Habari wanajamii!
Mimi ni
HoD katika taasisi moja ya serikali, inayojihusisha na utoaji wa elimu ya juu Jijini DSM, huko nyuma tuliwai kuomba ofisi ya Rais Utumishi wa umma, kutangaza nafasi za kazi ambazo zipo wazi hapa ofisini kwetu, nyingi zake zikiwa ni walimu, na chache zilikuwa za watu wa utawala!
Baada ya mchakato wa kutangaza na hatimaye waombaji kuitwa na tume katika APTITUDE TEST, ikaja zamu ya Oral interview na Practical interview kwa upande wa walimu! Mimi nilikuwa memba wa interview panel wa taasisi nikishirikiana na wale maofisa kutoka utumishi!
Cha kusikitisha ni namna watanzania wenzangu wasivokuwa na umakini katika masuala muhimu kama utafutaji wa ajira na hasa interview, ama niseme sijui ni masihara ama uswahili wetu! Makosa mengi yalifanywa na wahojiwa kiasi cha kunitia simanzi mle ndani ya INTERVIEW PANEL, huku nikichoka kwa kujua upuuzi wote ule, wametoka katika vyuo vyenye majina makubwa hapa nchini! Baadhi ya makosa yaliofanywa na waombaji kazi ni haya hapa:
- Wengi walikuwa na maelezo marefu sana, tena yasiyo ya msingi ktk swali la kwanza kwa kila muulizwaji. Wote walianza kwa kuulizwa: "Tell us about your historical background" Yaani hapa watu walibwabwaja, aiseeee1 watu wakataja mpaka wanasiasa, wakataja vyama, idadi ya watoto, wengine wakataja hadi mambo ya ndoa, kuna waliotaja hobby zao, yaaani maelezo mengi mpk huruma! walichemka vibaya!
- Hii nchi kuna urasimu sana kama uliwahi ama bado unafanya kazi serikalini, na kisha ukaomba kazi sehemu nyingine, serikalini! katika interview ile, sijui ni kutokujua (nimewasamehe) ama ni kupenda sifa, wasailiwa walikuwa na mbwembwe sana wakati wakujibu swali hili! Katika panel niliokuwepo, kati ya wasailiwa 15, 7 walisema wamewahi ama wanafanya kazi serikalini, afisa utumishi kutoka UTUMISHI aliwadisqualify kuendelea na interview wasaliwa wa aina ile, on the spot!
- Wengi hawakutii agizo la kwamba kama wapo na kazi ya serikali, wapitishe maombi yao kwa waajiri wao! Hii iliwagharinu ktk ukumbi wa interview!
- Ushamba na dharau! kuna walioambiwa watengeneze SLIDES not less than 10 ndani ya 1 hour, kwa topic aipendayo msailiwa, bado watanzania wenzangu, kuna wasailiwa waliandaa slides 3, wengine 2, kuna jamaa na Masters yake nje, aliandaa slide 1 tu, ya Mathematics! Katika dunia ya leo skills za computer ni muhimu sana, unamuelewaje mtu mwenye Masters ambaye hata kuandaa slide 10 ndani ya lisaa 1 hawezi!
- UREMBO! Kosa hili lilinishangaza sana. Kuna bidada, msailiwa alikuwa mrembo, na alikuwa na mvuto kusema ukweli. Panel ilikuwa na wanaume wote, watano, sasa sijui yeye alikuwa na akili gani kichwani mwake kuhusu wanaume sisi, wakati woote wa maswali ya oral alikuwa na pozi, sijawahi ona hapa Dsm! Pozi mbele ya interview panel. Alikuwa anafanyiwa usaili wa kuwa assistant tutor, aisee wakati anapresent, tulikoma na swaga zake! mara kashika nywele, mara min kaivuta juu, mara kavua miwani, mara kaivaa! mara ananyata pale mbele, mara hereni zinawasha! mara scarf sijui inalegea, sijui inabana shingo! Tulitamani amalize dakika zake 30, aende zake!
- Muda! Kama kawaida yetu! wapo waliochelewa, na walipofahamishwa kuwa wamechelewa wakaanza kwa kuangua vilio!
- Mara nyingi, kila mwisho wa interview, msailiwa huulizwa kama ana swali ama maoni kwa panel! wengi hawakuuliza swali wala kutoa maoni yao! Kilinivutia kitu kimoja, wachache waliouliza, walikuwa wanaulizia maslahi na hasa Mshahara! Kwamba mshahara ni Tshs ngapi na kama kuna marupurupu mengine! Sikuweza kuelewa mara 1 kuwa walikuwa wana maana gani (mtanisamehe kama mimi nimewaelewa vibaya) kutaka kujua mshahara, kwa mimi nijuavyo, mshahara wa serikali huwa hauna room ya kubargain, sasa kama alishaapply, akafanya interview ya kwanza, na akaja interview ya pili, swali hili sikuweza kujuwa logic yake hata!
WaTanganyika wenzangu na hasa, wale wanaotafuta kazi za serikali, naomba tuwe makini na hizi mambo, maisha ya mtaaani ni magumu, wasio na ajira ni wengi sana, tupunguze masihara na mizaha yetu tuliozoea, tuongeze umakini katika hili!
Mwenye sikio na asikie!