Anna Mghwira: Tanzania tunataka Viwanda vya Aina gani kwa Maendeleo ya Taifa letu?

Anna Mghwira

R I P
Mar 9, 2012
206
362
Mjadala wa viwanda na Maendeleo ya Tanzania ni muhimu sana.

Lakini kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:
Tunataka Viwanda gani?

Mwalimu Nyerere alianzisha viwanda vingi. Tuliuza nguo nje. Tuliuza nyuzi, katani, ngano na nafaka zingine, chai, kahawa, nyama, matunda...nk. Viwanda vipo ila vingine vimekufa, vingine vimebinafsishwa.

Viwanda ni muhimu lakini tunataka viwanda gani?
 
Mama Anna Mghwira tunashukuru kwa maoni yako. Mimi ni mmoja kati ya watu tusiokubaliana na mambo mengi ya Sera za CCM chini ya Magufuli.

Lakini wacha tu tuunge mkono hili debe la rais wetu bila kijali ni viwanda vya aina gani ili mradi vitatoa ajira sio mbaya. Tukipoteza muda tusubiri nyie wasomi mpaka mtupeleke kwa mitazamo yenu iliyojaa nadharia tutachemsha. Nyie ni wale wasomi wenye mikakati mizuri isiyo na utekelezaji. Ninadhani ww na usomi wako sidhani kama umewahi kuanzisha mradi uliotoa ajira hata kwa watu mia, sana sana unaweza kukuta una Ngo inayosubiri hela ya wazungu.
 
Mama Anna! Naomba nikuulize swali hivi viwanda bila Elimu bora tutafika?

Nyinyi kama wapinzani mnasaidiaje Elimu ya Tanzania ambayo haipewe kipaumbele kwa maana kwamba serikali imejikita katika kuzalisha wengi lakini bila ubora. Mf wanafunzi wanachaguliwa form one hata kkk hawazijui?
 
Tatizo hata tukipendekeza hamna budget ya kujenga! infact tunataka viwanda vitakavyowezesha sector juu ya Mgongo Wa Umma(Kilimo) kuinuka.

Hii italeta manufaa kwa watanzania wengi Sana, kuanzia wasomi mpaka wakulima.
 
Tunahitaji viwanda vya aina zote
Heavy Industries, medium sized industries and Small industries

Ukishaanza kuplan viwanda vidogo vidogo tu unakuwa unajipoteza ramani.
 
Actually watanzania hatujawahi kuulizwa tunataka nini...ni watu wachache wanakaa huko wanatuamulia then wamatuaminisha kwa maneno matamu na lukuki juu ya kile wanachofikiri tunakitaka.
 
Tuanze na viwanda vidogo vidogo ambavyo baadae vita graduate na kuwa viwanda vikubwa.

Na tunaze na viwanda vinavyo tumia malighafi zetu kwa 100%

Na inapaswa kuwa na aina mbili za sera.
1. Vinwanda vidogo vidogo ambavyo vingi vitakuwa vya wazawa.

2 Viwanda vikubwa vya wawekezaji toka nje ambao hawa pia viwanda vyao kwa namna moja au nyingine vinaweza tumia Output ya viwanda vidogo.

Ni hayo tu
 
Tehteheh! Heshima yako mama. Wenye hiyo slogan wakikujibu kwa ufasaha swali hilo, naomba nitag kisha niandalie kadi ya ACT jina la mwanachama Daniel Zwangendaba.

Tuliposema hii ni "mbiu" kama zile zilizopita za kilimo cha kufa na kupona, siasa ni kilimo, ukweli na uwazi, kilimo kwanza....etc etc tulikuwa tunamaanisha.
 
Mjadala wa viwanda na Maendeleo ya Tanzania ni muhimu sana.

Lakini kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:
Tunataka Viwanda gani?

Mwalimu Nyerere alianzisha viwanda vingi. Tuliuza nguo nje. Tuliuza nyuzi, katani, ngano na nafaka zingine, chai, kahawa, nyama, matunda...nk. Viwanda vipo ila vingine vimekufa, vingine vimebinafsishwa.

Viwanda ni muhimu lakini tunataka viwanda gani?

Kabla ya kuchagua aina ya viwanda ni vema kujua lengo la kuanzisha hivyo viwanda. Dunia ya sasa ni muhimu sana kufanya cost analysis kabla hujafanya lolote. Ndio maana hata wenye technolojia hupeleka viwanda nchi zenye gharama ndogo za uzalishaji ili kubakia "competitive".

Lengo letu kama taifa ni LIPI? kuzalisha ajira,kupunguza gharama za bidhaa tunazouziwa kutoka nje, kupunguza matumizi ya fedha za kigeni au kukuza uwezo wa ndani wa uzalishaji?

Kwa mfano kama lengo ni kukuza ajira, si lazima kuanzisha viwanda vitakavyotuma technolojia za zamani na gharama kubwa za uzalishaji ili tu ujigambe kuwa umeajiri watu 100,000 ambao ufanisi wa wanachozalisha(productivity) bado iko chini ukilinganisha na kama ungewaelekeza kwenye sekta nyengine zenye ufanisi(productivity) iko juu.

Kwa mtazamo wangu huu msukumo wa nchi ya viwanda ni pre-mature. kwa nini tusianze na nchi yenye nishati ya uhakika? mifumo ya umwagiliaji ya uhakika?mifumo ya usambazaji wa kinachozalishwa mashambani na kwengineko ya uhakika?mifumo ya uhifadhi wa tunavyozalisha ya uhakika? so far hii mufumo yote haipo. na kama ipo, iko kwenye hali mbaya, haina uwekezaji wa kueleweka kutoka serikalini wala sekta binafsi kutokana na ukiritimba uliopitiliza.

Ukileta kiwanda kikubwa bila nishati yatatokea ya Dangote, ukiongeza uzalishaji bila kuboresa uhifadhi yatatokea ya nyanya kuoza.

Kutokana na hayo, aina ya viwanda vinavyohitajika Tanzania ni viwanda vitakavyozalisha au kusaidia uwepo wa mifumo imara ya kuongeza productivity. Productivity ya kila mtanzania ikiongezeka labour participation itaongezeka, umasikini utapungua. wote tutafaidika.

Viwanda vya nguo sijui, baiskeli, sijui viatu tuwaachie wenye uwezo wa kuzalisha hizi bidhaa kwa gharama ya chini kutupita. kwa kuwa wana mifumo ya kufanya bei iwe chini. Tukikamilisha mifumo yetu tuanze na hivyo viwanda.

Factories without industries(mfumo thabiti wa ku-support viwanda) ni mazingaombwe.
 
Mama sisi mpaka sasa tunazalisha umeme usiozidi MW 1200 nchi nzima. Juzi hapa tulitembelewa na ndugu zetu wa Ethiopia wao wanazalisha umeme MW 13000 mpaka sasa achilia projects ambazo zipo kwenye pipeline. Kama unavyojua viwanda ni nishati sasa labda tuseme tunataka viwanda vya kutengeneza mikeka na vyungu ambayo havitumii nishati ya kutosha.
 
Kipaumbele kwa Viwanda tukaacha kilimo nyuma is a total failure. Ilitakiwa tupanue kilimo chetu ndipo tufikirie viwanda, rejeeni mapinduzi ya viwanda huko ulaya na Asia kadri siku zinavyokwenda.
 
Mjadala wa viwanda na Maendeleo ya Tanzania ni muhimu sana.

Lakini kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:
Tunataka Viwanda gani?

Mwalimu Nyerere alianzisha viwanda vingi. Tuliuza nguo nje. Tuliuza nyuzi, katani, ngano na nafaka zingine, chai, kahawa, nyama, matunda...nk. Viwanda vipo ila vingine vimekufa, vingine vimebinafsishwa.

Viwanda ni muhimu lakini tunataka viwanda gani?
Siamini Kama ndo Anna Mghirwa amepost hapa, Nahisi account iko hacked .
Ni wewe uligombea urais kwa ticket ya chama ambacho hakikuwa na uwezo wa kushinda na wewe ulilijua hilo, unapohoji viwanda, tukuhoji wewe uliyesema una imani na Magufuli na kisha ukaenda kumpongeza Lumumba.
Nataka tu nikukatishe tamaa kuwa, Tanzania chini ya ccm haiwezi kuendelea hata iweje, nchi imejaa laana ya dhuluma, uonevu na ukatili wa kila aina Kwa raia wake.
Kama miaka 59 ya utawala wa ccm nchi bado inanuka umaskini Kama kinyesi kibichi cha binadamu, umaskini unaochefua na kutapisha eti leo anakuja mtu na kuwalaghai kutakuwa na viwanda ,vitatoka wapi?
Hana strategies za kujenga au kufufua viwanda zaidi ya kuongoza nchi Kwa chuki, dharau na kubomoa na kuharibu hata kidogo alichojenga mwenzake.
Ogopa Sana mtu asiye penda kukosolewa na anayepinga kila kitu alichofanya mtangulizi wake, mtu ambaye ni bora akakaa kimya bila kuongea maana akiongea Kama mtu ana BP lazima afe.
Nyota njema huonekana tangu asubuhi, China,Malaysia Singapore tulikuwa nao kwenye umaskini miaka ya 1960,leo wako wapi?
Tanzania haiwezi kuendelea milele chini ya ccm.
 
Unaanza na viwanda vinavyoweza kumilikiwa na wazalendo. Kwa mfano vya kuongeza thamani mazso yetu ya kuliona na maini yetu. Viwanda kama DANGOTE SI CHETU NI CHA NIGERIA.. HATA ACASIA GROUP SI MGODI WETU NI WA MAREKANI
 
mama kwa kuwa Elimu ni bure tunataka Viwanda vya kufyatua watoto kwa wingi Elimu bure
 
Binafsi nahisi utawala uliyopita na huu uliopo zote zilikosa na imekosa clear VISION. Kama Magufuli alijipambanua kwenye majukwaa kwamba Tanzania yake itakuwa ya viwanda iweje strategies za kuipeleka nchi kwenye mfumo wa viwanda usionekane?

Mwaka wa pili wa utawala wake lakini bado Tanzania ya viwanda haionekani hata kwa mbali ndio kwanza tunafikitia kununua umeme from Ethiopia

Laiti tungekuwa na mpango mkakati mezani unaoeleweka na kutekelezeka nadhani tayari juhudi zingeonekana. Haiwezekani lengo kuu likawa ni viwanda hata kama vitakuwa subsidiary alafu mtu anakimbia B.O.T anachukua pesa na kukimbilia kununua bomberdier

So bado nashawishika kuamini utawala wa sasa bado haujawa na vision inayoeleweka ndio maana itakuwa ngumu kufikia malengo.
 
1. Viwanda vya zana za kilimo
2. Viwanda vya nguo na viatu
3. Viwanda vya vifaa vya ujenzi
4. Viwanda vya kusindika mazao
4. Viwanda vya magari na matrekta
 
Back
Top Bottom