Kafundishwa ubaya wa kukwepa kodi, kwani sio faida hiyo?Huyu jamaa ni mwanaccm kama walivyo matajiri wengi wa nchi hii , anamiliki kituo cha TV kama alivyo mwanaccm mwenzake Reginald Mengi .
Sasa cha kushangaza huyu aliamua kukiuka maadili ya utangazaji , kwa kuamua kuwanyima coverage wagombea wengine na kuwapromote wagombea wa ccm tu , na nina hakika kama tungekuwa kwenye nchi zenye kufuata sheria , vyombo vyake vya habari vingekuwa historia.
Nimebaki najiuliza hivi kwa mtu mzima kama huyu kuamua kupotosha umma kwamba ni ccm pekee inayoweza kuleta maendeleo kwa nchi hii , HUKU AKIJUA KWAMBA SIYO KWELI ( maana uko ushahidi wa wazi kwamba wameshindwa kwa karibu miaka 60 , hivyo hawataweza kwa miaka mitano ) , ALILENGA KUPATA NINI ?
Ikumbukwe kwamba kwa watu wa kanda ya ziwa kuangalia STARTV ni kama ibada , hivyo kuitumia kwa malengo ya kupotosha ni hatari sana !