Aloooh kweli nimeamini kwamba duniani kuna Siri kubwa ambayo wengi hawajui
Hawa wamarekani wametufanya tusijue Mambo yalio jificha ambayo yalipata kutokea
Haiwezekani Wagundue wao watupe sisi.
Afrika yapo maeneo yenye siri kubwa sana lakini watu ni waoga na wabinafsi kila mtu anapenda uhai na maisha yake.
Wenzetu wali sacrifice sana maisha yao mpaka kuzijua hizo siri. Usifikiri walizijua kwa propaganda na starehe ,walizijua kwa jasho na damu.
Nikupe tu mfano :
Afrika mpaka leo kuna miti hata ukiukata na machine ya namna gani hauanguki.
Kuna mapango ma milima yenye majoka makubwa yenye maajabu lakini hakuna msomi anayetafuta PhD kwa kufanya utafiti kwenye mapango hayo ajue kwa nini hayo majoka yanasemwa na je ni kweli au uongo na kama ni kweli yana siri gani?
Kuna shimo la Mungu kule mtwara ni Profesa gani alienda kutafiti huko akajua ni kwa nini watu wanaogopa kuingia huko?
Na kwa nini kuna imani kuwa mtu akishuka huko shimoni atapotelea huko? Bila shaka woga ubinafsi na hofu imetujaa .
Hayo mambo yote wazungu wanayo kwenye ramani zao wametulia tu wanatuangalia watakuja siku wachina watashuka huko watagundua kuna dhahabu ya kuokota tu halafu tutawaita wezi na mafisadi na mabeberu.
Kuna sehemu tulisimuliwa zamani kuwa maji yake yaliyokua yametokea kwa miujiza zamani baada ya ugomvi wa kifamilia na wakati wa usiku kuna maajabu na watu wanaonekana na kusikika wakifanya shughuli zao ndani ya maji na sauti za ng'ombe na mbuzi na kuku. Hata hivyo hakuna mtu hata Mimi mwenyewe mwenye ujasiri wa ku dive na kuingia huko ndani ya hilo bwawa la miujiza na kukutana na hao babu zetu wenye ujuzi mkubwa kuliko sisi. Tunasubiri wazungu wagundue halafu tuwalaumu kuwa ni wezi mabeberu na ujinga mwingine.
Waafrika ,waarabu ,wachina na wazungu kila mmoja ana historia yake aliyokua amerithishwa kwa njia ya masimulizi.Waafrika walizipuuza za kwao na kuona kuwa ni hadithi tu wakati wazungu na waarabu na wachina kwao hadithi ni kumbukumbu kubwa ya matukio ya kweli na wanafanyia utafiti kujua chanzo chake ilikua ni nini!?
Je,sio kweli kuwa hata sisi waafrika tulikua na hadithi ya majitu marefu?
Mpaka leo si bado tunasimuliana kuhusu mazimwi?
Ni msomi gani Tanzania aliyepata PhD kwa kufanya utafiti wa ukweli wa hayo mambo ? Akitokea Mzungu akaamua kufanya utafiti huo na baadae akatoa matokeo chanya tutabaki kuiomba serikali iwafukuze wazungu bila kujali mchango wao.