu mkuu vs Lilian Wassira pia maamuzi ua BAVICHA vs Kibona Dickson. Alilimwa barua kutoka kwa katibu mkuu kutokana na hilo. Ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani. Hakuhudhuria kabisa katika uzinduzi wa será mbadala za CHADEMA. Hii ilileta maswali, akasema "sio yeye pekee ambaye hakuwepo ukumbini"

Ushauri wangu katika hili;

Kimsingi nimekumbuka nyakati zile za Zitto na wenzake walipoanza kufuatiliwa kwa mpango wao wa mapinduzi ndani ya chama 2013, intelejensia ya CHADEMA ilikuwa Makini nyakati zile (sio sasa) waasi waligundulika mapema, wakashughulikiwa. Sasa hadi mwenyekiti anapangiwa kufanyiwa UASI, CHADEMA hawajachukua hatua kabla ba baada ya mpango mkakati kuvuja?

Sitegemei kusikia CHADEMA kama taasisi wakisema "tumezipata audio hizo na tunazifanyia kazi" utakuwa ni uzembe wa hali ya juu. Nyakati za mashaka nje ya chama, bado tunaendelea kuishi kwa 'kukumbatiana' na waasi ndani ya chama? CHADEMA imekutwa na kitu gani?

Hizi tuhuma ni jinai, ni UASI, licha ya kupelekwa polisi, muhimu zifanyiwe kazi ndani ya chama, hata wenye kuhusika na masuala ya 'intelejensia' wanapaswa kuwajibika, huu ni uzembe wa hali ya juu, taswira ya taasisi ni mwenyekiti, anaguswa vipi na 'wahuni' nanyi mpo?

Nyakati hizi sio za kumbembeleza yoyote ambaye anataka kufanya mapinduzi, UASI ndani ya chama, hawa hawana tofauti na wenye kuhamia CCM, kuwavua uanachama sio ujinga ni adabu, kuanza upya sio ujinga, wafukuzeni wote ikibidi, tuliingia mkenge mkubwa 2015, ni hatari.

Ushahidi unajitosheleza!

Namba ya mbunge wa Moshi vijijini, Anthony KOMU (CDM) katika kundi la whatsApp la "kanda ya kaskazini" ndio ambayo ilipakia ujumbe huo wa sauti, bila wengine kufahamu malengo ya kufanya hivyo.

Chini yake katika muktadha huo Kuna mjumbe mmoja (Joshua Bin Sira) alimuuliza KOMU kama ni yeye ameamua kupakia au kuvujisha ujumbe huo wa sauti, majibu ya KOMU yalikuwa ni yenye kutia shaka.

Ni namba halisi ambayo anatumia KOMU. Ni sauti halisi ya Kubenea na KOMU katika mazungumzo yao. Sababu za kurekodi ujumbe huo ndio hazifahamiki, ni bahati mbaya au ni kwa makusudi, hiyo ni kazi kitengo cha intelejensia ndani ya chama.

#MMM
 
The so-called ccm/jiwe supporters, you may think that that's right mechanism to finish Chadema/Mbowe but for sure you're slowly creating what will entirely eliminate you from tz politics. Time wilk tell
 
Back
Top Bottom