Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,907
2,000
Kuna ushahidi Musiba alihudhuria? Kama ni kweli alihudhuria, shutuma alizozitooa hadharani anawajibika kudhibitisha. Na kwenye kikao cha ulinzi na usalama, ni sehemu sahihi ya yeye kuitwa kuthibisha hayo mazito aliyoyasema kwa kuwa yanagusa usalama wa Taifa.
Hii nchi ina usalama wa taifa au wa ccm??
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,792
2,000
Mkuu Mwanahabari huru, kumbe upo?, kwa vile Ngurumo mwenyewe ameishaingia humu mazima in person akiwa ni verified, nakushauri sasa pumzika, acha mwenyewe aje, tubanane nae humu humu.

Ni kweli kuna kitu nimeona hapo sio tuu ni hatari kweli bali kinatisha, sisi ambao hatuna mahali pa kukimbilia, kuna wakati, unapaswa kufunga tuu mdomo na kushangaa, kama mimi ninavyoshangaa kwenye bandiko hili na haswa the authenticity of the story, ikizingatiwa imeripotiwa na mhariri wa kuaminika, ila pia inaweza kabisa kuwa ni concoction kwa sababu hata waandishi wakubwa na wahariri kama kina Salva, na Mtanzania, waliwahi ku concoct na kushuka na concoction kumhusu Dr. Salim Ahmed Salim.

This is something serious, something big, something very dangerous, mpaka sasa mimi bado siamini!.

Tusubiri.

P
Wewe tulia ukae kwa Amani kwani ukithubutu kugusa masilahi ya Maliyamungu Bashite ujue yatakukuta kama ya Lisu kule Dodoma alipogusa masilahi ya 10% ununuzi wa ndege na Siri za kuikomboa ndege kwa Siri kimya kimya apate kupiga cha kingine, tulia usiguse Dili za Naibu Rais Maliyamungu idd Amin Bashite utaishi kwa Amani na Heri Kisanduku makapero hatakaa apajue kwako.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,907
2,000
Mwanahabari Huru naona sasa umebobea kuleta taarifa za uchochezi hapa JF na Moderator wamekuacha tu!! Sina uhakika kama unaweza kutudhibitishia taarifa hii kama ni ya kweli kwa kuwa wewe ndiyo unaisambaza!!
Mtakimbiana mwaka huu, mkuu kumbe Mtulia yuko hoi?? Ila dua aliyoomba Mwalimu Salum pale viwanja vya buibui mwananyamala kinondoni, aliapa na kujiapiza atakaeshiriki kwa namna yoyote kudhulm nafsi, uhai, damu na ushindi wa mtu atateketea yeye na ukoo wake. Mtulia tayari hatujui ukoo wake, vipi wsle polisi walioua Aquilina? Vipi Makonda na timu yake?
 

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Oct 25, 2016
1,631
2,000
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Kufuatana na sheria za kikimbizi mkimbizi haruhusiwi kutumia nchi alipo kimbilia kuanza kuichokoza nchi yake alipotokea. - Ansbert jiongeze -
 

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,090
2,000
Duh. Huu upotoshaji wa CHADEMA, wanaongea lolote ili kujihami na maovu yao wanayoyafanya kila siku.
Yaani wao ni kubashiri lolote jf ili kulinda maovu yao. Mmeongea utumbo mwingi wa vikao bila ushahidi wowote.
 
Jan 23, 2018
72
95
Doh, dadeki bora Magu alivyowalipa hao jamaa wa Stirling. Mnajua hawa Stirling kumbe walishafungua kesi ingine hapa marekani wakitaka kushikilia na Boeing inayotengenezwa hapa. Kesi ilifunguliwa mwaka Jana October, Washington DC, sababu kule ndio kuna ubalozi wa marekani . Oneni mlalamikaji kaifuta lini kesi ya hapa marekani. Kaifuta juzi tarehe 29 baada ya kulipwa na Magu. Na ukiangalia mlolongo wa kesi, Tanzania ilifika mahakamani January 2018 kujibu kesi. Baada ya kutokea mahakamani ndo wakamalizana na Stirling Engineering.
.
.
Ingieni google and search Stirling civil engineering vs United Republic of Tanzania
.
.
Mzee huyo ukurupukaji wafanyiege huko huko Tz, kuna wengine ni majiwe kweli kweli. Ona sasa ulichozea dola milioni 38 za walipa kodi for absolutely nothing.hii inatisha sana uruhusiwi kusema ukisema wewe ni mhaini vngoz wa chadema wanakosa gani? Kosa lao ni kusema?
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,920
2,000
Asylum ya kubumba inagharama za kuharibu credibility na ethnicity ya mtu. Kwani nilazima utengeneze justifications zisizo na mashiko. Ole wako wale unaowadanganya wakikushtukia....! Hii dunia ukubwa wake utauona kama sawa na ule wa yai la mjusi.
 

bhokesa

Senior Member
Feb 23, 2018
138
250
Duh!.
Ngurumo, Ngurumo, Ngurumo...
Hii kali...
Kwanza kwaheri

kisha karibu

Hii ya kwako Ngurumo kali!, yaani wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam wanaripoti kwako Ngurumo!...
bora umekimbia! maana...

Hata hivyo, kwenye tasnia ya media, hakuna kitu kama MBM, kilichopo ni waandishi wasio ma mipaka, Journalists San Frontiers
P
Mayala, hata swali ulilouliza rais kuhusu kuvunja katiba ulikuwa kazini? Hata kama raisni msukuma ndo mmeamua kutuuua? Kutuonea? Ni dhambi ipi kuwa upinzani? Halafu huu urais wa wasukuma hautaisha? Mmeamua kuvuruga nchi na kutesa watanzania? Haya ni wakati wenu.
 

dafity

JF-Expert Member
Aug 16, 2008
1,772
2,000
Kufuatana na sheria za kikimbizi mkimbizi haruhusiwi kutumia nchi alipo kimbilia kuanza kuichokoza nchi yake alipotokea. - Ansbert jiongeze -
Umewafuatilia Edward Snowden na Julian Assange wanadili vipi na nchi zao wakiwa huko ukimbizini?
Fanya utafiti
 

MAGO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,176
2,000
ma
Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
mange kimambi huwa anazipata vipi? kikubwa hapa kuna wau wengi tu walioko kwenye system hawapendi na hawafurahii yanayoendelea ila tu hawana pa kuongelea. So kweu sisi watu kama kimangi na hata hyu Ngurumo ni muhimu sana kwa jamii yetu kwa sasa.
 

Daniel kulwa Nyawayi

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
277
250
Inamaana amezipata hizi taarifa akiwa huko ugaibuni? Kama ni hivyo sasa nihatari,nani amemfikishia taarifa za kikao hicho? Kwa kifupi kuna uvujaji mwingi sana wa taarifa kama ni hivyo,haiwezekani mtu yuko ugaibuni akaqeza kudukua siri za vikao hapa kwetuu
Kama Marekani alidai uchaguzi wake umedukuliwa na Mrusi sembuse nchi masikini na hisiyo na teknolojia kama ya kwetu!!!?
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,792
2,000
Duh. Huu upotoshaji wa CHADEMA, wanaongea lolote ili kujihami na maovu yao wanayoyafanya kila siku.
Yaani wao ni kubashiri lolote jf ili kulinda maovu yao. Mmeongea utumbo mwingi wa vikao bila ushahidi wowote.
Wewe acha ufala utumbo mnaongea nyie vilaza wa Le mutuz na Boss wenu Maliyamungu Bashite, akiongea Msiba ujinga mnaomtuma mbona hamuombi ushahidi wowote? Ya msiba hatahitaji ushahidi lakini ya chadema kuwajibu CCM mnataka ushahidi? Tambua kuwa watanzania si wajinga kiasi mnachofikiria wanajua kutafakari ni yupi kati ya CCM na chadema anayewahadaa watanzania.
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,792
2,000
Mtakimbiana mwaka huu, mkuu kumbe Mtulia yuko hoi?? Ila dua aliyoomba Mwalimu Salum pale viwanja vya buibui mwananyamala kinondoni, aliapa na kujiapiza atakaeshiriki kwa namna yoyote kudhulm nafsi, uhai, damu na ushindi wa mtu atateketea yeye na ukoo wake. Mtulia tayari hatujui ukoo wake, vipi wsle polisi walioua Aquilina? Vipi Makonda na timu yake?
Naibu Rais ndugu Maliyamungu Bashite na kikundi chake saa 24 wanashinda na waganga wa kienyeji wanaishi kwa wasiwasi hawajiamini
 

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
1,967
2,000
Aaah wapi......this is just a guessing
Kuna baadhi ya mambo ni ya kufikirika unaweza kuyaweka kwenye maandishi yakaonekana ni ukweli kutokana na wakati tuliopo
Mfano
kama ambavyo wengi wetu tunajaribu kumhusisha MBOWE na UPOTEVU wa SAANANE...
Au kuwahusisha CHADEMA NA BAADHI YA MAUAJI

Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
WHAT IF IKITHIBITIKA HUU MUDA PIA MAKONDA ALIKUWA KANISANI?
Me naomba tufatilie ni wapi jana MAKONDA ALISALI...hili tuthibutishe hiki

Hivyo nyie k.m. mnataka nini hasa? Hamna kingine cha kuwaeleza watu zaidi ya Magufuli kafanya nini au Makonda kafanya nini? Hamwoni kama nyie ni wajinga wa akili? Mna amini vitu ambavyo havina maana yeyote kwa taifa letu na maendeleo ya binadam. Watu wazima mna behave kama watoto wa darasa la kwanza?

Rais hawezi kuondolewa kwa kuandika upuuzi. Kama hamumtaki kuna legal processes zimewekwa za kufuata. Subirini 2020 mumpigie kura mtakaye mwona anafaa kuwaongoza. Mwacheni Magufuli amalize kazi yake halafu ndiyo mje na matakwa yenu.

Rais yeyote duniani akiapishwa tu lazima atawaweka watu anao waamini kuongoza serikali yake. Kama nyie ma-journalist uchwara hamumtaki RC Makonda nendeni basi 2020 mkachukue forms za kugombea urais nyie wenyewe ili muwachague watu mnao wataka kutawala.
Rais Magufuli yeye wamemwona Paul Makonda anafaa kumsaidia kuongoza. Mbona anafanya kazi nzuri?

Niwaambie siri wajerumani, watu au taifa ambalo limeendelea sana ki-technic na ustaarabu duniani, waliwahi kuwa na waziri wa mambo ya nchi za nje kwa jina anaitwa Yoshka Fisher ambaye hata highschool hakumaliza, sembuse chuo kikuu? Ajabu ni kwamba mpaka leo, kama nitakuwa na takwimu za uhakika, hakuna kiongozi mwingine ambaye amewahi kupendwa kama yeye. Na alifanya kazi yake vizuri sana.

Résultats Google Recherche d'images correspondant à https://charlie-p-2ac84d7056ca7f9d.s3.amazonaws.com/clips/thumbnails/000/005/811/medium/1HY7885_005_lt.jpg?1481902914

Halafu nyie wenda wazimu na watu ambao hata kuta za chuo kikuu hamjaziona kwa ndani mnathubutu kutwa kucha kupiga soga la Mh. Makonda kana kwamba yeye naye ni mwuuza madawa ya kulevya kama nyie bila haibu na sentimental, Ai see, mnasikitisha Sana.

Yaani nyie mnajiona mna akili kuliko watanzania wote walio mpigia kura Magufuli na hapo hapo kutuzuga tena! Nyie washamba sana. Yaani kwa uongo wenu usio na kichwa wala miguu, mnaoneka kama vile mmetoka bush leo! Yaani ni wakamba kupindukia. Ni vikaragosi. U-journalism gani huo? Huo ni ukoma kwa taarifa zenu. Nendeni kwenu vijijini mkawadanganye mababu na mabibi zenu.

Ma-journalist wanuka jasho wala kuoga hamwogi mnathubutu leo kutufundisha sisi uongo na upuuzi wenu kuhusu Makonda, are you really serious?

Nasikitika Rais Magufuli ana huruma sana na nyie, haki ya Mungu! Ningetamani wote nyie awaweke jela na kuwafungia leseni zenu za u-journalist uchwara kama mnazo.

Nyie ni wababaishaji. Hiyo kazi hamwiiwezi. Wahuni tu nyie wa mitaani na sio jingine. Mmejazwa udaku tu ambao mnataka kututapikia sisi. Ningewashauri mwache ujinga wenu. Sisi sio watu wa level yenu wakutuletea ukoma wenu.

Kuandika uongo ni ofend pia, mkae mkijua! Mkishikwa na kutiwa romande mnaanza kulialia. Eti mnajiita ma-journalist, Ma-journalist gani nyie wakuandika mambo ya uchi uchi! Mmesomea wapi? Pangoni? Nendeni mkafie mbali wasaliti wa nchi yetu nyie.

Mnajua kuwa nyie ni wauaji wakubwa wa jamii yetu kwa uongo wenu? Mna uhakika RC Makonda anaweza akafanya kikao cha usalama kujadili uchawi kweli? Mnaamini hivyo kweli? Au mna lengo la kuwapumbaza watanzania kwa maovu yenu?

Kama mnataka vita si nendeni Syria mkapigane? Kwa nini mnatufuatafuata sisi na viongozi wetu? Hamwoni kuwa mna bor? No one on Earth can take you seriously!

Wenzetu wazungu wana waza jinsi gani ya kuokoa binadam kwa janga lijalo la environment, ili aende kwenye Safari nyingine, nyie ndiyo kwamza mna limbuka na viji-devices vya Samsung na Aple kuandika mambo ya **** ****.
Pelekeni ushoga wenu huko kwenu mnakotoka.

Nyie ni vichaa na manyang'au!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom