Anguko la CHADEMA hili hapa

Anguko la CHADEMA hili hapa

Nimeona Kikongwe akishambulia Vikongwe wanzake.

Kwa hiyo mlipokea MSUKULE? Teteteeee..........
Tutampa darsa kama tunalowapa nyinyi humu kila siku, simlaumu sana kwa kuwa katokea hukohuko kwa vichwa maji, uliona chama cha siasa gani Duniani kikaendeshwa na DJ?

Bora huyo kastuka mapema, lakini misukule wengine kama wewe ni majanga tu.
 
Mtela Mwampamba,

Tutendee haki japo "kiduchu," ifanyie editing post yako, iwe japo na paragraphs, bado tu unakuwa na akili za Ufipa?

Mkuu umeniwakilisha na mimi, maana nimejikuta nasoma tu hakuna kupumzika.

ajitaidi kutenga aya ili asomeke vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Tutampa darsa kama tunalowapa nyinyi humu kila siku, simlaumu sana kwa kuwa katokea hukohuko kwa vichwa maji, uliona chama cha siasa gani Duniani kikaendeshwa na DJ?

Bora huyo kastuka mapema, lakini misukule wengine kama wewe ni majanga tu.

Wenye kuelewa tumekuelewa, mhusika na yeye ajue hili somo ni lake hivyo alifanyie kazi.!
 
Nasema hapana,mwenye macho haambiwi tazama,akili za mwenzio changanya na za kwako.

CCM inajenga nchi,hebu tazama hawa watendaji wanavyochapa kazi.

Viongozi wa CCM wanahangaika na kuzifahamu kisha kuzitatua kero za wana nchi,hawa wenzetu wao ni helikopta tu,mwanzo mwisho.Tutafika?

Wapinzani wanapotosha watanzania na hasa vijana.

Miundombinu ni moja ya Ilani za CCM kwa mwaka 2010,Tumeweza na bado sehemu chache tu.

Amani na Umoja ndio nguzo kuu ya watanzania chini ya CCM,wapinzani hawawezi kuleta amani,wapinzani hawana mashiko.Hivi Zambia wamepewa wapinzani,je kipi cha maendeleo ya haraka kimeletwa?si wana hifadhi kubwa kuliko zote Afrika?wapinzani hawana nia nzuri,wa vyama vyote tu iwe CDM au CUF ama hiyo UKAWA.

Tutavunja muungano au tuunde serikali 3,za nini?,kwa maslahi ya nani?,aah wapi!Somalia imeharibika vibaya sana,South Sudan na ile Sudan ya Khartoum leo zinatamaniana tena,ipo wapi Urusi ya sasa?sasa hata mmarekani ana sauti mbele ya Urusi hii na sio ile ya USSR.

Kama koti la muungano ni kero basi kero hizo zinatibika,maana hata koti likiw ana kiraka dawa ni kukata vipande vitatu?hapana,dawa ni kulishona pale tu penye jeraha na ndio tunachotaka.

UKAWA,wanatumia fedha kwa fujo,walikuwa wapi wakati wa kukusanywa kwa maoni ya Tume ya Warioba?,umaarufu kwenye mambo nyeti ya nchi ni ujinga.

Nchi haiwezi kuongozwa na mission town,nchi inapaswa kuongozwa na watu makini.Lazima tuseme tu ukweli na hata wakitukana tutapambana nao.

Hapana,lazima tujenge Muungano imara wa nchi 2 tu.Maoni ya watu 350,000 sio ya watanzania Milioni 44.Hapana nasema hapana.

Haya na tuachane na hayo sasa,twendeni tukajenge nchi.

Hongera Mhe Katibu Mkuu Kinana,hujataka kukaa ofisini na kucheza na karatasi,umeamua kuchapa kazi.

CCM NDIO NJIA KUU.


Mtela umeshaingia CCM na kupokelewa kwa nderemo na vifijo.
Upo ndani ya chama chenye serikali,chenye ukwas wa kutisha,chenye wasomi waliopindukia,sera zake zinaruhusu ukiupata mwanya unakuwa millionea within days.
Kwa nini bado unahangaika na watu amabo hawana serikali,wanaishi kwa ruzuku,aliyesoma ni mmoja,why??
Tumia fursa vizuri ukiwa CCM achana na CDM amabayo imeshakufa (kwa maneno yako).
 
Hilo neno "kumnanga" huwa mnalikosea maana na muktadha wake, kumnanga ni kumpamba (kumsifu) kupita kiasi, mimi sijampamba na wala sijamsifu, na kusema kweli hata post yake sijaisoma, ilivyo imenikatisha tamaa kuisoma.

Kwa ufupi nimemponda, sijamnanga hata kidogo.
shukran shangazi... nakunanga na wewe sasa:A S 13:
 
mmmmh mleta hoja cdhan ka ana credibility ya ku point figure kwa viongoz wa chadema......!!!

mbona hujaonyesha chaguz ndogo zilizofanyika nchini wkt zitto ni kiongoz.....au inatosha kusema hata kama walishindwa watu wengi walikuja kumsikiliza zitto??

vp ushawishi wa zitto jimbon kwake kutoka madiwan 11 kubaki 1 kipind chote cha zitto.....au huo nao ni ukomavu wa kisiasa wa zitto?
 
Mtoto mjinga sana huyu, Igunga na Arumeru nini kilianza? Arumeru Zitto ndio alikuwa anata ngazi nia ya Urais mara nia sijui ya kitu gani....umesahau Tuntemeke alivyo andika uongo kuhusu jimbo la Nassari sio......Zitto hakuwahi kufika Arumeru wakati wote wa uchaguzi......ndio kundi la Pm 7 lilikuwa liko peak..........
 
Chadema kwa siasa za chuki na ubaguzi, zimewafanya muishie kufa kibudu, Wassira. Aliwatahadharisha mapema.
 
Uongo weka kando,
chadema kimetetereka sana;
Jipangeni jamani, demokrasia kwetu ni muhimu zaidi.
 
Dr Slaa HAFAI kuwa Rais wa Tanzania 2015-2020
Dr Slaa ni Miongoni mwa Wanasiasa Wakongwe na
Machachali Hapa Nchini.Harakati zake Zimeanza
Zamani, Tangu Akiwa Mtumishi wa Kanisa Katoliki
(Padre) na Baadae Akafukuzwa Baada ya
Kuonyesha Utovu wa Nidhamu, Inasemekana
Haka Kamchezo Katamu Kalikuwa Chachu ya yeye
Kufukuzwa Upadre.
Nimekuwa Nikijiuliza,
1. Hivi Huyu Dr Slaa Alianza Kuwa na Ndoto za
Kuwa Raisi wa Nchi Hii Tangu Lini??Maana mimi
Nafahamu Alikuwa Padre, sasa Mapadre na Uraisi
katika nchi hii wapi na wapi??Maana Mapadre
Wameapa Kuwa Watumishi wa Mungu hadi Kufa
kwao…..Sasa Huyu Dr Slaa Kabla ya Kuwa Padre
Alikula Kiapo Kipi??
Na Kama aliapa kuwa Mtumishi wa Mungu
(Padre) na Akashindwa…Anawezaje Kunishawishi
Ataweza Kuwa Raisi wa Nchi Hii kwa Kipindi cha
Miaka Mitano??
Lakini Pia Nimekuwa Nikijiuliza
2. Hivi ni Kipi Alichokifanya Dr Slaa Hata
awashawishi Watanzania Hususani Vijana
Kumpigia Kura ili awe Raisi wa Nchi Hii??Maana
Mimi Namfahamu Dr Slaa Kama Mlopokaji,Mtu
Mwenye Jaziba, Mvunja Ndoa za Watu,Ndumila
Kuwili Maana Upadre anautaka,Uccm anautaka
na Uchadema anautaka Pia…..Msela Maana Hadi
leo Hajaoa Licha ya Kuwa na Miaka 72.
3. Jamani Hivi ni kweli Tumekosa Watanzania
Wazalendo,wenye Historia nzuri ,Wenye Elimu na
Wachapa Kazi,Wasio na Kashfa za Ubakaji Hadi
Tumchague Dr Slaa kuwa Raisi wa Nchi Hii??
Ikumbukwe ya Kwamba,Dr Slaa Alilazimishwa
Kugombea Uraisi kwa Ticket ya Chadema mwaka
2010,yeye Hakutaka, Alikuwa Anajua Kabisa
Hawezi Kushinda ndio Maana Aliilazimisha
Chadema Kuingia MKATABA wa Kumlipa Mshahara
na Posho kama Wabunge endapo Atashindwa
kwenye Kinyang’anyiro Hicho.
4. Hebu Tujiuliize Pia..Hivi Historia ya Dr Slaa
Inatushawishi Kumchagua Kuwa Raisi wa Nchi
Hii??Maana mimi naona Hostoria yake
Imepindapinda kama Zigzag Line…….
Kiukweli Kabisa,Dr Slaa ni Mroho wa
Madaraka,Mbinafsi kama Freeman Mbowe…ndio
maana Alivyokatwa jina lake katika kura za maoni
ndani ya CCM mwaka 1995 Akaamua Kukimbilia
Chadema.Huwezi Kusema Dr Slaa Anaipenda
Chadema Maana Bila Kukatwa jina,asingekuwa
Chadema Hivi Leo….
UFUPISHO
Dr Slaa Hafai Kuwa Rais wa Nchi Hii kwa Sababu
1. Sio Muaminifu, Haaminiki Sio kwenye Masuala
ya Kiutawala tu bali hadi kwa Vimada wake..
2. MUHAFIDHINA, Akichaguliwa, Hata Kubali
Kutoka Madarakani,atakuwa King’ang’anizi kama
Museven…
3. Hana Uwazi, Ameshindwa Kusimamia Usomwaji
wa Taarifa ya Mapato na Matumizi ndani ya
Chadema…
4. Mgonjwa, Anaumwa Kisukari na
Pressure….Taifa Linaweza Kula Hasara za Kufanya
Uchaguzi Mwingine Katikati ya 2015-2020 Maana
Afya ya Mtu Huyu ni kama Mvua za Dodoma…..
Vijana Tutafakari kwa Kina….Nani Anatufaa Lakini
Tusipoteze Muda Kumfikiria Dr Slaa…
Viva Vijana Vivaaaaa……..
 
Badala ya kufanya tathimini ya ANGUKO LAKO unajadili anguko la CHADEMA.
 
4. Mgonjwa, Anaumwa Kisukari na
Pressure….Taifa Linaweza Kula Hasara za Kufanya
Uchaguzi Mwingine Katikati ya 2015-2020 Maana
Afya ya Mtu Huyu ni kama Mvua za Dodoma…..
Vijana Tutafakari kwa Kina….Nani Anatufaa Lakini
Tusipoteze Muda Kumfikiria Dr Slaa…
Viva Vijana Vivaaaaa……..
Mtela Mwampamba, "nature" haiendi kwa matakwa yako binafsi! yeyote anaweza kufa wakati wowote! usidhani kuwa na umri mdogo ni uhakika wa kuishi! wala kushinda unaandika upumbavu wako hapa sio tiketi ya maisha marefu. Naamini unaweza ukafa wakati wowote ukamuacha unayedhani ni mgojwa anadunda. Jifunze kuwa na kauri za heshima kijana.
 
Back
Top Bottom