Nimekugongea thanks mwandishi wa thread na heshima kwa kusimama (standing ovation) kwa Ansbert Ngurumo.
Tatizo ni zaidi ya kauli mbiu. Ebu fikiria hao mawaziri wameteuliwaje kama siyo kishikaji? Halafu kumbuka birds of same feathers flock togather. Wote wote kabisa wana umbumbu wa kiwango kikubwa tu juu ya uendeshaji wa serikali, baya zaidi uwaziri ni fursa pekee ya kujinufaisha kiwadhifa na kimaslahi.
Nikujuvyeni uzoefu wangu serikalini. Rais anapoingia madarakani na anapounda serikali yake muongozo hapa bongo ni yeye anavyotaka au anavyoshauriwa hata na mkewe, hakuna standing instructions zinazombana kuzingatia maslahi ya taifa kwa sababu hazipo kwa katiba ambayo ndiyo mkataba na wananchi. Mtakumbuka Nyerere aliwahi kusema angetaka angekuwa dikteta, alikuwa anamaanisha hicho. Lakini tuangalie anavyotoa majukumu ya utekelezaji (Mandate) kwa kila wizara.
1. Utayarishaji wake siyo makini kwa sababu hayana mwongozo bayana na yanafanywa kwa kulipua.
2. Mikakati yake pamoja na kutokuzingatia majukumu haifuatiliwi na kukubalika kukidhi mahitaji kwa kutoelewa, kwa ulege lege wa serikali au kwa mapungu wa uwezo wa watendaji (Low capacity).
3. Hakuna rasilimali zinazoambatana na majukumu hayo kwa sababu hazipo ila ni kutegemea bajeti ya makusanyo ya kila siku ambayo yanavuja.
4. Hakuna mrejesho unaofuata uwepo wa mfumo wa uthibiti wa kisayansi (Monitoring and Evaluation System)
Kwa hayo yaliyotajwa hapo kila kitu kinafanyika kiholela yaani utendaji wa serikali ni wa zima moto hawa agenda wala taratibu za utendaji.
Tabia inayozungumzwa hapo kwenye hii thread ya kufokea mawaziri na watendaji ni dhahiri shahiri udikteta wa namna fulani unaokubalika na genge zima za utawala. Kwa hiyo ni kweli kabisa ni anguko lililokwisha tokea. Ubaya ni kwamba hawa jamaa hawataki kuambiwa hivyo wala hawaoni tatizo ni nini kwa sababu ulimwengu wanaoishi ni tofauti na tunaoishi wananchi wote.
Chakufanya
1.Katiba MPYA ni lazima
2. Siasa za kitoto zinazoendeshwa nchini ziachwe, kuwe na umakini kwa wananchi kuelewa wanapoiingiza serikali ni kwa mkataba upi wa utekelezaji na si ahadi. Mkataba wa utekelezaji ni wenye sera, mikakati, na mipango ya utekezaji wenye rasilimali watu, pesa, taaluma na maadili yanayopimika kwa muda mfupi, wa kati na muda mrefu. Haya yote yakiwa yametoka kwa wananchi siyo kwa watawala walio out of touch na reality ya maisha ya watu.
3. Vyombo vya serikali vizingatie taaluma na utendaji huru usio na shinikizo la kisiasa. Limesemwa vizuri na Ansbert Ngurumo, anguko la kauli mbiu, anguko la rais, anguko la serikali yake lakini ni anguko la nchi.
Kweli nimefarijika na hii thread inajenga taswira ya JF inayotakiwa.