Anna Kilango atiwa mbaroni kwa tuhuma za kutoa rushwa

Anna Kilango atiwa mbaroni kwa tuhuma za kutoa rushwa

Shobi

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
3,401
Reaction score
4,391
Mbunge wa CCM Same Mashariki Anna Kilango inadaiwa alikamatwa na polisi jana usiku majira ya saa 5 usiku katika eneo la Dimbwi kijijini cha Bagamoyo, kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa wapiga kura. Mtoa taarifa wetu alisema kuwa Anna alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Gonja.

Vile vile mpambe wa Anna aliyejulikana kwa jina moja la Nuru juzi alimvamia dereva wa mgombea mmoja na kumpiga kwa kumtuhumu kuwa na bahasha za kuwagawia wapigakura, Nuru nae alikamatwa na kuwekwa ndani hata hivyo yuko nje kwa dhamana.


Baada ya kuenea kwa taarifa hizo, JamiiForums ilimtafuta Mbunge huyo ili pamoja na mambo mengine aweze kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, juhudi hizo hazikuzaa matunda.

Simu yake ya mkononi ilipokelewa na mwanamke mmoja (Hakujitambulisha) ambaye mara baada tu ya kupokea bila hata mwandishi wetu kujitambulisha kuwa yeye ninani mwanamke huyo alisikika akisema "umekosea namba" na kisha kukata simu.

Juhudi za kumtafuta Mbunge huyo wa Same Magharibu (CCM) bado zinaendelea.
 
Huwezi tenganisha Ccm na rushwa. Ni sawa na uji na mgonjwa. Ondokeni tunahitaji Taifa lenye maadili
 
siku zote ccm wameamini kwamba rushwa ndio njia pekee ya kupata nafasi mbalimbali sasa hali hiyo imeanza kuwala wao wenyewe mwaka huu cha moto watakiona kwani wanaposhutumiana wanatengeneza uadui wao kwa wao
 
hawa watu wapumbavu sana,utaendaje kutoa rushwa wrewe mwenyewe personal,like an idiot?.
sijui kwanini hawamwigi lowasa,kama unataka kutoa rushwa tumia wapambe daaaamn....

Wewe alikutumia wapambe? au ndio mnamchafua mtu ili mpate vyeo..!!
 
Mwaka huu bundi kaingia CCM, kila sehemu ni vurumai,huku rushwa,kule kupigana ,hapa kurogana......laana ya watz inawatafuna!
 
Back
Top Bottom