Ansbert Ngurumo: Paul Makonda aongoza kikao cha maangamizi ya CHADEMA ambacho ni hatari kwa Taifa

The man is very smart in head and very intelligent. I like him the way he speak and everything he does, he does his things systematic always. I like the way he spoke yesterday, he was not reading anywhere? That kind of leaders we want alll the time sio viongizi wa kuwachezea kama watoto. Muda wa kuchezeana ulishapitwa Hapa Kazi Tu
Una akili za kitoto sana.
 
Nina maswali machache kwako mwandishi kwanza umesema kikao cha siri, wewe ulijuaje kama kirikuwa cha siri. Au nawe ndo umeamua kutengeneza Propaganda zako utuletee hapa, sidhani kama kikao cha siri wewe unaweza kufahamu kinafanyika wapi na muda gani?
maswali ya mtoto wa chekechea.watu wengine si mkae kimya tuu!
 
Musiba anatuletea habari na vielelezo (evidence) Sasa hii ya kwako ni kama katiba kwamba tuikubali duuuu
Msiba kakupa evidence ipi ndugu yangu kuhusu magaidi aliyowataja???. Huoni kama wote anaowataja ni kama ni adui wa chama tawala
 
Magufuli ameweka historia kuwa "msukuma" wa kwanza kuwa Rais wa nchi yetu. Lakini ameweka historia pia kuwa Rais mbovu kuliko wote kuwahi kutokea katika nchi hii. hata kama atajenga madaraja milioni moja, fly-over 500, na kuweka treni za umeme, kitendo cha kutothamini uhuru na uhai wa binadamu mwingine, ni kitendo hata wanyama hawafanyi. Bahati mbaya kwa wasukuma kwamba rais wa aina hii ni msukuma. pia sina hakika sana na usukuma wake, maana wasukuma tunawajua sana tu. nadhani anahitaji kuhojiwa na uhamiaji
 
mkewe alitutahadharisha kwamba mumewe ni kichaa aliwahi kupiga mototo wake na kumuaua bado tukambeza,,acha tuvurugwe dadeki
 
Hakuna siri tena. Leo tarehe 30:03:2018, saa tisa kamili (9:00) alasiri, saa ambayo Bwana Yesu Kristo alikata roho msalabani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika muda ule ule, Paul Makonda, alikuwa anafungua kikao maalumu cha kupanga mambo maovu dhidi ya viongozi waandamizi wa Chadema na wakosoaji wengine wa serikali. Kikao hicho, ambacho alikiita kikao cha “ulinzi na usalama,” katika ukumbi wa polisi Kurasini, kiliahirishwa saa moja kamili (1:00) usiku.
Katika kikao hicho, yalijadiliwa mambo mengi mazito.

Nimechagua machache tu yafuatayo, ndiyo nitaweka bayana, ili kuonyesha dunia jinsi kiburi, jeuri, sifa na madaraka ya watu wawili (JPM na Makonda) vinavyohatarisha usalama wa taifa letu. Mengine yanafanyiwa kazi na vyombo muhimu.

1. Mbali na Freeman Mbowe na viongozi wenzake walio gerezani Segerea, wengine waliojadiliwa na kikao hiki, ambao watakamatwa muda wowote kuanzia sasa ni wabunge: Godbless Lema (Arusha), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Esther Bulaya (Bunda), Joseph Selasini (Rombo), na kiongozi wa Jumuiya za Kiislamu, Ustadhi Rajab Katimba. Eti hawa ni "majasusi wa Chadema!"

2. Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Bw. Cyprian Musiba, ambaye amekuwa anakutana na waandishi wa habari na kutoa matamko ya shari na tuhuma kali dhidi ya watu wanaokosoa serikali. Alikuwa kikaoni - kikao cha “ulinzi na usalama” mkoa wa Dar es Salaam. Katika moja ya hoja zake, alisema Ansbert Ngurumo anachafua serikali akiwa huko Ulaya; na kwamba ingekuwa vema serikali iweke utaratibu wa kumfuatilia huko aliko na kumdhibiti. Baadhi ya wajumbe walisema hakuna haja, bali serikali ibane hawa hawa waliopo nchini, hasa Heche na Lema. Hasira dhidi ya Lema zilitokana zaidi na kauli yake kutaja Dk. Modestus Kipilimba kwamba anashinikizwa na kushirikishwa katika kupanga mateso dhidi ya wapinzani. Mbali na kusaka fursa ya kumtesa, wanatengeneza “mabomu” dhidi ya mbunge huyo wa Arusha.

3. Wamekerwa na suala la ugonjwa wa Abdallah Mtulia (mbunge wa Kinondoni) kujulikana, wakadai kwamba ugonjwa wake umesababishwa na Chadema. Mtulia ana hali mbaya hospitalini. Makonda na Musiba wamejiapiza kuwa watapambana na Chadema kwa mbinu zote kwa kutumia dola na "uchawi."

4. Kesi ya Mbowe inawapasua kichwa, inawatia hofu (kwa sababu ni ya kubumba); hata mawakili wa serikali wamesema wanalinda hadhi ya taaluma yao, hawataki kuchafuka au kuchafua taaluma zao kwa kesi za kubumba za polisi.

5. Serikali inakerwa mno na taarifa za vikao vyao vya siri kuvuja, na jambo hili linawafanya wachelewe kutekeleza uovu wao wanaopanga dhidi ya Mbowe. Wamesema zamu hii watakuwa makini zaidi.

Yapo mengi, lakini haya ndiyo nimeona vema niyaanike hapa, ili Watanzania na dunia nzima ijue kinachoendelea nyuma ya pazia, wajue aina ya “viongozi” walionao, na wajue nani anahatarisha usalama wa nchi. Hivi ndivyo Bashite na kikosi chake walivyoadhimisha Ijumaa Kuu – kwa kumkejeli Mungu!

MASWALI MAGUMU:
a) Bado Watanzania mnajiuliza nani anamtuma Musiba kufanya press conferences na kutoa matamko ya kushambulia watu kwa tuhuma za ajabu ajabu?
b) Bado mnataka kujua mamlaka inayomlinda Musiba?
c) Idara ya Usalama wa Taifa haijui haya au imenyosha mikono, inafuata maagizo, na imeamua kuacha hatima ya usalama wa nchi hii mikononi mwa watu wawili?
d) Kuna mtu anadhani Makonda anafanya haya kwa hiari yake tu, bila idhini na baraka za Rais Magufuli anayesema maneno ya ajabu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wake, hadharani bila aibu, kwamba, “sijaribiwi…. nitawavunja miguu?”
e) Kwa mikakati hii, kwa kuhatarisha badala ya kulinda uhai na usalama wetu, rais anadhani nchi iko salama, na yeye mwenyewe yuko salama?
f) Wakati uovu huu unapangwa rasmi, Rais Magufuli alikuwa kanisani kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, “anasali.” Je, naye alibusu msalaba? Kama ndiyo, busu lake lina tofauti gani na busu la Yuda kwa Bwana Yesu – busu la usaliti kwa Watanzania alioapa kuwalinda?
g) Mateso na vifo vya wapinzani na wakosoaji wake ndiyo zawadi ya Pasaka ambayo rais anaandalia Watanzania mwaka huu 2018?
h) Kama utawala wa Kaisari uliangukwa kwa sababu ya kiburi, jeuri na ulevi wa madaraka, utawala wa Magufuli utanusurika vipi ukiwa na sifa zile zile?

Mengine nabaki nayo. Tuendelee kutafakari haya.

Ansbert Ngurumo
MHARIRI BILA MIPAKA (MBM)
Mtulia anaendeleaje?,mlitupa habari kuwa yu mahututi,wa leo wa kesho.
 
Dalili ni mbaya mno kwa serikali ya sasa kwa kuamua kugombana na maaskofu.
Bila kupima uzito wala kutumia akili, angalau kidogo, Bashite amejipa majukumu ya ugomvi huo, akianza na mbinu dhaifu kabisa ya eti kuwachafua maaskofu ambao kimsingi, wana daraja la manabii.
Machi 26 mwaka huu wakati wa
kuzindua magari ya MSD Bashite aliwaambia waheshimiwa waliokuwa chumba cha kumsubiria mgeni rasmi kuwa Askofu wa Karagwe na wa Lushoto ndio vinara wa waraka wa KKKT.
Akasema ameambiwa na Askofu mwenzao ambaye aliwapiga chenga na kukataa kuhudhuria kikao cha maaskofu.
Bashite alidai Askofu huyo amemuapia kuwa waraka huo hautosomwa katika dayosisi yake. Bashite akasema atawakomesha kama alivyomkomesha Gwajima.
Akasema anao wanawake walio tayari kuitetea nchi. Aliungwa mkono na Mkuu wa "kitengo" Kanda ya DSM. Viongozi wa Wizara walikuwepo walibaki kimya.
Kesho yake Bashite alimwagiza Dr. Abbas (Msemaji wa Serikali) kutafuta gazeti la kufanya kazi hiyo. Dr. Abas alipost kwenye group fulani habari za gazeti la udaku la mwaka 2015 zinazomhusu Askofu wa Karagwe. Siku hiyo hiyo Bashite akapost sala maalum inayowalaani maaskofu. Jumatano Bashite akapost maelezo kuwa anahitaji habari za viongozi wa dini waliotelekeza watoto. Kwa kuwa ni Bashite na Dr. Abbas, hii ni vita ya serikali na maaskofu. Waraka umekolea.
!!!!????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom