Ansbert Ngurumo amchana Kikwete live...

Chadema mmezidi chuki sana na Kikwete kubalini yaishe uchaguzi ulishapita jipangeni for 2015 ambapo yeye hatakuwepo kwa kuendelea kumsakama Kikwete na wakati sio Mgombea 2015 ni kupoteza muda na ni ujinga wa kutotambua adui aliyopo mbele yako!
 
Namshauri JK awe anapitia makala za wachambuzi kama za kina Ansbert Ngurumo labda zitamsaidia ku-improve perfomance yake na watendaji wake
 
wakubwa,

Huu ndo uandishi unaojenga nchi, a smart president will observe this well articulated critism,

Watanzania tuache uoga na kuwajaza sifa usalama wa taifa, mbona mnakosa uzalendo na kuwa na nidhamu ya woga,

Lazima tuwalinde kwa gharama zote waandishi ambao ni critics, sio waandishi maslahi
 
Ansbert Ngurumo anaona mbali.... hebu oneni hii makala ya kanjanjai anayeishi kwa "kulamba vidonda" kama inzi. Inahusu the same topic...
Maggid Mjengwa Mei 11 2011
KUNA wakati Mama Maria Nyerere alipata kuulizwa swali la kukera kutoka kwa mwandishi kijana. Mwandishi yule alimwuliza Mama Maria Nyerere: ”Hivi, inakuwaje Mwalimu ameondoka na kuacha familia yake ikiishi katika hali ya kawaida sana bila kuwa na mali nyingi wakati tunaona watendaji wa siku hizi wana mali na wengine wanasomesha watoto wao nje ya nchi?”
Mama Maria Nyerere alimjibu mwandishi Yule: ”Naona wewe bado ni kijana sana, hukuwepo wakati ule wa Azimio la Arusha, lakini hiyo sio sababu ya wewe kushindwa kufahamu ya nyuma; maana ulitakiwa kusoma. Wakati wa Mwalimu kulikuwa na Azimio la Arusha na miiko ya viongozi. Na Mwalimu kama kiongozi asingeweza kufanya tofauti na yale ambayo aliyasimamia na aliwataka wenzake katika uongozi wayafuate”, Alisema Mama Maria Nyerere.
Nimehusisha hapa kauli ya Mama Maria Nyerere maana, msingi wa alichozungumza Rais Kikwete juzi na alichozungumza Mama Maria Nyerere, ni madhara ya kuporomoka kwa Maadili ya Uongozi. Si ni juzi hapa tumemsikia Rais wetu Jakaya Kikwete akitamka;
“I want to hear you guys out there in the field!” Alitamka Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kimombo. Akimaanisha, anataka awasikie watendaji wake wakiwa kwa watu.
Ndio, Kikwete alikuwa akizungumza na watendaji wakuu serikalini kule Dodoma. Ni kwenye semina elekezi. Na hakika, watendaji wale walikuwa wengi ukumbini - mawaziri , manaibu mawaziri, makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu na wengine.
Tafsiri yangu; kwanza kabisa, nimeipenda sana hotuba ya Kikwete ingawa TBC1 hawakuweza kuimalizia kutokana na matatizo ya kiufundi. Nitaitafuta niisome kwa ujumla wake.
Vinginevyo; katika kile nilichokisia, nilimwona Rais aliyekuwa mkali na mwenye kuwashutumu kweli kweli watendaji wake. Katikati ya mistari naziona ishara za Kikwete, katika muda mfupi ujao, kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri na watendaji wa ngazi mbalimbali serikalini. Kwa kufanya hilo kutakuwa na maana kubwa zaidi ya alichokizungumza kwa watendaji wake pale Dodoma na alichotaka kuwaambia Watanzania.
Naam. Rais ‘ aliwasema’ sana watendaji wake, kama nitatumia lugha ya kwenye sebule zetu. Kikwete niliyemwona, pasi na shaka, alikuwa mkweli kwa nafsi yake. Alitoa dukuduku lake la moyoni. Watendaji wale walionekana kuwa kimya wakati mwingi. Kuna ambao waliinamisha vichwa.
Hotuba ya Kikwete ilikuwa na ukweli mwingi juu ya hali halisi. Kikwete alikuwa anazungumzia sehemu ndogo tu ya kero ya wananchi kwa watendaji wao. Bila shaka, mle ukumbini kuna waliotoka wakinung’unika; “ Bwana Mkubwa katuumbua!”
Si tumemsikia, Kikwete amekemea uvivu, ubabe, uasherati na hata umangimeza. Kama kuna alilolisahau Kikwete, basi ni ushirikina, maana, tunajua kuwa baadhi ya watendaji wetu ni mahodari katika kuendekeza ushirikina. Hutokea kuwa wanapokuwa nje ya ofisi zao, basi, wako kwa waganga wa kienyeji wanapiga ramli.
Turudi kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais; “ Kazi ya Waziri si kusoma mafaili tu”, anasema Kikwete na kisha anaongeza: “Tokeni!” Na hilo ndilo neno lililosikika mara kwa mara kwenye hotuba ile. Kikwete alilisitiza sana umuhimu wa watendaji kutoka na kwenda kwa wananchi. “Ni nani kati yenu shughuli zake ziko ofisini tu?” Aliuliza Mkuu wa Nchi. Kama ilivyotarajiwa, hakuna aliyenyoosha kidole.
Kikwete anasema: ” Tubadilike jamani”. Lakini, nilichokiona kwenye sura za wengi wa watendaji wale ni ugumu uliopo wa kubadilika. Inahusu change of mindset; kwa maana ya kubadilika kifikra. Na bila shaka, JK mwenyewe analijua hilo. Swali ni hili; “How can you change from a fixed mindset to a growth one?” – Unawezaje kubadilika kutoka kwenye fikra mgando hadi fikra zinazokua? Naam. Mbwa mzee hafundishwi kukaa, au? Inawezekana kama mbwa mwenyewe akiwa na utayari wa kijifunza.
Watendaji wale baadhi yao wanasumbuliwa na maradhi ya kuendekeza “Ubwana na Umangimeza” . Si ndio, wanapenda sana kujikweza. Wanapenda ‘ ubosi’. Na ndio maana itawawia ugumu kweli waheshimiwa hao kukaa chumba kimoja na vijana maafisa habari wao. Si ni vijana wadogo tu, tena wamemaliza vyuo vikuu juzi tu. Eti bosi mzima ampe maelezo kijana Afisa Habari juu ya habari za Wizara kisha kijana huyo azungumze na umma, waapi bwana?
Kinachohitajika haraka ni mabadiliko ya kifikra kwa baadhi ya watendaji wetu. Kutoka kwenye ukale na kuingia kwenye usasa. Vinginevyo tutabaki pale pale na kauli za; “Mimi si msemaji wa Wizara!”
Lakini, tutakosea pia tukidhani kuwa baadhi ya watendaji wetu wako ‘bize’ sana maofisini wakisoma mafaili; maana kuna ukweli mwingine, ni huu: Baadhi ya watendaji wetu wako ‘bize’ sana kufanya mambo yao binafsi, ndani na nje ya ofisi. Si tunajua kuwa baadhi ya watendaji wetu ni wafanyabiashara na wengine wanaendesha hata viwanda vya uzalishaji?
“Mr. President, they are not out in the fields, but they are at their sites!” Na mie nimejaribu umombo, kumwambia Mheshimiwa Rais kuwa baadhi ya watendaji wake mara nyingi hawako kwa wananchi, bali kwenye maeneo yao ya miradi binafsi. Si huwa tunasikia; “Niko kwenye site yangu bwana!” Na mtendaji akiwa ofisini, atatumia hata simu ya ofisi kuwalekeza kazi watu walio kwenye site yake. Naam. Ana ujenzi unaendelea kwenye site zake na anaufuatilia kwa karibu! Hivi mtendaji kama huyu anaweza kweli kuwa na muda wa kutosha kufuatilia mambo ya wananchi?
Ndio, katika utaratibu wa sasa na hasa baada ya kuondokana na kanuni, miiko na maadili ya uongozi ya enzi za Mwalimu, ni vigumu ukawa na mawaziri na watendaji wengine wasio na miradi ya biashara, mashamba na hata viwanda ambayo wao wenyewe ndo wasimamiaji. Hivi waheshimiwa hawa watapata wapi muda wa kusimamia biashara, mashamba na viwanda vyao kama si kuiba muda wa kuwatumikia wananchi na hata kutumia rasilimali za umma?
Inahusu swali hili: Ni nani atauzima mshumaa wa Serikali? Na hapa kuna kisa nilichopata kusimulia; Naam, miongoni mwa viongozi waliopata kuongoza dola ya Kiislam hususan baada ya Mtume Muhammad (SAW) na baada ya masahaba ni Khalifa Umar bin Abdulaziz. Wanazuoni wa Kiislam wanatwambia kuwa utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ulijaa uadilifu. Si kwa viongozi tu, hata kwa raia wake.
Inasemwa kuwa moja ya mafanikio makubwa ya utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz ni kukusanya zakka. Katika Uislam, zakka ni ibada ya lazima kwa mwenye nacho kuwapa masikini, yatima, wajane, wasafiri, raia na wengineo wenye kuhitaji.
Watu walijengewa imani kubwa kiasi kwamba hakuna aliyethubutu kukwepa kutoa zakka. Hata wale waliopokea zakka walikuwa waadilifu, hawakupokea zakka mara mbili kama walishapokea kabla. Wote waliostahili kupata zakka walipata zakka. Hakika, zakka zilitolewa zikajaa mabohari.
Siku moja raia mmoja alikwenda kwenye ofisi ya Khalifa Umar bin Abdulaziz. Wakati wa maongezi yao, Khalifa Umar alikuwa akihangaika kuupuliza na kuuzima mshumaa mmoja na kuwasha mwingine. Alikuwa na mishumaa miwili mezani. Kadri mazungumzo yalivyoendelea, Umar aliendelea kufanya hivyo. Alipuliza mshumaa mmoja ukazimika, kisha akawasha mwingine.
Jambo hilo lilimstaajabisha sana mgeni wa Khalifa Umar bin Abdulaziz. Akauliza; "Je, ni kwa nini unazima mshumaa huu na kuwasha mwingine, kisha huo nao unauzima na kuwasha ule wa kwanza? Khalifa Umar bin Abdulaziz akamjibu; "Mshumaa huu ni wa Serikali, wewe unaponiuliza habari za Serikali nauwasha. Lakini naona mara unauliza habari za familia yangu, ndio maana nauzima wa Serikali na nauwasha mshumaa wangu mwingine nilioununua kwa pesa za mfukoni mwangu. Nachelea nisije fanya dhuluma kwa mali ya nchi."
Ndugu zangu, bila shaka, hicho ni kisa chenye kutupa mafundisho muhimu juu ya dhana nzima ya Maadili katika Utumishi wa Umma. Tafakari.
 
Kama ni ujinga mi ni namba moja kila nikisoma hapa na kichwa cha habari siambulii chochote kabisa, nimekubali kuitwa mjinga kwa hili, Kwa herini.
 
Mara nyingi nimekuwa nikiuliza watu wanaosema wasaidizi wa raisi ndo wanaomwangusha! Je na maamuzi yake binafsi pia yanauhusiano na wasaidizi pia? angalau sasa tumeanza kupata watu wanaosema mapungufu ya raisi ya wanayasema waziwazi. hongera mwandishi kwa kusema waandishi wa habari wengine walichokifungia macho.
 
Sababu kubwa inayonifanya nisilikose TZ Daima la J'pili ni articles za Ansbert Ngurumo. He is my hero, end of story!!
 
Rais amefanikiwa kuwashawishi baadhi ya watu-hasa wa kawaida. Nilikuwa kwenye daladala namsikiliza kupitia redio wakati anawachana wasaidizi wake, watu wengi walifurahi wakiamini kuwa sasa rais ameanza 'kufanya kazi'.

Wengine tukakumbuka semina za ngurdoto na ziara ya karibuni ktk kila wizara. Tukakumbuka kwamba siku hizi umezuka mtindo wa kufanya kazi kupitia vyombo vya habari (tv+redio). Kila mtu (mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya) anang'aka akiona kamera. Yaani mtu anang'aka kweli mbele ya kamera za tv ili wadanganyika wajue anachapa kazi. Serikali kwa sasa imeshikwa kila kona, nadhani ipo tayari kupata point kwa njia zozote, ili mradi wapumue walau hata kwa sekunde.
 
Ansbert, keep it up. Our county needs brilliant brains like yous to move forward. I have been saying all along that Jk and ccm are total failures. We need to act now!
 
Chadema mmezidi chuki sana na Kikwete kubalini yaishe uchaguzi ulishapita jipangeni for 2015 ambapo yeye hatakuwepo kwa kuendelea kumsakama Kikwete na wakati sio Mgombea 2015 ni kupoteza muda na ni ujinga wa kutotambua adui aliyopo mbele yako!
Napingana na mtazamo wako. Kama kiongozi kukosolewa ni chachu ya kujipanga na kudumu katika kuongoza. Nahisi hata JK akibahatika kuisoma ataichukulia article hii na maoni yaliofuata kama changamoto na sio kuyapuuza kama ulivyochukulia wewe kwa sababu itakua kama hapo kwenye red.
 
Ansbert, keep it up. Our county needs brilliant brains like yous to move forward. I have been saying all along that Jk and ccm are total failures. We need to act now!
 
Chadema mmezidi chuki sana na Kikwete kubalini yaishe uchaguzi ulishapita jipangeni for 2015 ambapo yeye hatakuwepo kwa kuendelea kumsakama Kikwete na wakati sio Mgombea 2015 ni kupoteza muda na ni ujinga wa kutotambua adui aliyopo mbele yako!
Inamaana Kikwete ni adui wa Chadema Kama ulivyoandika!?.
 
this is one of the very few best piece of articles i've read. This guy is great....the way he present his message is superb, entertaining, educative and above all stimulate thinking which 2 me is the most important quality of any written statement leave alone am article. Brilliant mkuu!
 
Back
Top Bottom