Anguko la Dola ya Urusi li karibu

Anguko la Dola ya Urusi li karibu

kwani alitangaza vita wapi! ila walisema kaka red line waloeka isivukwe kwahio hata mjeshi yakienda wapi red line haiwez kuvuka nawakivuka tegemea crimea nyengine kijana
Nakubali hakutangaza lakini alikuwa ashaenda piga chabo tayari, aangalie hali ya hewa ka iko shwari, achukue kiulaini lakini akaonekana mchana kweupe, ikabidi aibu na viswahili vingi. Tamaa tu yake lakini sahi ashashtukiziwa na dunia, all eyes on mother Russia! 🤣
 
Asymmetrical responses ya Russia kwa atakeye vuka 'red line' ambayo wameichora wenyewe Russia siyo ya kujaribu. Wanamaanisha wale...na wako serious.
Wale ni sawa na terrorists tu, wanauwa raia wa Syria kule, na kila mtu anajua. Assad msaada mkubwa alitoa kwa hao pumba. Mnyama sana mrusi!
 
Nchi za kibabe Kama Murusi,N Korea,Irun,Hazifai kuzisifia kabisa maana zime fanya dunia kuwa mahali pa kuogofya badala ya utulivu na amani.
Aamani kama ilioko Iraq ,Libya na Afgha au ,tumieni akili katika kufikiri ,bila Marekani dunia ingelikua salama sana
 
Grammatical mistake. It supposed to be: "Not only is the Us better economically but---------".

Coming to the topic, The US is indeed economically giant and has more military facilities and weapons than any other country in the world, in contrary, Russia has fewer but SOPHISTICATED/ advanced military facilities and weapons than any other country.
Ajiulize tu kwann Marekani anapiga kelele kuuzwa mifumo ya ulinzi ya S-400 ambayo mifumo hio kwa Russia sio mipya ?
 
Anguko la Urusi linasemwa na mtu ambaye hajui siku itaishaje? Nimeamini wanaodemka na vigoma wapo wengi

Hawa ma prophet of doom hawakati tamaa, stori hizi za kufukirika/kusadikika kuhusu anguko la URUSI hazija anza leo,zilianza mapema baada ya kupinduliwa kwa utawala wa kifalme ambao ulikuwa na nasaba na ufalme wa Uingereza, Uingereza na Merikani walikasirika na kuchukizwa sana na mapinduzi ya Urusi ya Oct,1917 kwa kutaifishwa mali zao, kuuwawa kwa famile nzima ya Mfalme wa Urusi Tzar Nicolas pamoja na yeye enzi hizo, Nicolas alikuwa ni Puppet wa mataifa ya magharibi licha ya kuwa na undugu wa damu na Ufalme wa Uingereza.

Chuki za tangu mwaka 1917 ndio zinaendelezwa mpaka sasa kwa kutumia mbinu tofauti,leo watasingizia kupinga ukomunisti,kesho watasingizia Joseph Stalin,kesho kutwa Nikita Krushchev,mtondogoo Brezhnev - viongozi pekee ambao mataifa ya magharabi walielewana nao ni: Mikail Gorbachev na baadae Mlevi wa kupindukia Yeltsin - walikubalika kwa viongozi wa magharibi kwa kukubali kusambaratisha taifa la Urusi ambalo mbili ya tatu ya World land mass belongs to Russia,Urusi ndilo Taifa pekee Duniani lenye vast quantity ya mali asili au nyinyi hilo hamlijui!!

Kelele zote za magharibi lengo lao wanataka Urusi isambaratike kabisa hisiwe tishio kwao kijeshi na Big Petroleum Companies za magharibi including mineral companies waruhusiwe ku-exploit utajiri mkubwa wa Taifa la Urusi kwa manufaa ya Mataifa yao - akili zao zote zipo kwenye wizi/unyonyaji/uporaji ie kutawala Dunia kiuchumi na kijeshi wapo radhi kuingia vitani kujaribu ku-maintain status zao za kijinga,and they will never succeed kuisambaratisha Urusi,wataishia kumzulia Putin kutokana na msimamo wake dhabiti dhidi ya mataifa ya magharibi,vile vile Putin hapendwi baada ya kufufua uwezo wa Urusi kijeshi na kiuchumi - wanamuona ni nukusi kabisa, cha ajabu baadhi yetu waswahili tunaiga chuki za magharabi dhidi ya Urusi bila sababu zozote za msingi tunakuwa tu bendera fuata upepo kwa kuwa CNN na BBC wanatangaza kwamba Warusi ni Wabaya wanataka na sisi tuchukulie madai ya media za magharibi kama ni Gospel TRUTH.
 
Chalii angu umeandika kishabiki Sana.. kwanza nikukumbushe Jambo kuhusu neno "makala" neno makala Lina maana ya mfululizo au andiko kuhusu Jambo Fulani lakini Ni ukweli mtupu na sio maoni.. na Kama Ni maoni director, mwandishi ama producer lazima aandike na kusema wazi kwamba alisemalo Ni maoni tu na sio fact. Umenipata? Hilo moja
Mbili naomba nikukumbushe tu mwaka 2008 pamoja na uwepo wa Marekani( militarily) katika taifa la Georgia.. Russia iliivamia na kuichakaza Georgia vilivyo unajua US alifanyaje?
Walikimbia bila kugeuka huku wakibweka kutoka Washington. Cha ajabu zaidi warusi walingia Hadi alipokuwemo kambi ya pamoja ya Georgia na Marekani.. hapo akachukua Humvee nne akapakiza huyoo mbele...
Maskini Georgia akachapwa Sana Hadi ardhi kubwa tu ikamegwa na kuwa vitaifa viwili vinavyotambulika tu na Urusi.
Waukraine wakileta kelele za kutest kina Cha maji hata Leo ardhi yao itamegwa Tena na kuitwa Russia.. sitamani hili litokee..
 
Russia ni kama Iran tu budget kubwe militarily ila maendeleo nehi

Same tu N.Korea
Duh Urusi unaifananisha na N Korea..
Russia Ni taifa kubwa kijeshi , kiuchumi na kiteknolojia..
Bila shAka nchi yako inatumia Ak 47 kuwaua akina Akwilina.. hiyo Ak 47 iltengenezwa mwaka 1947..
Nikukumbushe tu dunia mzima hskuna kama Russia katika teknolojia y anga za mbali.
Kwaheri
 
Ulichoandika hapo sio Makala...Ni simlizi za kishabiki unaonyesha tu ushabiki wako...Makala Ingejaaa facts na mifano.
Nimemwelekeza pia hapo juu.. eti urojo huu nao Ni makala?
Tusaidiane kubadilisha hili jukwaani
 
Hebu nitajie madhara ya nuclear iwapo vita hiyo itapiganwa huko, kwa mimi mkazi wa hapa goba.
Mkazi wa goba kwanza salaam Sana.. ikipigwa nuclear Washington na New York kwanza kabisa ndo itakuwa mwisho wa kuperuzi Jf.
Pili anguko la uchumi.
Nb. Wataalam waongeze zaidi
 
Back
Top Bottom