Ang'atwa korodani aking'ang'ania penzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ang'atwa korodani aking'ang'ania penzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 6, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAUME mmoja ambaye ni mkulima, Selemani Abdallah miaka 47 amejeruhiwa sehemu zake za siri baada ya kung'atwa korodani na mke wake.

  Tukio hilo, lilitokea juzi katika Kijiji cha Mindu Kata ya Mkuzi wilayani Muheza ambako anaishi na mke wake aliyefahamika kwa jina moja la Maria.

  Akizungumza na Mwandishi wetu, Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tanga, Jafari Mohamedi alisema mkulima huyo aling'atwa na mke wake usiku wakati na kwamba walikuwa wakigombana masuala ya mapenzi.

  Mohamedi alisema chanzo kikubwa cha ugomvi huo, kimetokana na mwanaume huyo kudai mapenzi kwa mke wake usiku wakati amelewa.

  Alisema mke wake alimnyima mapenzi akidai amechoka hawezi kufanya kitendo hicho na mume, lakini mume wake aliendelea kumlazimisha.


  Mohamedi aliongeza kuwa mkulima huyo alimshika kwa nguvu mke wake ili ampe penzi, lakini walivutana na mke alipata nafasi na kumng'ata korodani mume wake na kulipasua moja.

  Kutokana na hali hiyo mwanaume alipiga kelele ndipo watu walijitokeza na kumpeleka polisi Muheza mjini na kupewa PF3 na kupelekwa hospitali ya Teule kulazwa kwa ajili ya matibabu.

  Baada ya taarifa hiyo, polisi walimkamata mwanamke huyo na kumfikisha katika kituo cha polisi kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Dunia hii imeisha sijui tuende wapi. Sasa kama tunachakachuliw a kimaisha unarudi nyumbani angalau basi mama akuliwaze nae anakungata hii ngumu kabis. Mimi naona kama huyo mama alikuwa ameshachakachul iwa akawa hoi ndio maana hakutaka.Pia ina nipa picha Kina Dadapoa ndio maana hawakosi biashara kwani mazingirakama haya yanashawishi kujimuvuzisha. Kinababa tuunde vikundi vya Usawa wa jinsia Wenzetu Kenya walishafanya hivyo baada ya mwenzao kula kichapo.Huyo mzee keshahasiwa hana kazi tena huyo mama ni Muuaji hafai.Hiyo ni sawa ni kufanya fojo IKULU.Pia naamini ana mume mwingine kafanya hayo ili Mumewe asimsumbue.Tuwe Macho Kiama Chaja
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  I can imagine, how painful it was!
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  S/times wanawake ni wakorofi sana unamg'ata mtu bailojia kuu? uzao? kwa nini hakumng'ata hata usoni? huyo mwanamke ni kicheche kana wanaume nje ya ndoa
   
 5. D

  Dick JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa upande mmoja, ni haki na halali ya mme kupata ndoa kutoka kwa mwenzie. Katika mazingira ya kawaida, mke hatakiwi kukatalia penzi.

  Kwa upande wa pili, ni mazingira yapi huyo mme astahili kupata hiyo ndoa? Inawezekana huyo bwn alirudi usiku sana mke ameshapumzika kutokana na shughuli za mchana kutwa, au anaumwa (mambo ya wakubwa), au walishakubaliana kuwa anywe kiasi ndo haki hiyo itapatikana, mme kanywa kupita kiasi pengine.

  I stand to be neutral, kwa kuwa sielewi mzizi/chanzo (tofauti) cha tatizo ni nini japo sijui huyo mama 'kesho atakula' wapi.
   
 6. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yaani huyo mke???? Bora angemng'ata akamwacha, yeye kaling'ata hadi KALIPASUA???? Huyo jamaa nampa Pole sana koz ile kitu inauma sana......
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  uuuh...afadhali...
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Linavojua kuuma hilo likiungo, Loh! Jamaa alipata mateso ya ajabu. Nadhani alizimia kabisa.
   
 9. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Unajua maumivu yake?

  Inasikitisha sana hata wale waliooa na kutolea mahali na kuunganishwa na Mungu bado nao kula tunda ni kazi.....Sijui tunakwenda wapi?
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mie nadhani zipo sababu nyingi za msingi za mke kumnyima unyumba mume au mume kumnyima unyumba mke ila kumngata korodani naona kama hiyo ndoa inawalakini yawezekana walioana wakiwa hawapendani kwa dhati toka mioyoni mwao kwasababu kwa kungata hiyo kitu unawezampotezea maisha mwenzako!binti inaelekea alikuwa na hasira sana!kwa kulazimishwa
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  hatuendi mahali kwa sababu wakati mwingine wanaume hupenda kula tunda kwa namna yao wanayotaka wenyewe bila kufanya mawasiliano mazuri na mliwa......sasa unafikiri kitakachofuata hapo ni nini kama si kung'ata
   
 12. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwa mke na Mume najua lazima kuwe na makubaliano lakini walipooana ni wazi kuwa walikubaliana kuishi kwa shida na raha.Sasa ni kipi cha kumnyima mwenza wako haki yake ya msingi huoni mwanamke kutoa sababu za kuchoka akiwa katika ndoa ni kumuonea mwenzie.Kwani asinge kubali kwenda kumpa hata kimoja tu cha hamu?
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  ki ukweli kisa cha mama kung'ata mimi na wewe hatuwezi jua....unaweza kuta alikuwa na stress za maisha na zimesababishwa na huyo huyo baba, ni vigumu kwa yeye kupata hisia za kufanya mapenzi na mumewe....inaonekana kilichokuwa kinataka kutokea hapo ni ubakaji......wakati mwingine mnatubaka sana jamani.....itabidi katiba mpya ilitizame hili
   
 14. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  sasa kama hamuwezi kukamilisha time table ya mieleka si mturuhusu bana tulegalaiz small hauz, hivi mimi niko boiling point halaf unaniambia nisubilie kesho. aaaaargh lazima mkubali kwamba mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja bana! matokeo yake ndio haya ,kiwanda cha kutengeza watoto kishawekwa demeji.
   
 15. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  hapo naomba nirizevu komenti zangu......ngoja kwanza tuendelee na uchunguzi wa huu ung'atwaji
   
 16. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hapa hamna uchunguzi, jamaa auguze majeraha na huyu mama ang'olewe meno kwa amri ya polisi ili kuepusha ajali nyengine kama hii in ze fyucha.
   
 17. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  teh teh...aking'olewa meno atatumia kucha....ili mradi korodani zisumbuke
   
 18. e

  ejogo JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa huyu mama amekibomoa kiwanda cha kutengeneza watoto, hataki tena production ya watoto!!!! I feel very sorry for the man!
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Duh noma, kabisa unang'atwa tena na mkeo mmh kazi kweli
  Bora angempa apige hata 1 kuliko kumng'atua mmewe pum*u
  mambo hayao tena duh!:eek:
   
 20. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  sasa badala ya condoms itabidi tuvae na korodani proof, kwa hali hii ni kweli TANZANIA TUNAHITAJI KATIBA MPYA.
   
Loading...