Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Viongozi wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wiki iliyopita walifanikiwa kuruka kiunzi na mtego mkali kwa ustawi wa Chama chao baada ya kuwabakiza Wabunge wake wawili walioonekana watukutu - Saed Kubenea na Anthony Komu. Hata hivyo, si kabla hawajaonyeshana ubabe wakati ambao kundi la Mbowe lilitaka wafukuzwe lakini kundi lililoongozwa na Edward Lowassa lilifanikiwa kutuliza hali na kuwabakiza Wabunge hao.
Viongozi wa Kamati Kuu waliotaka Kubenea na Komu wafukuzwe ndani ya Chama ni:
- Freeman Mbowe - Mwenyekiti.
- Mch. Peter Msigwa.
- Godbless Lema.
- Halima Mdee.
- Ester Bulaya.
- Boniface Jacob.
- Dk. Vincent Mashinji - Katibu Mkuu.
- Edward Lowassa.
- Frederick Sumaye.
- Joseph Mbilinyi.
- Prof. Mwesiga Baregu.
- Prof. Abdallah Safari.
- Arcardo Ntagazwa.
- Cecil Mwambe.
Je, haya makundi yako hivyo accidentally ama ni organized. Time will tell but bila shaka uamuzi huu utakuwa umeongeza kambi ndani ya CHADEMA kuelekea katika Chaguzi za Chama.
Wabunge Anthony Komu na Saed Kubenea.