Unapotosha kwa kujua au kutojua? Mwenekiti wa CCM alifariki na hajachaguliwa wala kuteuliwa mwingine. Upinzani wameomba kukutana na Rais si Mwenyekiti wa CCM, Lakini hata kama Rais ndiye angekuwa ndiye Mwenyekiti wa CCM wao wanapoomba kukutana na Rais hawaombi kukutana na Mwenyekiti automatically!, na ndiyo maana watakutana Ikulu na siyo Lumumba au CCM Dodoma!
Tujifunze kutofautisha haya mambo mawili, na hili limekuwa tatizo la muda mrefu, rais anafanya ziara ya Kiserikali kwa gharama za serikali lakini wakati huo huo anafanya na shughuli za chama kwa gharama hiyo hiyo.