Anguko La CCM Arumeru: Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anguko La CCM Arumeru: Tafsiri Yangu

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by maggid, Apr 2, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  Unaweza kuwatawanya watu kwa mabomu , lakini kamwe, mabomu hayawezi kuitawanya mioyo ya watu yenye kutaka mabadiliko.


  Habari kubwa usiku wa kuamkia leo ni anguko la CCM kule Arumeru Mashariki kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha Ubunge.


  Tafsiri yangu;


  Kuna wakati Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alipata kutamka; " CCM haina hati miliki ya kutawala". Mkapa aliusema ukweli wake ambao kwa bahati mbaya hupata tabu kuusimamia. Na hakika, idadi ya Watanzania wenye kutaka mabadiliko inazidi kuongezeka. Na katika siasa za nchi hii ukiona wanawake watu wazima wanashiriki mikutano ya kampeni ya wapinzani, basi, ujue ni ishara ya mabadiliko yanayokuja.


  Na ukweli mwingine ni huu; vijana wengi zaidi wamekuwa mstari wa mbele katika kutaka mabadiliko hayo. Kimsingi Arumeru Mashariki wamechagua mabadiliko. Na si kwamba Chadema ni chama bora na makini sana, la hasha, Watanzania wengi zaidi vijana wanaonyesha kuichukia CCM. Miongoni mwao ni Wana-CCM. Kiukweli, mvuto wa Chama Cha Mapinduzi kwa Watanzania na hususan vijana unazidi kupungua.


  Na ajabu ya matokeo ya Arumeru?


  Katika hali isiyo ya kawaida, kuna Wana- CCM waliyoyapokea kwa furaha matokeo ya chama chao kushindwa Arumeru. Tafsiri yake? Ni kushamiri, si tu kwa makundi ndani ya chama hicho, bali, hofu ya kutokea kwa mpasuko ndani ya chama hicho katika mbio za kuusaka Urais ifikapo mwaka 2015.

  Kitakachotokea sasa ndani ya chama hicho ni ‘ Witch hunting’- kutafutana uchawi. Bila shaka, kuna maswali yatakayoulizwa. Moja kubwa ni hili; kimeshindwa chama au mgombea? Na msukumo wa swali hilo ni katika kumtafuta mchawi na kukitenganisha chama na mgombea katika ‘Anguko la Arumeru’. Huo utakuwa ni mwendelezo wa ‘ Vita vya Panzi’ ndani ya CCM. Lakini, katika siasa, kuna wanaoamini pia, kuwa wakati mwingine kuna lazima ya kuwepo kwa ‘ Vita vya Panzi’ ili kujitenganisha na kumbikumbi.


  CCM ifanye nini?  Jibu; ifuate njia ya Dr Harrison Mwakyembe


  Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Ipinda hivi majuzi Dr Mwakyembe alitoa kwa watu wake kauli ya ‘ Kichifu’ na iliyojaa hekima na busara. Alisema; “ Mimi sikubaliani na mtu yeyote anayesema kitu cha kwanza ni chama chako…. Hapana, mimi kitu cha kwanza kwangu siyo CCM , cha kwanza mimi ni Mtanzania, cha pili ndio tunaingia kwenye vyama. Mtu anayekimbilia chama kuwa cha kwanza hivi hicho chama kingetokea wapi kama siyo taifa?”. ( Dr Harrison Mwakyembe, Nipashe, Machi 31, 2012)

  Na nilimwona na kumsikia Dr. Mwakyembe akiyasema hayo kwenye runinga. Umati ule uliomshangilia Dr Mwakyembe ulikuwa wa wananchi bila kujali itikadi zao. Kulikuwa na Wana -Chadema pia, na kiongozi wa Chadema alipewa kipaza sauti kuongea kumkaribisha ‘ Chifu Mwakyembe’ aliyerudi nyumbani na mtazamo mpya wa kizalendo.


  Kuifuata njia ya Mwakyembe itawasaidia CCM kurudisha umaarufu wao. Maana, moja ya sababu za wananchi walio wengi kuichukia CCM ni hulka yake ya kuwabagua wapinzani na kuwaona ni watu wasiofaa kushiriki uongozi wa nchi.

  WaTanzania wengi sasa wanatambua, kuwa si kweli wapinzani ni watu wabaya. Ni maadui. Kwamba watasababisha vita na vurugu. Wananchi wameona pia kazi njema inayofanywa na upinzani. Ghiliba hii ya CCM kuwachonganisha wapinzani kwa wananchi imepitwa na wakati. Badala yake, inachangia kupunguza kura za CCM.


  Na CCM isipobadilika sasa, na Chadema ikabaki kama ilivyo sasa bila kusambaratika, basi, CCM itakuwa na wakati mgumu sana ifikapo 2015, maana, kuna ‘Jeshi kubwa’ la vijana linalojiandaa na kushiriki uchaguzi wa 2015. Jeshi hili linaundwa na vijana wengi wasio na ajira wala hakika ya maisha yao ya kesho. Wanaiona CCM kama sehemu ya matatizo yao. Wana kiu ya kumpata mkombozi.


  Na wanafunzi hawa wa Shule za Kata wamegeuka kuwa ‘ agitators’ wazuri wa mabadiliko. Ikumbukwe, shule za kata ziko vijijini. Siku hizi hata waliokuwa wakiitwa ‘ wajinga’ wa vijijini wamepata walimu wa kuwafungua macho. Watoto wao wenyewe wanaosoma au waliomaliza shule za kata na kubaki vijijini kwa vile hata uwezo wa kujisomesha elimu ya juu hawana. Hawa hawana mapenzi na CCM.


  Na katika vijana mia moja hii leo, utapata kazi kubwa kuwapata 20 wanaoipenda CCM. Huu ndio ukweli wa hali halisi. CCM ibadilike na kuwa chama cha kisasa kilicho tayari hata kuongoza nchi pamoja na wenzao wa upinzani. Yumkini jitihada za CCM kuangamiza upinzani zaweza kuwa na madhara makubwa endapo CCM itapata bahati mbaya ya kuondolewa madarakani 2015. Maana, anguko hilo laweza pia kumaanisha kifo cha chama hicho.


  CCM haipaswi sasa kufikiria mikakati ya kuangamiza upinzani ili watawale daima. Dhana ya ’ CCM Daima’ ni ndoto iliyopitwa na wakati. Katika Tanzania ya sasa kuna wengi wenye kuombea kubaki hai na kushiriki kuzifuta ndoto kama hizo.


  CCM ya sasa inapaswa kupanga mikakati ya kuendelea kuongoza dola huku ikishirikiana hata na wapinzani. Ingawa hata huo ni mtihani mgumu wenye kukihitaji chama hicho kuwa na watu makini zaidi badala ya waendekeza fitina na majungu.


  Na hii ni tafsiri yangu.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Haya mkuu maggid...........
   
 3. dazenp

  dazenp Senior Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tetesi zimeanza kusambaa mitandaoni usiku huu. Kwa mujibu wa mtandao wa JamiiForums, Baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti inaripotiwa na mtandao huo kuwa CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM. Hata hivyo, matokeo rasmi hayajatangazwa na Tume ya Uchaguzi. Hivyo basi, taarifa hizi zinabaki kuwa ni tetesi kwa vile hazijathibitishwa rasmi hadi wakati huu tunaporipoti.........................................................................................................................hayaaaaa
   
 4. dazenp

  dazenp Senior Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Read between the lines between your posts ..............i can see CCM in you......Mjengwa hiyo ni copy and paste ya Blogu yako
   
 5. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,032
  Likes Received: 564
  Trophy Points: 280
  Good analysis
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mda mwingine ukijitoa kwenye mlengo wa ccm unakuwa mzuri kweli bwana!
  Hawajachelewa sana ingawaje kwa sasa wanamzigo mzito kuleta ccm kwenye mstari!
   
 7. D

  Davie Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Uchambuzi mzuri Majjid,...ila hawa watawala wa CCM cjui kama wanasikia ushauri...
   
 8. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Aha bwana Maggid wakati mwingine unangonjera kavu! ccm ibadilike ili iweje? mi naamini usemi aliosema nyerere siku alipohojiwa na bbc wakati akitangaza kung,atuka 1984 namnukuu" kile ambacho nilishindwa kukifanya katika miaka 24 ya kuwa rais na maka sita ya kuwa mwenyekiti wa chama kwa ujumla miaka 30, siwezi kukifanya hata nikipewa miaka mingine 30" hii alimaanisha yeye kama binadamu wa kawaida huwa inafika kipindi akili haibadiliki tena na kila uanachokifanya utatumia uzoefu wa nyuma, hivyo unavyosema ccm ibadilike wakati mfumo wake ni uleule mi nakushangaa! kwa kifupi ili tusonge mbele lazima ccm ikae pembeni la sivyo ngonjera zitabaki zilezile " mwakyembe kapewa sumu, jairo kaiba fedha, lowassa fisadi,epa n.k na wengine watakaojitokeza mbeleni".
   
 9. M

  MLO Senior Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wito wote wanaoamini bado kuna mafinikio kupitia mgongo wa ccm kuamka na kubadilika.
  Alipewa Hadhi zote.Rais,mwenyekiti mstaafu na Yeye ndiye amebeba Orodha ya ukoo wa MWL akaambulia " HATUDANGANYIKI" "PEOPLES POWER"Mbuzi hana Nguvu lakini makelele yake huzaa nguvu za ajabu Arusha na Kilimanjaro wailisikia kilio cha chadema kubakwa.wote wakahamia Arumeru.Tushikamane tutashinda
   
 10. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni akili ya mtu taahira tu atakayefikiria kuwa yale aliyoamini na kutenda 1977, akiyatenda leo atapata matokeo tofauti. If "you do'nt like to change with change then change will change you"
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Yaani bado unawaonea huruma, unawapenda mpaka kuwasikitikia kiasi hicho!!
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Uchambuzi mzuri
   
 13. u

  umumura Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi ninafikiri kwamba, Kama CCM kinataka, kama chama kiendelee kuwepo na kuwa na ushawishi, kijiandalie mazingira ya kuondoka madarakani chenyewe, wakae pemmbeni kwa muda wa miaka kumi kwa makusudi kabisa, kwa muda huo kijisafishe (ile dhana ya kujivua gamba itatekelezeka tu kama CCM itakua bench), baada ya hapo wajipange wagombee uraisi, yaani hapa ni 2025. Lakini kikidhani kitaendelea kuhadaa wanannchi, kuiba kura , kuua upinzania kwa nguvu ya fedha kikisaidia na usalaama wa taifa na vyombo vya jeshi, wataanguka anguko kuu, ambalo ama hakika hawatasimama tena.Salama ya CCM ni kujiandaa kuondoka ikulu wao wenyewe, ama sivyo wanajizika.
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwanini inakuwa tafsiri yako kila siku??? au ndo uandishi wa siku hizi?:nono::nono:
   
 15. b

  bluhende Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  big up Mjengwa kwa uchambuzi makini. Wasiwasi wangu ni kuwa ccm hakuna dalili za mabadiliko. Kwanza chama kimekosa msimamo, kwasababu haijulikani kinasimamia nini. Hebu jiulize kuhusu kujivua gamba, tuliaminishwa kuwa kuna mapacha watatu wanaochafua chama inabidi waondoke lakini mpaka leo wapo na bado wanaendelea kufadhili chama. Ccm inatakiwa iwaombe radhi watanzania kwa usanii huu. Mboma chadema imeweza kuwavua uanachama madiwani kule Arusha. Pili, iache siasa za ghiliba na matusi. Rais mstaafu mkapa kipindi cha utawala wake aliuza mashamba yote kwa wawekezaji leo hii anatoa wapi ujasiri wa kuahidi kurudisha mashamba hayo kwa wananchi? Kama sio kufilisika kisiasa ni nini? Tatu, ccm hawana watu wa kuongoza kampeni mpaka wamtumie Lusinde ambaye ni dhahiri hana si elimu ahera au elimu dunia tu lakini hata kiwango chake cha busara kiko chini kuliko kawaida (below average). Chama pamoja na kuwa na rasimali za kutosha kimeendelea na utamaduni kuombaomba kutoka kwa matajiri wachache ambao wakati mwingine huitwa mafisadi. Mwisho ccm inabidi izaliwe upya kimfumo na kimkakati. Yaani kirudi mikononi mwa wanachama. Mimi sio mtabiri wala nabii lakini nionavyo mimi ccm iko mahututi na hakuna dalili za kuzinduka. Ingawa 2015 inaweza kuwa ni karibu sana kufanya mazishi ya chama hiki lakini zote zinaonyesha ugonjwa wake hauna tiba. It is just a matter of time kifo kiko palepale.
   
 16. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  OP ED yake imebatizwa hilo jina ni suala la kitaaluma kama ilivyo ''kichwa maji'', nilonge nisilonge, kiona mbali, makala ya Mwanakijiji na nyingine nyingi.
   
 17. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Leo Maggid Umekuwa newtral, inapolazimu sema kile kilicho cha kweli na sio kuwapaka CCM mafuta kwa mgongo wa chupa.
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maggid, sometimes ni busara na uungwana kutoa pongezi tu hasa ile siku ya kwanza ya tukio na katika kinyang'anyiro kilichokuwa na kila aina ya vuta nikuvute na visa!!!!!!
   
 19. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  maggid, hili lichama ndo kwaheri
   
 20. s

  sanjo JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mkuu Maggid,

  Huo ushauri utapita upande wa sikio la kushoto na kutokea la kuria. Agenda kuu ya CCM ni kulinda ulaji wa watawala kwa gharama yeyote. Kwao kushindwa kwenye uchaguzi ni sawa la kunyang'anywa tonge la ugali kinywani. Kwa wale ambao wanajua tafsiri sahihi ya njaa bila shaka wanatambua maana ya mtu kunyang'anywa chakula mdomoni wakati mtu tayari ana njaa ya siku kadhaa. Hasira yake huwa haina mfano kwani hata ustaarabu hukosekana kabisa.

  Kwa ufupi, CCM ilikosa mwelekeo na muunganiko wake kwa wakulima na wafanyakazi toka Azimio la Zanzibar.
   
Loading...