Nasema hapana,mwenye macho haambiwi tazama,akili za mwenzio changanya na za kwako.
CCM inajenga nchi,hebu tazama hawa watendaji wanavyochapa kazi.
Viongozi wa CCM wanahangaika na kuzifahamu kisha kuzitatua kero za wana nchi,hawa wenzetu wao ni helikopta tu,mwanzo mwisho.Tutafika?
Wapinzani wanapotosha watanzania na hasa vijana.
Miundombinu ni moja ya Ilani za CCM kwa mwaka 2010,Tumeweza na bado sehemu chache tu.
Amani na Umoja ndio nguzo kuu ya watanzania chini ya CCM,wapinzani hawawezi kuleta amani,wapinzani hawana mashiko.Hivi Zambia wamepewa wapinzani,je kipi cha maendeleo ya haraka kimeletwa?si wana hifadhi kubwa kuliko zote Afrika?wapinzani hawana nia nzuri,wa vyama vyote tu iwe CDM au CUF ama hiyo UKAWA.
Tutavunja muungano au tuunde serikali 3,za nini?,kwa maslahi ya nani?,aah wapi!Somalia imeharibika vibaya sana,South Sudan na ile Sudan ya Khartoum leo zinatamaniana tena,ipo wapi Urusi ya sasa?sasa hata mmarekani ana sauti mbele ya Urusi hii na sio ile ya USSR.
Kama koti la muungano ni kero basi kero hizo zinatibika,maana hata koti likiw ana kiraka dawa ni kukata vipande vitatu?hapana,dawa ni kulishona pale tu penye jeraha na ndio tunachotaka.
UKAWA,wanatumia fedha kwa fujo,walikuwa wapi wakati wa kukusanywa kwa maoni ya Tume ya Warioba?,umaarufu kwenye mambo nyeti ya nchi ni ujinga.
Nchi haiwezi kuongozwa na mission town,nchi inapaswa kuongozwa na watu makini.Lazima tuseme tu ukweli na hata wakitukana tutapambana nao.
Hapana,lazima tujenge Muungano imara wa nchi 2 tu.Maoni ya watu 350,000 sio ya watanzania Milioni 44.Hapana nasema hapana.
Haya na tuachane na hayo sasa,twendeni tukajenge nchi.
Hongera Mhe Katibu Mkuu Kinana,hujataka kukaa ofisini na kucheza na karatasi,umeamua kuchapa kazi.
CCM NDIO NJIA KUU.