Anguko la Upinzani nani alaumiwe?

Anguko la Upinzani nani alaumiwe?

Je kuanguka na kupoteza ushawishi kwa vyama vya upinzani nani alaumiwe?

Tukizungumzia Upinzani kwa miaka 15 mfululizo tunawazungumzia chadema

Hawa ndio walikuwa wanawavuruta wenzao

Lakini toka awamu ya tano iingie madarakani ni km wameishiwa pumzi kwa lugha ya mtaani tunasema wamekuwa kama mbwa mwenye mapengo hata wakibweka sauti inarudi tumboni

Je walikosea wapi mpaka kupoteza ushawishi? Je nini kifanyike waweze kuaminika tena?

Je wanaweza wakapotea kabisa 2020 na TLP kikaibuka kama chama kikuu cha upinzani?

Tuwashauri Wapinzani walijikwaa wapi? Ili waweze kwenda sawa na mchapa Kazi Rais Magufuli
Hivi upinzani umeanguka au umeminywa mbavu?
 
Mzee Mkapa kwenye kitabu chake amekiri kuwa upinzani umeimarika Ile chama chetu ccm ndivyo kinachotuharibia siasa kwani haitaki mijadala ya kushindanisha hoja. Ndiyo maana tangu 1995 haujakuwepo tena mjadala wa wagombea urais! Mzee Mkapa ni mfia ccm; hivyo ujue mpaka anaamua kukosoa chama chake kiasi hivyo maana yake uzalendo umemshinda.
 
Back
Top Bottom