Ansbert Ngurumo, Neville Meena, Jesse Kwayu, na Absalom Kibanda, mjue mpo kwenye binocular, hiyo ni shibe ya muda tu

troiker

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
1,430
2,264
Hawa wahariri kwa sasa wanalamba asali haswa chini ya waziri wa habari na utangazaji Nape Nnauye, hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyefahamu jambo hili.

Watu hawa wameuza utu wao kwa vipande vya dinali zitokanazo na kodi, tozo mbalimbali za Watanzania maskini.

Kuna mambo ya kifisadi nchi hii yanaendelea, wanayajua lakini kwa kuwa wanalamba asali, wapo kimya! Imani yao ipo kwa Nape Nnauye ili awape shavu serikalini, ikiwemo na ahadi ya ukurugenzi mawasiliano Ikulu. Hivyo wameamua kufubaza taaluma zao katika kulisaidia taifa.

Napenda kuwakumbusha raha hizi mzipatazo kwa sasa ikiwemo ukwasi mnaodunduliza huko mbeleni mtazitapika tu, kama sio nyie basi kizazi chenu. Nasema tena binocular inachungulia na kurekodi maisha yenu ya kila siku.

Vyombo vyenu vya habari vinatia kinyaa kwa sasa, hakuna criticism nyuzi za kuisaidia serikali, mmejaza mapambio na habari nyepesi nyepesi sana za wizi wa kuku, na matukio ya ngono ya nchi za jirani zetu. Lingine kubwa mnaloliweza ni kupambana na Marehemu hayati Magufuli, kwa ujira wa mafisadi.

Nasikia pia mmezindua kitabu cha mashambulizi kwa hayati Magufuli, mkiishambulia Chato kwa kuwa huko wanaishi wasio Watanzania, je, hilo mtendalo ndio litapoteza legacy ya hayati Magufuli kwa Watanzania?

Hivi tuseme hamuoni mega projects alizoanzisha na zilikwenda kwa kasi ya kutisha,? lakini hivi sasa zinasuasua? Zikikumbwa na ubadhirifu, expenditures cost ziki rise kila uchao?

Nawakumbusha hayati Magufuli aliigusa hii nchi na miradi mikubwa sana ya kimaendeleo karibu kila eneo,mbona hamtaji mradi mkubwa wa maji jijini Arusha?daraja la busisi, flyovers,mastendi ya kisasa,bwawa la umeme,Sgr,viwanja vya ndege vimeboreshwa kila mahala,ujenzi wa meli mpya, kwanini chato iwe nongwa?,,acheni upuuzi

Narudia tena, nchi hii mafisadi hutumia waandish,wahariri i kama tissue papers. Mkae mkijua maisha hubadilika wakati wowote, na umzanie ndiye kumbe sie.

Kazi kwenu wachumia matumbo, kwa sasa endeleeni kunawili, muda ni wa kwenu, ila kumbukeni mnalitumbukiza taifa shimoni kwa kuunyamazia ukweli wa kinachoendelea nchini kwa sasa.

Nawasilisha.
 
Hawa wahariri kwa sasa wanalamba asali haswa chini ya waziri wa habari na utangazaji Nape Nnauye,hakuna mtanzania mwenye akili asiyefahamu jambo hili.
Watu hao wameuza utu wao kwa vipande vya dinali zitokanazo na kodi na tozo mbalimbali za watanzania maskini.



Nawsilisha.
Wamekubali kuwa watumwa kwa senti, wapo kazini, natamani nisikie wakitoka hadharani kutamka wamepata faida kiasi gani kwa huu upuuzi walioufanya
 
Hawa wahariri kwa sasa wanalamba asali haswa chini ya waziri wa habari na utangazaji Nape Nnauye,hakuna mtanzania mwenye akili timamu asiyefahamu jambo hili.

Watu hao wameuza utu wao kwa vipande vya dinali zitokanazo na kodi ,tozo mbalimbali za watanzania maskini.

Kuna mambo ya kifisadi nchi hii yanaendelea , wanayajua lakini kwa kuwa wanalamba asali, wapo kimya imani yao ipo kwa Nape Nnauye, ili awape shavu serikalini ,ikiwemo na ahadi ya ukurugenzi mawasiliano Ikulu, wameamua kufubaza taaluma zao katika kulisaidia taifa.
Umeandika takataka
 
Back
Top Bottom