Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
Nimefatilia sana aina ya siasa za upinzani ktk kipindi hiki cha awamu ya tano kwa kweli usipokaa chini na kutafakari unaweza amini kama kweli hawa watu wanaonewa. Nasema hivi kwa sbb msingi wa uwajibikaji na kufuata sheria za Nchi unafuatwa nukta hadi nukta. Aina ya siasa za mazoea zinazofanywa na hawa jamaa ndizo hizo zinazowasumbua kiasi cha kuona kwamba hawatendewi haki wanaminywa kila kona lakn hapana.
Sakata la Lissu ni moja ya matukio ambayo yaliikumba Nchi ktk nyakati tofauti na maeneo tofauti. Nikisema hivyo unajua nn namaanisha. Tulishuhudia mauaji ya raia na askari kule kibiti wilayani mkuranga mkoani Pwani, Tulishuhudia yule mzungu aliyeuawa masaki aliyekuwa akishughurika na ujangili wa tembo wetu, Tulishuhudia shambulio la mwanajeshi mstaafu akiwa ktk gari yake getini, nk. Lkn mpaka leo hakuna aliyehoji nn mwendelezo wa haya matukio wote hoja imehamia kwa Lissu. Sifurahishwi na tukio hili bali nahuzunishwa kulibeba hili tukio kama ajenda ya kisiasa na kuanza kuwapaka matope viongozi wa Nchi kana kwamba Nchi hii kila raia kapewa askari wa kumlinda. Muhalifu ana mbinu nyingi sana za kupoteza ushahidi hasa pale anapotaka kufanya uhalifu cha kwanza ni kusoma mazingira na kutafuta mbinu zitakazomfanya afanye tukio lake kirahisi na asijulikane na hasa maeneo ambayo anajua kuwa kumeimarishwa ulinzi. Hivyo bado nitabaki kupinga vikali shutuma dhidi ya Serikali juu ya shambulio hili na kinachotakiwa ni kutoa ushirikiano pale ambapo vyombo vya kiupelelezi vinafanya kazi yake jambo ambalo halipo na hawalitaki hata kulisikia.
Hoja ya pili ninayoona inazungumziwa hapa ni kwa nn Lissu hajatibiwa na Serikali kama wabunge wengine?
Kila kitu kina sheria zake na taratibu zake ambazo hujiwekea. Na kama unaenda kinyume na utaratibu huo hakuna wa kumlaumu. Hakuna asiyejua kuwa ili mbunge akatibiwe nje ya Nchi kunahitajika kibali maalumu kutoka juu ikiwa mamlaka ya kitabibu imethibitisha kuwa mgonjwa ana ulazima wa kwenda kumtibiaa Nje ya Nchi. Na sehemu yenye mamlaka hayo ni Hospital ya Taifa Muhimbili. Tujiulize je Lissu alipewa kibali kutoka wapi kwenda nje ya Nchi kutibiwa? Hospital ya Dodoma ilikuwa na mamlaka ya kumsafirisha Lissu kwenda Kenya? Huduma aliyoipata Lissu Kenya hospital yetu Muhimbili wasingeiweza? Unapojiamulia jambo kwa utashi wako ina maana si unajiweza! Sasa hapo lawama zinatoka wapi? Rufaa ya kwenda Ubeligiji ilitoka wapi? Kuna utaratibu wwt uliotumika hata alipopata nafuu kiasi alipokuwa Kenya? Hoja yao ni kwa sbb ya usalama wake kwa sbb walishahukumu kuwa akiletwa Muhimbili watesi wake ambao ni viongozi wa Nchi hii itakuwa rahisi kutimiza azma yao. Leo hii lawama kibao serikali imesusa kumtibia lkn mliangalia wapi mlipojikwaa?
Hoja ya 3 ni kwamba hakuna kauli yyt kutoka kwa Mh. Rais kulaani juu ya tukio hili.
Nasema si kweli. Baada ya taarifa kusambaa tuliona Mh. Rais akitweet kwenye ukurasa wake wa tweeter kulaani tukio hili na kuviomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua na kuwakamata waliohusika na tukio hili. Lkn ajabu kwa hili wanakwambia sio official haya ni maajabu sana ikiwa mambo mengi mnamfataga hukohuko tweeter kujua leo Rais kasema nn. Huku mitandao hii hii ya kijamii ndipo tunapopata updates za kila siku mapema na ndio njia rahisi kwa sasa watu kujua kila jambo. Lkn kwa hili imeonekana halina nguvu. Sijui walitaka Rais asimame kwenye tv na kutangaza siku 3 za maombezi hata sielewi.
Hoja ya 4 eti Wabunge walikatazwa kwenda kumuona akiwa Nairobi hospital hivi wabunge na Makamu wa Rais nani mwenye ushawishi mkubwa au nafasi ya juu zaidi serikalini? Tena Mama Samia Suluhu alipokwenda na salamu za Mh. Rais alizipokea lkn baada ya kutoka kamkana tena kwa kuita na waandishi wa habari akiwa hsptl.
Sasa hivi kuna jipya mitandaoni baada ya kauli ya spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kutamka kusimamishia mshahara wake na stahiki nyingine kwa hoja kwamba ni mtoro. Wengi wameponda hili na kubeza huku wakionyesha kutokukubaliana na kauli hii lkn bila ya kutafakari kwa kina nini msingi wa kauli hii.
Hakuna mwenye chuki na mtu eti kisa mpinzani hali ya kuwa Nchi hii ni yetu sote. Lkn tujiulize Tundu Lissu ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ina maana kwamba ni Muajiriwa wa Bunge. Bunge linajua kuwa Mbunge wake ana ruhusa ya ugonjwa kutokana na matatizo yaliyompata. Lkn Bunge hilohilo bado linamlipa mshahara na stahiki nyingine kama Mbunge kwa kuwa ni haki yake. Zaidi ya ruhusa ya ugonjwa hakuna taarifa nyingine ambazo muajiri anazijua juu ya muajiriwa wake. Lkn inapotokea sasa huyu muajiriwa akiwa anafanya shughuli nyingine tofauti na kile kilichompeleka mojakwamoja anahesabiwa huyu mtu mtoro. Nani aliyemtuma kuzunguka Nchi nyingine kufanya mahojiano, vikao, na mikutano? Kwa ruhusa ipi kutoka kwa mwajiri wake? Hivi hiyo ni moja ya tiba ambayo daktari alimwandikia kwamba ili upone kabisa inabidi uzunguke Nchi za Magharibi ukaishutumu Nchi yako na serikali? Tuacheni ushabiki kwenye mambo serious kama haya.
Narudia kusema tena kuwa sheria inapopata wa kuifatilia nukta hadi nukta lazima mayowe utayasikia tu. Kwa hiyo hizi hoja za wapinzani zinazotrend kila kukicha ni kwa sbb ya kuishi kimazoea.