Anguko La CCM Arumeru: Tafsiri Yangu

Maggid, umenena. Ili kupata mwanga itabidi CCM kufanya mageuzi, kama siyo mapinduzi ya kifikra. Kwa bahati mbaya CCM iko 'bize' ikizika elimu. Mfano ni utitiri wa PhD za Wabunge wa CCM lakini ukiwauliza wamezipata vyuo gani au wamezisotea kwa kipindi gani hupati majibu zaidi ya kupuuzwa. Katika karne ya 21 elimu itasaidia kutambua njia hata namna ya kundesha siasa ndani ya nchi. Sasa itawezekanaje kuona njia bora wakati viongozi ni 'mbumbumbu' wakijivunia sifa ya mipasho tu. Yatakuwa maajabu kipofu kuongoza vipofu wenzake. Tutafakari
 
Maggid kwa CCM hii kubadilika ni kazi sana labda tusubiri CCM ya kina January, Ester Bulaya n.k kwa sasa kumbadilisha fikra mtu kama Willson Mkama, Kingunge, Lusinde, Kilango, Wassira, ni ndoto za alinacha kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom