Anna Kilango Malecela na Sefue warejeshwe kazini

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Mimi ni RAIA mwema kwa kuwa Kila mwezi nalipa kodi, pia natekeleza sheria za NCHI ndio maana sijafungwa wala kutiwa kizuizini.

Anna Kilango akiwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliondolewa na bosi wake kwa kile kilichodaiwa alimdanganya kuwa mkoa wa Shinyanga haukuwa na vibarua hewa. Natumia neno vibarua kwa kuwa watumishi NCHI hii ni wachache sana, wengi nikiwemo Mimi ni vibarua wa serikali. Anna alafukuzwa kazi.

Mwezi huu tumeona vituko vingi, MTU mmoja anapangiwa zaidi ya nafasi moja ya uteuzi, ukurugenzi wake , UKUU wa Wilaya wake. Ubunge wake, Ukurugenzi wake,Ukatibu tawala wa Wilaya wake ukurugenzi wa manispaa wake. Hawa wasingerushwa hewani watu wakapiga kelele ndio watumishi hewa ambao serikali imewaandaa kwa mbwembwe.

Ombeni Sefue licha ya kuonekana kuwa na umri mkubwa (above 60 years age), alikuwa makini kuliko huyu mhandisi wa sasahivi, pia Idara ya habari na mawasiliano ya Ikulu iangaliwe vema, Msigwa kama ametimiza vigezo athibitishwe awe mkurugenzi kamili sio kukaimu Kila uchao, anakosa molari ya kazi na ufanisi pia.

Najua NCHI hii kama wewe sio Kada wa CCM, PROF, DR,MHANDISI huwezi kisikilizwa hoja zako. Walio karibu na Rais wampe haya huenda akachambua Hata moja likamsaidia.
 
Mimi ni RAIA mwema kwa kuwa Kila mwezi nalipa kodi, pia natekeleza sheria za NCHI ndio maana sijafungwa wala kutiwa kizuizini.

Anna Kilango akiwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliondolewa na bosi wake kwa kile kilichodaiwa alimdanganya kuwa mkoa wa Shinyanga haukuwa na vibarua hewa. Natumia neno vibarua kwa kuwa watumishi NCHI hii ni wachache sana, wengi nikiwemo Mimi ni vibarua wa serikali. Anna alafukuzwa kazi.

Mwezi huu tumeona vituko vingi, MTU mmoja anapangiwa zaidi ya nafasi moja ya uteuzi, ukurugenzi wake , UKUU wa Wilaya wake. Ubunge wake, Ukurugenzi wake,Ukatibu tawala wa Wilaya wake ukurugenzi wa manispaa wake. Hawa wasingerushwa hewani watu wakapiga kelele ndio watumishi hewa ambao serikali imewaandaa kwa mbwembwe.

Ombeni Sefue licha ya kuonekana kuwa na umkubwa alikuwa makini kuliko huyu mhandisi wa sasahivi, pia Idara ya habari na mawasiliano ya Ikulu iangaliwe vema, Msigwa kama ametimiza vigezo athibitishwe awe mkurugenzi kamili sio kukaimu Kila uchao, anakosa molari ya kazi na ufanisi pia.

Najua NCHI hii kama wewe sio Kada wa CCM, PROF, DR,MHANDISI huwezi kisikilizwa hoja zako. Walio karibu na Rais wampe haya huenda akachambua Hata moja likamsaidia.

Unapigania watu walio na miaka 60+ warudishwe kazini? Wewe utakuwa siyo mzima!
 
Mkuu mtoa mada naomba nikuulize swali vp wewe ukiwa kazini alafu uondolewe wawekwe wao vp uko tayari??
 
Huyu angeanza mwemyewe kujitumbua haya makosa yanajirudia sana ni aibu tuna usalama wataifa tuna washauri lkn empty hayo ndo ya hovyoo anayoyasema raisi kila kuchwapo
 
Mkuu mtoa mada naomba nikuulize swali vp wewe ukiwa kazini alafu uondolewe wawekwe wao vp uko tayari??

Inashangaza! hivi nani huko Ikulu ambaye anafanya makosa ya kitoto namna hii? Mbona Rais wetu yuko makini lakini kuna watu wanafanya makosa yanayodhalilisha taasisi yake ya urais?? ni kweli kwamba mtu anaweza kuteuliwa katika nafasi tatu tofauti kwa interval ya wiki moja?? Nothing personal, lakini huyu Msigwa ajitazame kama hiyo nafasi inamwenea. Kazi yake si kusaini na kupeleka uteuzi katika vyombo vya habari. Labda kama hajafundishwa nini maana ya kusaini document!
 
Hivi tatizo ni ugumu wa kuelewa au vijana hamsomi magazeti na mitandao? Ajira zote zimesimamishwa kwa muda wa miezi miwili wakati uhakiki unafanyika wa watumishi wa umma. Sasa hao watu wako watarudishwa kwa mlango upi wakati mlango mkuu umefungwa?
 
Hawa wote ilielezwa kuwa watapangiwa kazi nyingine.
Unajuaje kama hawajapangiwa?
Au kila uteuzi ni lazima utangazwe?
 
Hivi kweli kazi za hawa watu zimeishia wapi!!? Tuliambiwa watapangiwa kazi nyingine lakini mpaka leo kimya. Au hiyo ndiyo ilikuwa holizontal droping siyo!! Wanakula mshahara wa bure .......... wanakuja ofisini wanapewa magazeti mpaka wawe frustrated waache wenyewe.

List imekuwa kubwa; Malecela, Sifue, Dau, Asha-Rose .....!!!
 
Kukosea huku si bure kutakuwa na vitwanga vingi pale house nyeupe. Yaani watu kabla ya kutoa press release wanapiga vitwanga vya kutosha. Mmmh ni mwendo wa vitwanga tu kwani si vinachangia economy bwana. Natania tu so nisitafutwe coz sina 7m
 
Hivi tatizo ni ugumu wa kuelewa au vijana hamsomi magazeti na mitandao? Ajira zote zimesimamishwa kwa muda wa miezi miwili wakati uhakiki unafanyika wa watumishi wa umma. Sasa hao watu wako watarudishwa kwa mlango upi wakati mlango mkuu umefungwa?

Ulukolokwitanga,
Hivi hawa wanaotangazwa kwa mbwembwe na bashasha na kwa kurudiwarudiwa majina kwa cheo hicho hicho au vyeo tofauti katika sehemu tofauti tunaziita ni ajira au uteuzi? u-DC,u-DED, u-DAS/RAS siyo ajira? Unaposema umesimamisha ajira na huku unaendelea kutangaza majina ya watu kujaza nafasi hizo hiyo siyo ajira?? Nauliza tu!!
 
Ina maana serikali hawana mfumo wa komputa wa kucompile utumishi wao kwa ujumla ndio maana wanabugi step kwa kurundikiana vyeo kwa mtu mmoja. Ila kama wangekuwa na mfumo dhabiti ungekuwa unawaonyesha kuwa huyo mnayempa ukurugenzi ni mkuu wa wilaya tayari or otherwise. Yaani kifupi mfumo huo wa database ungecheki kujirudia rudia kwa data (Data redundancy) hivyo primary key ingekuwa jina. Hivyo unapoingiza jina la mtu unayetakakumteua ingekuwa inakujulisha kuwa huyu ni muajiriwa au mteuliwa kwenye nafasi fulani hivyo unaachana naye.
 
Back
Top Bottom