Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,193
Kwa muda mrefu sasa baada ya kifo cha Hayati Magufuli tumeshuhudia minyukano ya wazi ya kutokukubaliana baina ya Makada wa CCM kuhusu mwenendo wa baadhi ya mambo yawahusuyo wao kwa wao.
Hivi karibuni kwa mfano Makada na waliopata kuwa Katibu wa Nec na Uenezi wa chama kile ndugu Nape Nnauye na mwenzake ndugu Hamfrey Polepole kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wamekuwa wakiandika maneno ya kejeri ambayo kwayo hutafsirika kwa wapambe wao kama ni kutupiana ndogo baina yao.
Aliyekoleza zaidi minyukano hiyo ni Kada mwingine na M/kiti mustaafu wa Jumuiya ya wazazi CCM bwana Bulembo alipojitokeza na kumnanga waziwazi ndugu Polepole na aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM hapo kabla ndugu Bashiru Ally kwamba kwa upamoja wao walikuwa wageni ndani ya CCM na alishangazwa na ukimbelembele wao kuhusu CCM ilihali hawana hizo sifa za kukisemea CCM kupitiliza.
Ikumbukwe bwana Polepole alikuwa anaendesha kipindi maarufu kijulikanacho 'shule ya uongozi' ambacho ni wazi kilikuwa mwiba kwa kina Bulembo na wenzake hali iliyopelekea baadhi ya Makada kuomba TCRA ikifungie kipindi hicho kwa madai eti kinamkosea adabu Mkuu wa Nchi.
Hivi sasa kipindi hicho kimefungiwa kwa muda usiojulikana.
Ni mengi yasikikayo mtaani na kwenye mitandao ya kijamii inavyotia mashaka uwezo wa CCM kujisimamia yenyewe kumaliza tofauti za Makada wake.
Kolezo la kutisha zaidi kuhusu mgogoro huo ni pale mapema jana Spika wa Bunge la Tanzania na mwanachama wa CCM aliposema deni la nchi ni kubwa na anadhani endapo Viongozi wataendelea kukopa huenda Nchi itauzwa kufidia madeni hayo.
Rais Samia mapema leo aliposhuhudia utilianaji saini kuhusu mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Makutupora kwenda Tabora amenukuliwa kuwananga wanaohoji namna anavyokopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo jambo ambalo wadadisi wa mambo wanahisi pengine alikuwa akimjibu bwana Spika kwa alichokisema jana kuhusu deni la Taifa.
Je,minyukano hiyo na mingine inayoendelea itakiacha CCM imara ama ndiyo anguko lake li karibu?!