Anne Semamba Makinda's Profile!

Kuna uhakikisho wowote kuwa Rostam Azizi na Edward Lowassa wana mkono katika hili kama ilivyodaiwa na baadhi ya magazeti kama Dira?
 
Background yake kifamilia ikoje?

Baba yake mzazi alikuwa Mkuu wa mikoa kadhaa to start with... so it didnt come as sheer luck/kubahatisha kwake kuingia kwenye siasa mapema.Si mnajua tena... watoto huwa na hulka kufuata nyayo za mzazi/wazazi.
Pia kifamilia, nadhani wana undugu ya Jackson Makweta aliywahi kuwa Waziri kwa miaka mingi.
 

Haaa haaa very interesting. katika siasa za Tanzania kuna watu nimewasikia toka nikiwa Primary miaka mingi iliyopita. Ni pamoja na Anna Abdalah, Anna Makinda, Jackson Makweta, Kingunge, Msekwa, Kimiti nk.

Kuna baadhi wameng'atuka wenyewe kwa busara zao.

Thanks. Nice to know the background.
 
sio mume tuu hata kama na hawara zake wapo wadau tunaomba taarifa tuzifanyie kazi kwani yana nafasi katika utendaji wake wakila siku katika nafasi yake ya uspika! sawa?
 
Nimesikia leo amechaguliwa na tayari kaitisha Press Conference na kutangaza viapumbele vyake.

Tukipewa nafasi WANAWAKE TUNAWEZA mwaya.
 
Nakumbuka miaka ya 1990's alirudi jimbo la Njombe kugombea baada ya kuwa katika viti maalum kwa muda mrefu akaambulia kuulizwa kuwa na wananchi wa Njombe"ALIKWINA???" maana yake "ALIKUWA WAPI MUDA WOTE?"
 
Hii ni kwa hisani ya rafiki yangu Kiungani



Sahihisho nadhani huyo Prof wa SUA ni Kapinga (RIP) na si Ndunguru.

Usisahihishe huku ukidhani. Mtoa mada yuko sahihi: ni Professor Bruno Ndunguru aliyekuwa SUA hadi miaka ya 1980
 
Wanyalukolo oyeeeeee!!! Anna vya kunyumba kabisa. siwo Semamba safisha jina lako kwa kuwatumikia zaidi watanzania kuliko baadhi ya watu. Kila la heri mama.
 

Kuna mdau alipost hii:


 


ukiacha ile spreadsheet yako ya matokeo, nakukubali kama dataman...maana kila kitu lazima umwage data. keep it up
 
Nimesikia leo amechaguliwa na tayari kaitisha Press Conference na kutangaza viapumbele vyake.

Tukipewa nafasi WANAWAKE TUNAWEZA mwaya.

mkipewa? msipopewa mnalala doro siyo? haya mmepewa kidole juu, juu tafadhali
 
Wakati wanazaa naye Prof. tayari alikuwa ameoa au bado? Hii itasaidia kujua background yake in Moral Values.

Prof Ndunguru bado yuko hai mzimaaaaa! Tulipokuwa chuoni miaka hiyoooooo ya sabini na ushee inasemekana huyu mama alikuwa mchumba wake, lakini kwa bahati mbaya mambo hayakwenda kama yalivyopangwa. Ila Prof alioa mwanamke mwengine wa kabila moja la Kaskazini mwa Tanzania.

Mimi mwenyewe nilihudhuria hiyo harusi ya Prof na huyo mke wake wa sasa.

Ila mama Makinda ni mchapa kazi na asihukumiwe kwa kosa lililotokea miaka zaidi ya thelathini nyuma. Aangaliwe alivyo hivi sasa kwa maoni yangu ni mtu mwenye heshima yake hana maskandali. Ingekuwa ni mama maskandali basi hapo bungeni pangekuwa moto na wengi wangekwisha jitokeza kujipendekeza.
 
ukiacha ile spreadsheet yako ya matokeo, nakukubali kama dataman...maana kila kitu lazima umwage data. keep it up

Haaa haaa Mkuu, tuko pamoja. Ile sheet ilibidi nilurudi kwa source aliponipa details nili-update.

Mkuu JF hairuhusiwi Kuchakachua.
 
Nakumbuka miaka ya 1990's alirudi jimbo la Njombe kugombea baada ya kuwa katika viti maalum kwa muda mrefu akaambulia kuulizwa kuwa na wananchi wa Njombe"ALIKWINA???" maana yake "ALIKUWA WAPI MUDA WOTE?"

Hivi nimesoma mahali kuwa amekuwa Mbunge miaka 35. Ni nani alikuwa Mbunge wa jimbo alilogombea kabla yake?
 
mkipewa? msipopewa mnalala doro siyo? haya mmepewa kidole juu, juu tafadhali

Mbali na nafasi ya Uspika nadhani yuko katika uongozi zaidi ya miaka 35. natamani moja aniambie footprints zake ziko wapi au ni nini hasa alichofanya cha Watanzania kumkumbuka.

Yes 2008 kuna shule JK alifungua. Sina uhakika kama ni yake au ni ya jina lake tu. Mbali na hilo, kuna nini tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…