Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Good People

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2016
Posts
938
Reaction score
1,819
Bank kubwa Tanzania CRDB bank imepata hasara ya Sh Billion 2 katika hesabu zake za robo mwaka (Quarterly Financial Statements) Suala limenistua sana baada ya kuona Twiga Bancorc ilikua insolvent/ ilifilisika hivi karibuni.

Wajuzi wa mambo naomba mtujuze hii private bank (CRDB) wame conceal profit to avoid Tax liability au kweli wame incur loss naomba TRA walifatilie hili huenda CRDB wame conceal profit for the quarter

Taarifa za fedha zinaonesha kuwa mikopo mingi haijalipwa (underperforming Loans) lakini pia CRDB walikua wana accumulated tax/deni la kodi la muda mrefu.

Mwaka 2015 in 3rd quarter kama hii walipata faida ya Sh. 37.9 Billion after statutory deduction/Tax and Interests!

Banking and Financial Institution Act ya (2006) Section 32(3) inazitaka Taasisi hizo kuandaa taarifa za fedha.

Waliosoma Uhasibu kidogo mnaweza mkapitia Financial Statements (Balance sheet na Statement of Income Statement)

1477867840170.jpg


Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

 
Good People,

Hamna namna hizo financial statements ukazi-screenshot into two docs kisha ukazi-attach independently?! Hivyo ilivyo, sie tunaopenda kutumia reference tunashindwa kwavile haionekani vizuri hasa juu! So, if posible, ningeshauri doc ya kwanza iishie kwenye SELECTED FINANCIAL CONDITION INDICATORS na doc ya pili ianzie kwenye STATEMENT OF COMPREHENSIV INCOME FOR THE PERIOD ENDED 30TH SEPTEMBER, 2016. Nadhani ukiweka kwa hiyo staili, zinaweza kusomeka vizuri... nimecheki kwenye tovuti yao lakini bado hawajaweka!
upload_2016-10-30_22-31-52.png


upload_2016-10-30_22-33-3.png


Nimezitoa website ya CRDB, acha kamba.
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
 
Ningelijua ningelianza kutiririka, ila juzi member humu alisema Tanzania huenda ikaingia kwenye recession, kama sio depression kabisa.
Basi nimekufananisha maana ID hii tumewahi jadili nayo mambo haya kwa kina sana!!

Anyway uchumi wetu unayumba kutokana na govt kupunguza sana matumizi coz chumi changa kama zetu zinahitaji sana kuwa boosted na govt expenditure kama serikali haitumii basi mzunguko unadorora na kuziathiri pia benki...

Nimemsikia Magufuli akijisifu kuwapa kazi nyingi TBA za serikali hii pia inaua uchumi coz TBA ni serikali so serikali inazungusha pesa mfukoni kwake badala ya kuwapa kazi makampuni watakaolipa kodi na kuajiri vijana wengi zaidi!

Hii ya CRDB kutoka kupata faida ya 30 billion mpaka hasara ya 2 billion ni msiba!! Hii si figisu ni kitu dhahiri kwani benki zote transactions zake pamoja na mitiririko yote ya fedha zao zipo monitored na BoT ni vigumu kudanganya!!

Jambo lingine lilichangia kuanguka huku ni hofu za wateja dhidi ya serikali!! Serikali ya JPM imeonesha dhahiri kutotabirika!! Hakuna mwekezaji au tajiri yeyote anayeweza wekeza pesa zake kusikotabirika!! So wengi waliondoa fedha zao benki ili kuondokana na hofu dhidi ya serikali isiyotabirika so benki zinakosa amana na mitaji....

Kingine ni madeni yasiyolipika kama vile mikopo ya watumishi hewa.... madeni ya biashara zilizoanguka kama hoteli n.k n.k

Katika ishu JPM anahitaji kuwa serious ni uchumi!! Hayo mengine anayohangaika nayo yatampotezea muda tu huku nchi ikielekea ilipo Zimbabwe... ni suala la muda tu utatuambia!!

CC Kobello Pohamba Richard
 
Kwa miaka mingi CRDB ilikuwa ikifanya biashara na serikali na hivyo kuwa na fedha za kiinimacho kwamba inafanya biashara safi na faida inapatikana kila mwaka.

Na hata kupanua shughuli zake hadi Burundi ni katika kuufahamisha umma kwamba ni benki inayoweza kuaminiwa.

Lakini nyuma ya pazia kulikuwa na ubadhirifu mkubwa na ufisadi kati ya wafanyakazi wa CRDB pamoja na wale watumishi waso waaminifu wa serikali.

Walichokuwa wakifanya ni kucheza na zile amana za serikali na pia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakitumika kuidhinisha mikopo hewa ya hadi milioni 300 ilhali thamani halisi ya mkopo au nyumba ni milioni 100-150

Hapo ndipo utaalam wa Dr Charles Kimei ambae ni mchumi wa kuaminiwa kupewa vyombo vya Fedha , unapoleta mashaka makubwa.
 
Basi nimekufananisha maana ID hii tumewahi jadili nayo mambo haya kwa kina sana!!

Anyway uchumi wetu unayumba kutokana na govt kupunguza sana matumizi coz chumi changa kama zetu zinahitaji sana kuwa boosted na govt expenditure kama serikali haitumii basi mzunguko unadorora na kuziathiri pia benki...

Nimemsikia Magufuli akijisifu kuwapa kazi nyingi TBA za serikali hii pia inaua uchumi coz TBA ni serikali so serikali inazungusha pesa mfukoni kwake badala ya kuwapa kazi makampuni watakaolipa kodi na kuajiri vijana wengi zaidi!

Hii ya CRDB kutoka kupata faida ya 30 billion mpaka hasara ya 2 billion ni msiba!! Hii si figisu ni kitu dhahiri kwani benki zote transactions zake pamoja na mitiririko yote ya fedha zao zipo monitored na BoT ni vigumu kudanganya!!

Jambo lingine lilichangia kuanguka huku ni hofu za wateja dhidi ya serikali!! Serikali ya JPM imeonesha dhahiri kutotabirika!! Hakuna mwekezaji au tajiri yeyote anayeweza wekeza pesa zake kusikotabirika!! So wengi waliondoa fedha zao benki ili kuondokana na hofu dhidi ya serikali isiyotabirika so benki zinakosa amana na mitaji....

Kingine ni madeni yasiyolipika kama vile mikopo ya watumishi hewa.... madeni ya biashara zilizoanguka kama hoteli n.k n.k

Katika ishu JPM anahitaji kuwa serious ni uchumi!! Hayo mengine anayohangaika nayo yatampotezea muda tu huku nchi ikielekea ilipo Zimbabwe... ni suala la muda tu utatuambia!!

CC Kobello Pohamba Richard

Mkuu Lusungo, serikali inayo fedha na kuanzia mwakani itaiambia BOT iingize fedha kwenye mzunguko.

Lakini ni lazima serikali ibane matumizi ili kuwe na uwiano na mapato na matumizi.

Hili la hizi benki tumelijadili sana hapa JF na sasa umefika wakati wake kwamba ni zile benki halisi ndizo zitaweza kusalimika lakini zile za binafsi haziwezi kusalimika kwani pia zilikuwa zikitumika kutorosha fedha nje ya nchi na ufisadi mwingine.

Kuhusu watu kuficha fedha kwa hofu ya serikali hii kutotabirika hio nadhani ni hofu tu ila wapo watu ambao walitorosha fedha kwa kuhofia kuulizwa wamezipataje.

Ila bado wapo wafanyabiashara wana fedha zao kwenye mabenki na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Lakini serikali ikianza kuongeza fedha kwenye mzunguko baada ya mipango yake yote kukamilika ambayo inafanya sasa hivi na BOT, basi hali itakuwa shwari.

Mkuu, mambo ambayo yalikuwa yakitendeka hapa nchini ni mambo ya hatari sana kuhusu uchumi wetu yaani haukuwa uchumi wa Tanzania, ulikuwa ni uchumi wa kigeni ulotawaliwa na dola na shilingi yetu ilifika hadi tshs 3800 kwa GBP 1! Yaani ilikuwa ikielekea Tshs 4,000!

Sasa hivi utashangaa ukiingia Azania Bancorp unaona tellers wako na kazi zingine lakini BOT staff wapo nyuma ya counters wanashughulikia masuala muhimu.
 
Kama wamepata hasara wanawaambia share holders hiyo hasara imetokana na nini? Bank zote zilikuwa zinafanya biashara na pesa za watu (mashirika ya umma nk.) Wacha waisome number wafanye shughuli za ki-bank sio kukaa na kungoja baraka ya kuwaibia walipa kodi. They need to change how they operate.
Pia kwa miaka na miaka "fat cats" wa CRDB wamekuwa kwenye safety zone kwa muda mrefu, marupurupu na mishahara ya kufa mtu, no accountability, sasa ndio tuwaone, kujifanya wako fresh kwa hela za watu, kama kweli wanaijua kazi yao tuone watakavyo "restructure"
 
Kuondoka kwa hela za serikari akuwezi kuwa na immediate impact wala madeni ya serikari ayawezi affect hasara za benki in short space of time. Serikari azikopi millioni 100 za kujenga nyumba na wala bond ailipwi in a month time kwa hivyo impact ya serikari kutumia hela zake aziwezi onekana leo kwa sababu bado wanazilipa mabenki hela nyingi tu.

CRDB walishatoa statement ya kuzorota kwa sector kadhaa, risks zilizopo kwenye sector kadhaa kuzikopesha na risks za default ya mikopo yao kutokana na hali ya uchumi; kutokana na sababu hizo wakasema wanafanya assessment kwanza kuangalia perfomances ya mikopo na hali ya uchumi na ukienda BoT kuangalia monthly indicators utaona slow down in other sectors za uchumi.

Thats enough kukwambia hasara ziko njiani, serikari inahitaji kuja na stimulus policies (wameanza na ujenzi) alikadhalika na benki nao inabidi kuanza kuelewa interests zao sio uhalisia kwa uchumi wa Tanzania bila ya pesa ya ufisadi every one has to change.
 
Sh bilioni 2 si just under US $1 million?

Right?

Hizi ndizo hela za kuangusha benki?

Hiyo si deposit ya mtu mmoja tu benki?

Kama hizi figures ni kweli kwa benki kubwa kama CRDB, basi hali ya uchumi Tanzania ni mbaya kuliko nilivyokuwa nafikiri.

Mbaya sana tu.

Mpaka Magufuli ataisoma namba.
 
Karibu 5 trilioni imeondolewa kwenye mzunguko wa pesa nchini imelala pale BoT idle tu haifanyi kazi yoyote ile! wakati hii pesa ingekuwa kwenye mabenki ya biashara ingekuwa inazunguka kwa namna mbali mbali ikiwemo mikopo n.k. Hivyo benki za biashara zinafaidika na nchi pia inafaidika kwani watu wanakopa pesa wanafanya mambo mbali mbali ikiwemo kuinvest kwenye biashara mbali mbali, kufanya ujenzi etc. Wewe Rais hujui lolote kuhusu uchumi una washauri wa mambo ya uchumi lakini unakurupuka na kuondoa 5 trilioni shillings kwenye mzunguko wa pesa nchini.

Hapa kazi tu! Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu. Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession! Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
 
Tunajenga Tanzania moja lakini serikali inagombania fito,eti inasema benki zilikuwa zinatumia fedha za serikali kukopesha wananchi na kupata faida.

Ebbo!!, sasa na bakhresa,mengi,mohamed dewji na matajiri wengine wanaoweka fedha benki nao wazitoe kwa hoja kwamba benki huwa wanatumia hela zao kukopesha?

je wakishakopesha, serikali ikienda kuangalia balansi,au ikienda kuzichukua huwa inaambiwa "fedha zenu hazipo,tumezikopesha"....si huwa wanazikuta!!tena zikiwa na riba!!

je wanaokopa ni akina nani? si hawa akina hawa,asha,mwajuma,abdallah,masanja.....watanzania wenzetu ili wakaanzishe biashara zao ndogo ndogo wajikomboe na umasikini!,

sasa serikali imeona hawa watanzania.wanakopa fedha benki wanazifaidi(na inaamini eti zinazokopwa ni za serikali tu),ikaamua izitoe,sasa inamkomoa nani? inazikomoa benki au wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao sasa hawapati mikopo na wanalia hali ngumu!

halafu unapokusanya pesa na kwenda "kuzificha" benki kuu unazuia mzunguko,benki kuu itayahifadhi malundo kwa malundo ya pesa tu,haiwezi kwenda tandale kumkopesha mama ntilie,haiwezi kwenda mtaa wa kongo kumkopesha mjasiliamali,

kwa maana nyingine,"unakomba"hela zoote za nchi,"unazificha,halafu unataka watu wafanyeje? manake huku ni kuficha hela.

kingine,hiyo CRDB ni benki ya nani?si ni benki ya mtanzania? kama kwa.miaka zaidi ya 20wameonyesha uaminifu kwa kutopoteza hata senti ya umma iliyohifadhiwa pale,kwa nini wewe ukae mwezi tu serikalini eti uwazidi akili mwinyi,mkapa na kikwete!!

tunagombania fito,na kwa kuwa tunagombania fito,hakika nyumba haitaisha,ukishika fito unanyanganywa,na mimk ukishika fito nakunyanganya......tutagombana weee mwishowe akija aliyetupa kazi (mtanzania)kutaka akabidhiwe nyumba,tutakoma 2020
 
Sh bilioni 2 si just under US $1 million?

Right?

Hizi ndizo hela za kuangusha benki?


Hiyo si deposit ya mtu mmoja tu benki?

Kama hizi figures ni kweli kwa benki kubwa kama CRDB, basi hali ya uchumi Tanzania ni mbaya kuliko nilivyokuwa nafikiri.

Mbaya sana tu.

Mpaka Magufuli ataisoma namba.
Statement ndivyo zinavyoonesha lakini the problem ni kwamba, Deposit ya 2 Billion si lolote mbele ya Loss (Profit)ya 2 Billion kwa sababu, endapo tuta-assume ni loss incurred from loan default basi tungesema hiyo 2 billion ni roughly 20% of total loan default.

But all in all, inaonekana hali si nzuri manake hata ukipitia indicator moja moja, nyingi performance yake imeshuka! Hata number of employees nayo imee-drop kutoka 2809 hadi 2449! Tunajua hawajapunguza wafanyakazi lakini inaonesha hakuna replacement kwa wanaostaafu au kuacha kazi!
 
anahangaika kuwachekesha wananchi na kuwapa matumaini hewa kwa kutumbua sijui mara uhakiki,

unaacha suala msingi la kuboresha uchumi,kila siku unaomba vyeti vya mwalimu Tandahimba,cheti kimoja unakiomba mara kumi kumi,

huku unaacha uchumi unateketea kwa moto mkali,what a joke!! hivi anapolipa mishahara huwa anafikiri hela inatoka wapi? hizo ni kodi za biashara ndogondogo na za kati,

kimsingi,nasubiri nione Kampuni ya bia Tanzania nayo itatangaza kupungua kwa mapato yake,nataraji pia serengeti brewries watangaze hasara au kupungua kwa mapato
 
Statement ndivyo zinavyoonesha lakini the problem ni kwamba, Deposit ya 2 Billion si lolote mbele ya Loss (Profit)ya 2 Billion kwa sababu, endapo tuta-assume ni loss incurred from loan default basi tungesema hiyo 2 billion ni roughly 20% of total loan default.

But all in all, inaonekana hali si nzuri manake hata ukipitia indicator moja moja, nyingi performance yake imeshuka! Hata number of employees nayo imee-drop kutoka 2809 hadi 2449! Tunajua hawajapunguza wafanyakazi lakini inaonesha hakuna replacement kwa wanaostaafu au kuacha kazi!
Kilichoniumiza sana hapa ni kwamba nilikuwa naihesabu CRDB kama benki kubwa Tanzania - at one point, I believe in the nineties, CRDB, pamoja na NBC kabla haijavunjwa, zilikuwa zinatajwa katika benki kubwa za Afrika-, sasa kusikia inapata quartely loss ya US $1 million na hiyo inakuwa big deal, hili linanionesha kwamba benki hii sio kubwa hivyo.

Kwa sababu US $1 million ni hela fulani CRDB inatakiwa kuweza kuiweka katika margin yake tu.

That's just margin money. Ni hela ya kusumbua vibenki vidogo vinavyoanza biashara. Benki kubwa US $1M ilitakiwa kuwa kwenye margin of error.

Are the numbers I read on "The Wall Street Journal" giving me unrealistic expectations? or is CRDB making a US $ 5 - 10 million profit a quarter totally realistic?

Hivi Tanzania kuna wafanyabiashara wakubwa wangapi wenye hela zaidi ya US $ 1 million wenye account CRDB? Hela hizi CRDB inazizungushaje?

Tunalia mzunguko wa hela umedorora kwa sababu ya Magufuli kubana hela, hizi benki zinafanya kazi zake?

US $ 1 million is just 20 USD 50,000 Jeeps.

How many branches does CRDB have in Tanzania? How many ATMs does CRDB have? How much does CRDB make from interest?

Is this exposing how much CRDB was floating on sitting in government money and now that Magufuli is consolidating government money back into BOT banks like CRDB are sufferring?

Is this exposing hiw fraudulent the banking system in Tanzania is when a hatdass president like Magufuki steps in?

I was just reading about how Mgawe (former TPA DG) is being dragged into court over some banking sleaze. Is TPA just the tip of the iceberg?

Sawa deposit ya $ 2m is a different story from loss or profit of $ 2M.

But let's say our goal is at least breaking even.

A quarter has 3 months. Lets make that 90 days for simplicity.That means CRDB could not make a profit of $1M for 90 days?

Lets break that down daily to keep things in perspective.

Give them 100 days for filing and everything. I have done this bureaucratic filing with the Security and Exchange Commission in Washington DC as well as with the Financial Conduct Authority in London. So I can be sympathetic enough to throw in an extra 10 days.

That still means that CRDB cannot make a profit of US $ 10,000 a day. With all its customer base and parastatal tag.

Is that Charles Kimei fellow still MD? That guy is a shame to the banking community in Tanzania and probably a big part of the reason this mess is taking place.
 
Wengi hapa mnatarifa zisizo sahihi, siku zote katika nchi, mabenki ya kibiashara yanafanya kazi na serikali ili kuendeleza uchumi. Benki ya biashara haichapishi hela, inategemea hela toka benki kuu ya nchi kwa njia ya mkopo au ununuzi bond za serikali. Benki ya biashara hukopa kutoka benki kuu, kwa njia ya riba ya chini, na inatumia fedha hiyo kukopesha watu wa kawaida, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo, bila kusahau makampuni. Mikopo hiyo inawekewa riba ilio juu kuliko ile ikiyo kopea benki kuu. Sisi tukilipa mikopo yetu, benki inakata cha juu na kurudisha ilichokopa benki kuu kama ilivyo kubaliana awali.

Sasa serikali nilivyo ondoa fedha zake za makusanyo na matumizi kutoka benki za biashara haikutakiwa kuathiri uwezo wa benki ya biashara kujiendesha kwasababi benki ya biashara bado inauwezo wa kukopa kutoka benki kuu na kutumia hiyo hela kuisambaza kwa wafanyabiashara ili na wao waweze kuendeza uchumi. Benki za biashara zililemaa na pesa rahisi ya serikali maana hawailipi riba, na wanaweza kutumia hela hiyo hiyo ya serikali kuwakopesha watu wengine tena kwa riba ile ile ya juu. Lakini mabenki yamekutwa katika wakati mgumu kwasababu hawakutarajia kama serikali itakata mrija wa fedha zake kwenye mabenki ya binafsi. Mabenki mengine hata mitaji yao ilikuwa imeswekwa kwenye biashara nyingine, na sio rahisi kurudisha hiyo hela haraka bila hayo mabenki kupoteza hela au kupata hasara.

Ni wakati wa mabenki kuwa wabunifu na kuja na product zingine ambazo zitavutia wateja kuingia kwenye milango yao ya benki na kufanya biashara kama ilivyokuwa siku za nyuma.
 
Ukilinganisha quarter hii na same quarter last year utagundua yafuatayo

1. interest income imeongezeka
2. interest expense imeongezeka for obvious reason
3. Impairment imeongezeka
4. cost zimeongezeka

kulingana na mazingira yalivyo kinachotakiwa kuwapa watu wasiwasi ni hizo impairment. impairment charge ya 38bn kwa miezi mitatu inasikitisha. hii inatokana na mikopp iliyotolewa kufanya vibaya kwa sababu kadhaa. lakini kubwa zinaweza kuwa mikopo magumashi au mikopo iliyotolewa kwa sectors ambazo zimeathiriwa na hali ya uchumi wa sasa. sector hizo ni hotel, kilimo, serikali (wafanyakazi hewa na uhakiki wa vyeti umewakimbiza baadhi ya wafanyakazi), na zinginezo.

is it bad news?
inaweza kuwa ndio lakini ukiangalia full year mpaka september bado wana faida nzuri tu ya kibeef mtaji wao. cha msingi ili kukabiliana na hali hiyo wanapaswa kuhakikisha wanareview lending strategy na kuhakikisha collection na recoveries inaimarika

Naamini bado ni benki bora nchini kwa sasa na sio vizuri kushabikia benki kubwa kama CRDB ikiyumba, athari zake ni kubwa
 
Wengi hapa manatarifa zisizo sahihi, siku zote katika nchi, mabenki ya kibiashara yanafanya kazi na serikali ili kuendeleza uchumi. Benki ya biashara haichapishi hela, inategemea hela toka benki kuu ya nchi kwa njia ya mkopo au ununuzi bond za serikali. Benki ya biashara hukopa kutoka benki kuu, kwa njia ya riba ya chini, na intumia fedha hiyo kukopesha watu wa kawaida, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo, bila kusahau makampuni pia. Mikopo hiyo inawekewa riba ilio juu kuliko ile ikiyo kopea benki kuu. Sisi tukilipa mokopo yetu, benki inakata cha juu na kurudisha ilichokopa benki kuu kama ilivyo kubaliana awali.

Sasa serikali nilivyo ondoa fedha zake za makusanyo na matumizi kutoka benki za biashara haikutakiwa kuathiri uwezo wa benki ya biashara kujiendesha kwasababi benki ya biashara bado inauwezo wa kukopa kutoka benki kuu na kutumia hiyo hela kuisambaza kwa wafanyabiashara ili na wao waweze kuendeza uchumi. Benki za biashara zililemaa na pesa rahisi ya serikali maana hawailipi riba, na wanaweza kutumia hela hiyo hiyo ya serikali kuwakopesha watu wengine tena kwa riba ile ile ya juu. Lakini mabenki yamekutwa katika wakati mgumu kwasababu hawakutarajia kama serikali itakata mrija wa fedha zake kwenye mabenki ya binafsi. Mabenki mengine hata mitaji yao ilikuwa imeswekwa kwenye biashara nyingine, na sio rahisi kurudisha hiyo hela haraka bila hayo mabenki kupoteza hela au kupata hasara.

Ni wakati wa mabenki kuwa wabunifu na kuja na product zingine ambazo zitavutia wateja kuingia kwenye milango yao ya benki na kufanya biashara kama ilivyokuwa siku za nyuma.
BOT ineshidwa kufanya kazi yake ya kuwa mkopeshaji wa mabenkiya kibiashara na hivyo kufanya mikopo iwe ghali zaidi kutokana na gharama za amana ambazo benki hizi zinaingia kupata amana.
Pia kwa serikali kuhamisha pesa zote kwenye mabenki kumeatbiri ukopeshaji ili kuanzisha shughuli mpya za kiuchumi au kuendeleza zile za zamani. Importers wanategemea mikopo katika biashara zao huwezi kuangiza mzigo ukauuza same day i uweze kuagiza mwingine matokeo yake yanaenda kugusa sekta nyingine kama Bandari.
Kupata hasara katika mabenki kama nilivyosema hapo mwanzo biashara nyingi zimesimama uwezo wa kulipa mikopo ya wafanyabiashara hasa wadogo umekuwa mgumu hivyo mikopo imekuwa mibaya sheria za uendeshaji wa mabenki chini ya usimamizi wa BOT inazitaka benki kufuta mikopo mibaya kwenye vitabu vyake kupitia faida ili kuendelea kuwadai wakopaji wakati tayari wameifuta na pale wanalipa basi inaongezwa kwenye faida ya mwaka mkopaji huyu anapolipa.
Hii unaweza iona katika vitabu vya CRDB wamefuta mikopo mibaya ya almost 38billion ambayo ni wazi imepunguza faida kwa 38billion lakini hii inavifanya vitabu vyake kuwa safi na kutengeneza mkakati mpya. Jambo kama hili lilitikea miaka miwili iliyopita kwa NBC ambao walipata hasara ya kama 2billion kwa mwaka huo tofauti na Crdb wao bado kwa majumuisho ya kipindi cha robo tatu bado wanafaida ya zaidi ya 100 billion na uwezekano wa kupata faida zaidi kwa mwaka 2016 ni mkubwa kwasababu tayri sehemu kubwa ya mikopo yake mibaya ambayo inakula faida amekwisha ifuta kwenye vitabu vyake na kuwa deni la kawaida kwa wakopaji.

Ushauri:
1. Serikali kuzipa nafasi mabenki kutumia pesa wanazokusanya kutoka a maduhuri ya serikali kubaki huko ili waweze kukopesha au

2. BOT kufanya kazi ya kuyakopesha manenki ili nayo yaweze kukopesha kwa riba nafuu kwa wananchi na kukuza uchumi.

Tahadhari;
Kwa mabenki kushindwa kuwa na amana za kutosha kwa serikali kukimbizia makusanyo yote (ambayo commericial benki ndo wakusanyaji) itaua uwezo wa mabenki na hivyo ukusanyaji wa mapato ya serikali ukawa mgumu kwa vile BOT hawana matawi nchi nzima.

Pia serikali itambue mabe ki ni mshirika wake katika kujenga uchumi na hatua zizote za kudhoofiisha sekta hii ni kuua uchumi.

Mwisho kodi inaongezeka kwa kuwa na uwekezaji mpya hivyo serikali inatakiwa kuhamasisha uwekezaji binafsi i kuweza kuvuna kodi la sivyo tukimaliza kukusanya hizi Tax arrears tunatabaki hatuna cha kukusanya (hili limeanza kujitokeza utaona malengo ya umusanyaji wa mwezi October yatavyofikiwa kwa mbinde)
 
Back
Top Bottom