Antarctica bara lenye wanadamu wenye maarifa zaidi yetu

Antarctica bara lenye wanadamu wenye maarifa zaidi yetu

Kweli kabisa ushahidi unaopatikana sasa katika kipindi chetu

Unafanya tuangalie upya tena kwa usahihi Tariifa tulizonazo juu ya jamii za kale zilizotutangulia

Maana maswali ni mengi kuliko majibu

Mimi napenda sana kuunga Doti

Unajua huwa najiuliza sana kuhusiana na utamaduni wa kiyahudi ulivyoanza na ukichukulia historia yao ya wazee wao kuhama toka walipokuwepo na kuja karibu na misri

Nadhani kuna siri kubwa sana ikitegemea wayahudi wana nafasi kubwa kwenye kuchangia utamaduni wao kwenye dunia yetu
Kuna kitabu nimeanza kukisoma cha Qabalah mwandishi ni JFC Fuller, nimeanza kukisoma ila kinazungumzia watu wajinga wanaoamini Biblia nk hadi nikakata tamaa ya kuonyeshwa ujinga wangu wa kuamini dini yangu hii. Lakini nitaendelea kukisoma hadi mwisho, kama ni evidence ya ukweli Roho wa Mungu atanionyesha.
 
Mkuu ukisoma kitabu cha Jasher (unaweza kuki download freely) kinasema ukubwa wa mnara wa Babeli ni hivi.

:Foundation yake mzingo ni safari ya mtembea kwa miguu wale wa zamani kwa siku tatu bila kupumzika.
:
Height yake kwenda juu ni safari ya mwaka mzima " go and return " na hii ilisababisha mafundi kushindwa kuendelea na kazi baada ya Mungu kuwavurugia lugha kwa maana mafundi walioko juu wakiagiza tofali au maji, safari ya kufuata kifaa chini iligharimu mwaka mzima yaani kushuka chini na kurudi juu, mtu anaagizwa alete tofali yeye analeta maji baada ya mwaka. Mradi ukafa.
Mwenyezi Mungu wala hakutumia nguvu akili kidogo akawa vuruga waka poteana.
 
Jinsi unavyo chimba zaidi kujua ndivyo utajikuta hakuna unalolijua maana utaishia kuchanganyikiwa tu mambo yako complicated
Ni kweli kabisa mkuu lakini sikati tamaa ya kusoma zaidi, naomba tu share book and knowledge
 
Kuna kitabu nimeanza kukisoma cha Qabalah mwandishi ni JFC Fuller, nimeanza kukisoma ila kinazungumzia watu wajinga wanaoamini Biblia nk hadi nikakata tamaa ya kuonyeshwa ujinga wangu wa kuamini dini yangu hii. Lakini nitaendelea kukisoma hadi mwisho, kama ni evidence ya ukweli Roho wa Mungu atanionyesha.
Kuna mtu uwa anapenda niambia be careful with the information you read.
Kwa mfano hivi wajua karibia dini zote kuanzia Hindu, Budha hadi dini za kale za Egypt uwa ndani yake kuna story inayofanana na Yesu, kuzaliwa na mwanamke Bikra, kuwa binadamu mwenye nguvu za Uungu.. na mengine. Na ni dini ambazo ni za kale zaidi ya Ukristo?
 
Kuna kitabu nimeanza kukisoma cha Qabalah mwandishi ni JFC Fuller, nimeanza kukisoma ila kinazungumzia watu wajinga wanaoamini Biblia nk hadi nikakata tamaa ya kuonyeshwa ujinga wangu wa kuamini dini yangu hii. Lakini nitaendelea kukisoma hadi mwisho, kama ni evidence ya ukweli Roho wa Mungu atanionyesha.
Shida ni kwamba watu wengi wana chuki na wayahudi kwa sababu zao binafsi

Jambo ambalo linawafanya kuwa vipofu juu ya ujumbe wa kitabu chao
 
Mkuu kwa bandiko lako hili, kuna watu hasa wasiopenda kujisomea watapotoshwa na baadhi ya taarifa zisizo za kweli. Antarctica yaani " Terra Australis" ni kontinenti la tano katika dunia hii linayopatikana katika ule mzunguko wa kusini kabisa mwa dunia hii. Ukubwa wake ni karibia mara mbili ya ukubwa wa Australia na eneo hilo lote limefunikwa na barafu kwa kiasi kikubwa.

Bara hili lina baridi kali upepo mkavu unaolifanya eneo zima kutokuwa na mazingira ya kuruhusu binadamu kuishi bila kutumia nishati au nyenzo za ziada ili kuyashinda mazingira yake yasiyo rafiki. Mbali na binadamu kuna wanyama kama Seal,Penguine, na Nyamgumi ambao wameumbwa kustahimili mazingira yanayoweza kuwa na jotohasi linalofikia centigrade -63. Zaidi ya watafiti kutoka baadhi ya mataifa makubwa ya UK, France, Russia, Germany ambao wana kambi kule kwa ajili ya uchunguzi, hamna taifa lililoweka makazi katika eneo hilo.

Uwepo wa kontinent hili ulikuja kujulikana kwa mataifa mengine mwaka 1820 wakati wapelelezi wa kurusi na kijerumani walipouona mlima wa barafu kwa mara ya kwanza wakiwa kwenye safari za kiupelelezi, hata hivyo watu wa kwanza kutia nanga na kukanyaga ardhi ya Antarctica ni wachunguzi kutoka Norway kwenye mwaka 1895. Hapa inasadikiwa kuwa wanorway katika mazingira hayo ya baridi wanayamudu kwa kuwa nchi yao iko karibu sana na ule mzunguko wa kaskazini.. "Arctic Circle".

Antarctica ni eneo linalolindwa na mikataba ya kimataifa hasa ule wa Antarctic Treaty wa 1959 ambao ulisainiwa na nchi 12 mwanzoni na baadae kufikia nchi 38.. Mkataba huo unazuia matumizi ya eneo hilo kijeshi,kuchimba madini, kufanya majaribio ya kinuklia, kutupa taka taka za aina yoyote ile. Zaidi ya uchunguzi wa kibaolojia unaoendelea huko kwenye kambi inayoweza kupokea wanasayansi wapatao 4000, kuna mpango unaopangwa kuanza hivi karibuni wa kulifanya eneo hilo kama hifadhi ya Dunia na umetangazwa rasmi wiki iliyopita.
 
Aloooh kweli nimeamini kwamba duniani kuna Siri kubwa ambayo wengi hawajui

Hawa wamarekani wametufanya tusijue Mambo yalio jificha ambayo yalipata kutokea
 
Aloooh kweli nimeamini kwamba duniani kuna Siri kubwa ambayo wengi hawajui

Hawa wamarekani wametufanya tusijue Mambo yalio jificha ambayo yalipata kutokea
Ni kweli _na yote inatokana na kupenda kutafuniwa taarifa na kumeza tu

Na ndiyo ilivyo hulka ya mwanadamu wa kawaida IQ zero

Kuna watu wanapenda control sasa wakikuta Mazezeta yasioyopenda kuhoji kwao ni Raha
 
Mkuu kuwa makini sana u apokuwa unafuanya ufuatiliaji/research/kusoma.sio kila kinachoandikwa ni cha kweli,kwenye ilmu/historia kuna upotoshaji mkubwa na uchanganyaji wa facts na fiction.Hata kwenye maelezo yako kuna vitu umeandika ni known facts,kuna vyengine fiction,kuna speculations na vyengine mseto wa vyote.
Sasa wewe titi si ungesema hizo fact zako ili tujue ukweli? Kuliko kuja hapa na kuandika nusu utadhani jamaa kasema ndiye aliyeishi antarctica
 
Habari nyingine za ma-archeologist sio za kweli, hawa wanajifanya wana evidence ili kuweza ku proove umri wa existence ya binadama kwa kutumia michoro au majengo, vitu vingine sio vya kweli, ni vya kutengeneza tu, inawezekanaje alama ya mguu wa mtu ikawa engraved kwenye mwamba wa jiwe au alama za mapangoni zinaweza kuwa pia printed kwenye mwamba ili kutengeneza future history kutoka kwa wajenzi wa falsafa za dunia.
Well said walahi
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia kuhusu hili bara la antarctica kupitia vyanzo mbalimbali na nimekuwa nikistaajabu sana juu ya mambo ambayo yamejificha kwa miaka mingi na ambayo wanao yafahamu hawataki yafahamike sijui kwanini.
Lakini kila lililofichwa litafunuliwa na kuwa wazi kwakuwa sasa mambo yameanza kuwa hadharani baada ya theluji kuanza kuyeyuka katika bara hilo na mambo mengi kuanza kuwa wazi.
Kihistoria kwa muda mrefu binadamu hakuwa akijua kama kuna bara liitwalo Antarctica mpaka mwaka 1773 ambapo Nahodha ajulikanaye kama James Cook akiwa na wenzake ndipo alipoweza kugundua uwepo wa bara hilo. Lakini ajabu ni kwamba kuna ramani inayoonyesha Antarctica ambayo iligunduliwa huko Uturuki ambayo inadaiwa kwamba ilichorwa na kamanda kikosi cha maji cha jeshi la Uturuki mwaka 1513 aliyejulikana kwa jina la Haji Ahmed Muhiddin Piri , na ramani hiyo inaonyesha kuwa bara la Antarctica halikuwa na barafu.
Ina aminika kwamba Waturuki hawakuwahi kuvuka Bahari ya Midditeranean sasa waliwezaje kuchora ramani hiyo? Na wataalamu walivyoifanyia vipimo waligundua ilikuwa ina vipimo sawa kuliko hata ramani za kisasa. Katika ramani hiyo inaonyesha baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa vikipatikana katika bara hilo jambo ambalo lilikuja kuwa kweli ambapo NASA ilitumia satelite inayoweza kuangazia eneo na kupredict kilichoko chini na walipoitumia kwenye bara la antarctica ilionyesha mambo mengi yaliyokuwa chini ya barafu kama uwepo wa milima, mabonde, miamba, mito iliyoganda na kadhalika.
View attachment 920837
Kwa muda mrefu kuna shughuli za kijeshi na kiunguzi zilikuwa zikiendela huko katika bara la Antarctica kwa siri sana, na aliyeanzisha alikuwa Hitler ambaye alikuwa akiamini sana katika mambo ya aliens na super being. Kati ya mambo mengi aliyofanya hitler ni kufanya tafiti za mambo haya. Hitler alifadhili shughuli za kiutafiti mpaka Mesopotania, Uturuki, Antarctica na kila mahali alipowahi kusikia kulikuwa na na ealry civilizaition.
Hitler alipeleka wanasayansi na jeshi kubwa kufanya tafiti huko Antarctica na inasemekana kwamba aliweza kukuta teknolojia ya jamii ya watu ambao walikuwa ni wakubwa zaidi yetu wengine wakiwa hata na futi 18 kwa urefu. Jamii hiyo ilikuwa imeendelea ikiwa inatumia usafiri wa saucers na hitler aliweza kufanya back engineering na kutengeneza flying saucers zake. Kama utakuwa umefuatilia matukio ya watu kudai wameona flying saucers hasa wanajeshi wa Marekani yametokea miaka hiyo na inadaiwa zilikuwa ni silaha za NAZI walizokuwa wametengeneza kutokana na ugunduzi wao huko Antarctica.
View attachment 920848
View attachment 920849
Kwa taarifa zilizpo ni kwamba moja ya sababu ya wale wajulikanao kama the Allies akiwemo U.S kuungana kumtwanga Hitler ilikuwa ni kumuwahi kwakuwa waligundua amegundua teknolojia ambayo wakimuacha akaweza kuitumia vilivyo basi hawatakuwa na uwezo wa kumzuia. Walianza kwa kufanya jaribio la kuvamia military base yake huko Antarctica ambapo flying saucer ya NAZI iliwatandika vibaya na kuzamisha meli zao na kusababisha vifo vya maelfu ya askari.
baada ya kumalizika kwa vita marekani alianzisha military base yake huko na kuanza kuchunguza mambo mengi ambayo yamebaki kuwa siri.
Lakini hivi karibuni barafu imeyayuka na ukitumia google earth utawaeza kuona pyramids kadhaa, majengo, masalia ya makazi, na kuna picha nyingi ambazo serikali ya marekani imeitaka Google iondoe kwenye ramani zake zinazohusu Antarctica.
Moja wapo ya picha za hivi karibuni ni hiii hapa ambayo ilikuwa inapatikana Google earth ikiwa na coordinates.
View attachment 920858
Hii picha Google imeiondoa na kuanza kudai kuwa ni fake lakini wajuzi wa mambo wanasema kuwa ni moja wapo kati ya vifaa vya jamii hiyo ya kale iliyoishi Antarctica.
Je nini kiliikumba hiyo jamii?
Wajuzi wa mambo wanadai ya kwamba ilitokea janga la kiasili ambalo ndilo lilisababisha hata kuzama kwa Atlantis na hilo janga ndilo lilisababisha kuhama kwa polars na kuwa zilipo leo. Hivyo Antarctica kabla ya hilo janga hakukuwa na barafu wala baridi kama ilivyo leo.
Kuna mengi ya kujadiri moja wapo ni kwamba kuna upenyo wa kuingia ndani ya dunia eneo hilo ambako kuna jamii nyingine inaishi huko.
Pia kuna miji mingi ya kale imegunduliwa chini ya bahari inayoashiria kuwa walioishi kwenye miji hiyo wlaikuwa wana kimo kikubwa zaidi yetu kutokana na ukubwa wa majengo pamoja na ngazi za kupandia ambazo unakuta ngazo moja ina urefu kuliko binadamu wa kawaida.
Mwisho namalizia kwa kuwakumbusha kuna tukio lilitokea mwaka huu kama siyo mwishoni mwa mwaka jana wakati makandarasi wakichimba chini ya Msikiti ma Mecca walikutana na box ambalo walipolishika lilitoa Gama rays ambazo ziliua mamia ya watu. Ni tukio lilitangazwa kama lilivyo ila baadae wakabadiri na kusema ni crane zilianguka zikagongana na kuua watu 107View attachment 920872
Inasemekana Warusi ndiyo walikuja kulitoa hilo Box na kulionekana msafara wa Manuari za kivita na nyambizi na wanajeshi 4500 wakilisindikiza kuelekea Antarctica, na kabla ya kufanya hivyo Papa na Kiongozi wa kanisa la Urusi la Orthodox walikutana Cuba kujadiri juu ya suala hilo.
Yapo mengi sana ila nimeandika kwa kifupi tu.
That is true, ndugu ni kweli kabisa bila uongo, kuna siri nzito sana
 
Ni kweli _na yote inatokana na kupenda kutafuniwa taarifa na kumeza tu

Na ndiyo ilivyo hulka ya mwanadamu wa kawaida IQ zero

Kuna watu wanapenda control sasa wakikuta Mazezeta yasioyopenda kuhoji kwao ni Raha

Ndo Ivyo mkuu
 
Back
Top Bottom