Anna Kilango Malecela na Sefue warejeshwe kazini

Anna Kilango Malecela na Sefue warejeshwe kazini

vijana acheni chuki na ubaguzi .nchi ni wote .wazee, watoto na vijana
 
Kuna mambo machache nayaona yanaweza kupunguza ufanisi serikalin kufuatia viongozi na uteuzi wake:
1. Wingi wa ujio wa watu wapya ambao utawafanya wajifunze kwanza kabla ya kuzoea kazi zao.
2. Utekelezaji wa kazi unaozingatia zaidi maagizo badala ya ubunifu.
3. Wenye madaraka kugeuka kuwa wao ni kila kitu na walio chini yao kutakiwa kuwanyenyekea hata kama wana utaalmu.
na mengine ...
Kuna kakitabu kaliandikwa na Mwalimu Nyerere "TUJISAHIHISHE". Ni vizuri tukajisahihisha hasa katika kuweka safu mpya ya uongozi katika awamu hii ya tano
 
Cheo ni dhamana! Hivi Mleta mada ni Mtz au ndo wanasoma ulaya wanarudi kututawala! bila maadili! Ofisi ya umma u jiulize manake nn! kawaombee kazi ktk Mashirika binafs
 
Si bora hata Sefue hata kama ana miaka 80 kuliko huyu wa vituko vya kumwaibisha bosi wake! Katibu kiongozi gani ambaye ni mkuu wa utumishi serikalini kila siku blunders za aina hii tunaona?
Nina wasiwasi kama ana ujuzi wa kutumia kompyuta,
 
Uzee kitu gani Sefue arudishwe kwani anakuja kupigana miereka au kutumia akili, hao wahandisi sijui walandalasi wanampotosha Rais wetu mpendwa. Sefue atinge mjengoni
 
Siungi mkono hoja ya watumishi wenye umri wa kustaafu kurejeshwa ofisini kwa kuwa wenye uzoefu wapo na wahitimu tunao wengi , lakini pia siungi mkono wale waliothibitika kutoa taarifa za uongo kwa umma kurejeshwa ofisini.
Lakini pia Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu-Msigwa anapaswa kuonyesha weledi wa kazi yake ya kutuhabarisha taarifa za ikulu kwa umakini mkubwa na sio kutia saini kichwakichwa tu kila taarifa inayoenda kwa umma.
Taarifa hizi zenye mkanganyiko wa mtu mmoja kuteuliwa nafasi zaidi ya moja alipaswa kuhoji na baada ya kupewa majibu ya kina ndipo aandae taarifa moja tu kuwa wafuatao ni wakurugenzi na wale ambao majina yamejitokeza mara mbili ni kwamba mheshimiwa rais ameamua kuwabadilishia majukumu.
 
1468048824318.jpg
 
Hivi kweli kazi za hawa watu zimeishia wapi!!? Tuliambiwa watapangiwa kazi nyingine lakini mpaka leo kimya. Au hiyo ndiyo ilikuwa holizontal droping siyo!! Wanakula mshahara wa bure .......... wanakuja ofisini wanapewa magazeti mpaka wawe frustrated waache wenyewe.

List imekuwa kubwa; Malecela, Sifue, Dau, Asha-Rose .....!!!
Wanatafutiwa pressure tu kama sio kiarusi. Kama kabwe.
 
Si bora hata Sefue hata kama ana miaka 80 kuliko huyu wa vituko vya kumwaibisha bosi wake! Katibu kiongozi gani ambaye ni mkuu wa utumishi serikalini kila siku blunders za aina hii tunaona?
Blander gan mkuu!!!?
 
Mimi ni RAIA mwema kwa kuwa Kila mwezi nalipa kodi, pia natekeleza sheria za NCHI ndio maana sijafungwa wala kutiwa kizuizini.

Anna Kilango akiwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliondolewa na bosi wake kwa kile kilichodaiwa alimdanganya kuwa mkoa wa Shinyanga haukuwa na vibarua hewa. Natumia neno vibarua kwa kuwa watumishi NCHI hii ni wachache sana, wengi nikiwemo Mimi ni vibarua wa serikali. Anna alafukuzwa kazi.

Mwezi huu tumeona vituko vingi, MTU mmoja anapangiwa zaidi ya nafasi moja ya uteuzi, ukurugenzi wake , UKUU wa Wilaya wake. Ubunge wake, Ukurugenzi wake,Ukatibu tawala wa Wilaya wake ukurugenzi wa manispaa wake. Hawa wasingerushwa hewani watu wakapiga kelele ndio watumishi hewa ambao serikali imewaandaa kwa mbwembwe.

Ombeni Sefue licha ya kuonekana kuwa na umri mkubwa (above 60 years age), alikuwa makini kuliko huyu mhandisi wa sasahivi, pia Idara ya habari na mawasiliano ya Ikulu iangaliwe vema, Msigwa kama ametimiza vigezo athibitishwe awe mkurugenzi kamili sio kukaimu Kila uchao, anakosa molari ya kazi na ufanisi pia.

Najua NCHI hii kama wewe sio Kada wa CCM, PROF, DR,MHANDISI huwezi kisikilizwa hoja zako. Walio karibu na Rais wampe haya huenda akachambua Hata moja likamsaidia.
Huwezi kumlazimisha Rais,umeona mkataba wa Msigwa au unaandika kwa mazoea
Msigwa hajafikia unguli wa Akina salva Rweyemamu na Premmy kibanga,kiasi cha kupewa ukurugenzi,kwa hiyo acheni apikwe kwanza akiwiva atapewa tu
 
Hayo makosa yanajirudia sana lkn nimesikia mkuu anasoma sana taarifa anazopelekewa kabla hajazifanyia maamuzi, sijui hili la uteuzi chenga anapigwa wapi.
 
Watapangiwakazi nyingine kiherehere cha nn

Washakuliliaa njaa mapema
 
Ukiendekeza ya.mstaafu lazima ukalie.msumari
 
Tanzania tanzaniaa, nakupenda kwa moyo woteee,
Nchi yangu ya ajabu, jina lako ni tamu sanaaaaa,
Nilalapo nakuota wewee, niamkapo ni shwari kabisaaaa,
Tanzania tanzaniaa, .....................................................
 
Anne kasharudishwa,tena sasa kapewa nafasi nyeti zaidi...tusubiri mangine.SIJAKOSEA
 
Back
Top Bottom